Rais Magufuli ajibu hoja za Marekani, Asijifiche kwenye hoja za uzalendo, Kwanza sio Mzalendo

Rais Magufuli ajibu hoja za Marekani, Asijifiche kwenye hoja za uzalendo, Kwanza sio Mzalendo

Mkuu wewe ni mmoja wa watu ninaowaheshimu hapa jf kutokana na uwezo wako wa kujenga hoja... Pia hoja yako nakubaliana nayo japo sio 100%....Sisi bado hatujafikia uwezo wa kuuona ubaya wa marekani... Bado tunamuona kama mtu mzuri kwetu kutokana na misaada yake... Tumekuwa tukiangaliwa sana na marekani kwa siku za karibuni hasa kutokana na baadhi ya mambo uliyoyataja hapo juu..in general tuseme haki za binadamu...Lakini tujiulize huyu tunayemuangalia kama kioo kwa upande wa haki za binadamu anafuata kweli hiyo misingi ya haki za binadamu? US haoni shida kumpoteza mtu asiye mwananchi wake au anayeingilia masirahi yake... Kama angekuwa anafuata misingi ya hizo haki basi asingewatishia majaji na officials wa ICC kuwawekea vikwazo na kuwapiga pini wasiingie US kama wangeendelea na uchunguzi wao wa kesi ya askari wa marekani nchini afaghanistan...huyu mtu yupo kimasirahi zaidi... Note sipingani nawe,nakubali kwamba demokrasia nchini imeshuka....But si sahihi kabisa kuanza kumtegemea na kumpigia magoti US eti aingilie mambo yetu ya ndani... Yaani to the extent rais ainuke ajitetee kwenye media!!! Mimi sikubaliana nalo... Au unasemaje kiongozi?
Una hoja nzuri. Lakini kwa namna nyingine, tujitafakari, nani aliyesababisha tuingiliwe?

Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kama unafukuzwa na jambazi mwenye jambia ili uawe, mbele ukakutana na jamaa anayelaumiwa kwa ubabe, ana bunduki, akakuuliza unakimbia nini, nawe ukamwambia kuna jambazi ana jambia anataka kuniua. Yule mbabe akasema kaa hapa pembeni yangu, huyo jambazi nitapambana naye mimi, kwa mazingira hayo, utamwonaje yule mbabe? Utamwona kama mkombozi, mkorofi, mwonezi au mdhulumaji?
 
Hoja za marais wa Marekani atazijibu nani?
Marekani haijamtuma mtu kuua watu kufunga watu na kuteka watu hapana, Marekani haijatuma mtu kuwashambulia watu kwa risasi hapana, Marekani haijamtuma kuzima vyombo vya habari na kuzuia siasa kwa wapinzani kwa miaka 5 hapana,

Kama serikali haijawatuma hao watu kwanini hafanyi upelelezi kuleta mlejesho? kwanini hawakamatwi watekaji? wauaji na wanaopiga risasi?

Eti hoja ni kwa vile kadhibiti madini yasiibiwe hoja ya kipumbavu kweli nawapa somo tu wafuasi mnaoamini izi propaganda kutoka Ikulu ya Magufuli, hakuna nchi iliyodhibiti rasilimali zake kama Botswana lakini huwezi sikia wanapambana na upinzani.

Na huwezi sikia Marekani ikiwanyoshea kidole halafu eti unasema umedhibiti madini yapi yale ya twiga 84/16 upo serious kweli? unachekesha kweli ! jibu hoja za Marekani.

Umeyakoroga mwenyewe yanywe mwenyewe hakuna atakayekubeba uvune ulichopanda nakuhakikishia uchomoki uchaguzi mwaka huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnatia kichefuchefu kumuona marekani kama ndo standard unit wa kulinda haki za binadamu wakati dunia nzima inajua the opposite is true.
Kauwa wangapi inocent kuliko hata Lisu?
Leo akikohoa tu mnakimbilia JF kuanzisha thread kama vile Mungu kakohoa?
Mengine mnajidharilisha tu makamanda.
Huoni hadi Jiwe kamtuma Kabudi huko
Malikani kujieleza!So relax,hata Rais wako anajua Malikani ni nani!
 
Vizuri unavyojifariji,inakubalika kitaalam ili kupunguza uwezekano wa kufa ghafla endelea kuwaza tu magufuli hachomoki
Amejiandaa kisaikolojia amehamishia mali rwanda!wewe kidampa utakimbilia wapi ? Kabla hatujaila hiyo tigo !
 
