Halo wana JF.
Kuna tetesi nimepata kutoka chanzo nyeti serikalini, kuwa Professor Patrick Lomomba maarufu PLO wa nchini Kenya, atapewa uraia wa Tanzania siku yoyote ndani ya mwezi march 2020.
Lomomba ni msemaji hodari yaani kwa kingereza good orator. Amekuwa mshambuliaji mkuu wa mabeberu kwa kutetea raslimali za Africa na pia mfuasi mkubwa wa Rais Magufuli. Anaandaa kitabu cha The Magufulication of Africa.
Inadaiwa ktk tetesi hizo atakabidhiwa idara nyeti ya kupambana na ufisadi humu nchini Tanzania lakini inadaiwa wahafidhina serikalini ambao hawaamini watani wetu wa Kenya, wanapendekeza kama serikali imempenda gwiji hili la sayansi ya siasa, wampe chuo kikuu kimoja wapo nchini awe Vice Chancellor.
Naendelea kutafuta ukweli wa tetesi hii kabla muda haujaongea mwezi march 2020.