Rais Magufuli afanya mazungumzo na msomi Prof Patrick Loch Otieno Lumumba, msomi huyu ammwagia sifa lukuki Dr Magufuli

Rais Magufuli afanya mazungumzo na msomi Prof Patrick Loch Otieno Lumumba, msomi huyu ammwagia sifa lukuki Dr Magufuli

Pro Lumumba ana imani na Dr.Magufuli kwenye sera ya MAGULIFICATION anataka Magu agombee uraisi kwa kipindi kingine.
 
Oyaa. Hii Bara bara ya bagamoyo pale mapinga.mbona wameichimba chimba tu alafu wameitelekeza?
Kuanzia pale mapinga mpaka kwa kibosha.
Au mpunga umekataa?
Sasa hivi wameweka zile kokoto nyeusi tena kwa mafungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpunga haujakata bwashee........ Ile itachongwa hadi njia panda ya Vikawe na kandarasi yuko site ameshalipwa anachostahili!
 
Magulification of Africa imefungulia milango ya ikulu the bard of Nairobi.😎
 
1582615473131.png


MSOMI na mwanamajumui wa Afrika (Pan-Afranist), Profesa Patrick Lumumba amesema Rais Dk John Magufuli ni mfano wa kuigwa kutokana na uongozi wake wa kupigania rasilimali za nchi ikiwemo madini, kujenga nidhamu ya utumishi na kuimarisha uchumi.

Amesema Rais Magufuli ameweza kupambana vyema na wizi wa mali za umma, rushwa na ufisadi. Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya aliyasema hayo alipokutana na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam ambapo alisisitiza kuwa nchi zote za Afrika hazina budi kujifunza yanayofanyika Tanzania kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu jana, Gerson Msigwa, Profesa Lumumba amesema ni muhimu kwa Waafrika kijiamini na kuchukua hatua madhubuti za kuwaondoa katika hali ya sasa ambapo rasilimali zake zinachukuliwa na mataifa ya nje ilihali wananchi wake wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Rais Magufuli alimpongeza Profesa Lumumba kwa juhudi zake za kueleza wazi makosa ambayo yamekuwa yakisababisha nchi za Afrika kuendelea kubaki nyuma kiuchumi, kijamii na kisiasa na wajibu wa viongozi pamoja na wananchi wa Afrika katika kukabiliana changamoto zinazozikabili nchi zao.

Rais alimweleza Profesa Lumumba juhudi ambazo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wake imekuwa ikifanya katika kujenga uchumi imara wa kujitegemea ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme.

Nyingine ni kuongeza usambazaji wa umeme kutoka vijiji 2,018 hadi kufikia vijiji 8,587, ujenzi wa barabara na madaraja makubwa na madogo, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kuongeza ukusanyaji wa mapato, kudhibiti rasilimali muhimu kama madini pamoja na kupambana na ufisadi na rushwa. “Mimi sijawahi kukutana nawe kabla, lakini nakusikia na kukuona kupitia vyombo vya habari jinsi unavyopaza sauti kuhusu Bara la Afrika, nakupongeza kwa juhudi hizo, na ninafarijika kwamba unaisema vizuri Afrika,” alisema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli alikutana na Mwakilishi wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, anayeshughulikia masuala ya Afrika, Guenter Nooke, Ikulu, Dar es Salaam jana.

Nooke naye alimpongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa za maendeleo zilizofikiwa ikilinganishwa na nyakati za nyuma. Alisema Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji, biashara na masuala mengine ya kijamii. Rais Magufuli alisema serikali yake iko tayari kuendeleza ushirikiano wa kihistoria na Ujerumani na kuwaalika wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
 
Msomi wa sheria Africa amesema mi nani hadi nibishe

Kuna baadhi ya wasomi washeria Tanzania kazi yao kuropoka tu
 
Halo wana JF.

Kuna tetesi nimepata kutoka chanzo nyeti serikalini, kuwa Professor Patrick Lomomba maarufu PLO wa nchini Kenya, atapewa uraia wa Tanzania siku yoyote ndani ya mwezi march 2020.

Lomomba ni msemaji hodari yaani kwa kingereza good orator. Amekuwa mshambuliaji mkuu wa mabeberu kwa kutetea raslimali za Africa na pia mfuasi mkubwa wa Rais Magufuli. Anaandaa kitabu cha The Magufulication of Africa.

Inadaiwa ktk tetesi hizo atakabidhiwa idara nyeti ya kupambana na ufisadi humu nchini Tanzania lakini inadaiwa wahafidhina serikalini ambao hawaamini watani wetu wa Kenya, wanapendekeza kama serikali imempenda gwiji hili la sayansi ya siasa, wampe chuo kikuu kimoja wapo nchini awe Vice Chancellor.

Naendelea kutafuta ukweli wa tetesi hii kabla muda haujaongea mwezi march 2020.
 
Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili, je ataukana u-Kenya?

Halafu akipewa uraia asipewe ajira nyeti kihasara hivyo, watanzania wengi sana wamemzidi iq. Kwa nini afike tuu na kupewa ajira wakati watanzania kibao wanasota mtaani bila ajira!

Unforgetable
 
Hiyo habari haina ukweli wo wote. Hata wakati wa BWM kuna Profesor wa uchumi aliletwa na akatoa lectures nyingi tu pale Karimjee. Nadhani alikuwa anatoka nchi ya Brazil.
 
Back
Top Bottom