Yaani we ndio kichefuchefu full. Mtunyanyase kisa ulimbukeni wa madaraka kisha mtuambie Marekani hana rekodi ya haki za binadamu? Hata kama hana sifa nzuri za haki za binadamu, ili mradi anaingilia sisi kurudishwa kwenye mfumo bwana chama kimoja kimabavu, tunamuunga mkono.

Hii Serikali na CCM ya Magufuli ni malimbukeni wa madaraka!
Ni kichekesho kudai kuwa Mmarekani ATI Hana rekodi ya Haki za binadamu ilhali Serikali hii inapokea misaada ya kuhudumia wagonjwa wa UKIMWI kupitia TACAIDS....! Serikali hii inapokea misaada ya kifedha kwenye Elimu,Afya,Utawala Bora,UCHAGUZI Mkuu n.k. kupitia USAID....!
Misaada yote hiyo ni kwa ajili ya HAKI ZA BINADAMU.....! Sasa inakuwaje Marekani akihoji kuhusu Serikali ya CCM kubaka DEMOKRASIA kwa kuwaonea na kuwagandamiza CHADEMA na vyama vingine va Siasa??!!
 
Marekani alikataa mkataba wa mahaka ya makosa ya haki za binadamu na inajisifu kumuua Sulemani.

Imekataa mkataba unaozuia uharibifu wa mazingira lakini inaona wivu kwa Tanzania kujenga chanzo cha umeme na barabara ya lami Karatu-Musoma.

Sishabikii Magu lkn Marekani si nchi ya kurejea.
Ukiwekewa vikwazo ndo akili zitakaa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chochote kilicho nyuma ya pazia watanzania walio wengi wamekubali aje alitoe jiwe.
Wewe marekani ni nani kwako... Wewe anaweza jibu hoja zako... Katiba yetu inamtambua mtu anaitwa mmarekani hadi rais wetu ajibu hoja... Au unafikiri marekani ana urafiki na wewe.? Ungejua ya nyuma ya pazia ya marekani wala usingeongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mara mia kuwa brainwashed na marekani kuliko kuwa brainwashed na ccm, jiangalie alafu toa comments
We la Marekani hulioni unaona la Tanzania tu?
Hivi kwenye haki za binadamu unaweza kumquote Marekani kweli?
Mmekuwa brainwashed utafikiri hamjasoma?
Mnatia kichefuchefu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani haijamtuma mtu kuua watu kufunga watu na kuteka watu hapana, Marekani haijatuma mtu kuwashambulia watu kwa risasi hapana, Marekani haijamtuma kuzima vyombo vya habari na kuzuia siasa kwa wapinzani kwa miaka 5 hapana,

Kama serikali haijawatuma hao watu kwanini hafanyi upelelezi kuleta mlejesho? kwanini hawakamatwi watekaji? wauaji na wanaopiga risasi?

Eti hoja ni kwa vile kadhibiti madini yasiibiwe hoja ya kipumbavu kweli nawapa somo tu wafuasi mnaoamini izi propaganda kutoka Ikulu ya Magufuli, hakuna nchi iliyodhibiti rasilimali zake kama Botswana lakini huwezi sikia wanapambana na upinzani.

Na huwezi sikia Marekani ikiwanyoshea kidole halafu eti unasema umedhibiti madini yapi yale ya twiga 84/16 upo serious kweli? unachekesha kweli ! jibu hoja za Marekani.

Umeyakoroga mwenyewe yanywe mwenyewe hakuna atakayekubeba uvune ulichopanda nakuhakikishia uchomoki uchaguzi mwaka huu.
Nimeshangaa sana kwa hoja zilizotolewa...
Musiba alitangaza watu anaodhani wanatakiwa kuuwawa, lakini hakuna hata mmoja aliyesikika kuchukua hatua, ILA ALIPOSEMA TU KUWA NA YEYE AMETISHIWA KUUWAWA, polisi walimwita... SAS KWENYE HILI SIJUI MAREKENI WASEME NINI..
 
Una hoja nzuri. Lakini kwa namna nyingine, tujitafakari, nani aliyesababisha tuingiliwe?

Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kama unafukuzwa na jambazi mwenye jambia ili uawe, mbele ukakutana na jamaa anayelaumiwa kwa ubabe, ana bunduki, akakuuliza unakimbia nini, nawe ukamwambia kuna jambazi ana jambia anataka kuniua. Yule mbabe akasema kaa hapa pembeni yangu, huyo jambazi nitapambana naye mimi, kwa mazingira hayo, utamwonaje yule mbabe? Utamwona kama mkombozi, mkorofi, mwonezi au mdhulumaji?
Hapo nimekupata kiongozi.
 
Back
Top Bottom