Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Una hoja nzuri. Lakini kwa namna nyingine, tujitafakari, nani aliyesababisha tuingiliwe?Mkuu wewe ni mmoja wa watu ninaowaheshimu hapa jf kutokana na uwezo wako wa kujenga hoja... Pia hoja yako nakubaliana nayo japo sio 100%....Sisi bado hatujafikia uwezo wa kuuona ubaya wa marekani... Bado tunamuona kama mtu mzuri kwetu kutokana na misaada yake... Tumekuwa tukiangaliwa sana na marekani kwa siku za karibuni hasa kutokana na baadhi ya mambo uliyoyataja hapo juu..in general tuseme haki za binadamu...Lakini tujiulize huyu tunayemuangalia kama kioo kwa upande wa haki za binadamu anafuata kweli hiyo misingi ya haki za binadamu? US haoni shida kumpoteza mtu asiye mwananchi wake au anayeingilia masirahi yake... Kama angekuwa anafuata misingi ya hizo haki basi asingewatishia majaji na officials wa ICC kuwawekea vikwazo na kuwapiga pini wasiingie US kama wangeendelea na uchunguzi wao wa kesi ya askari wa marekani nchini afaghanistan...huyu mtu yupo kimasirahi zaidi... Note sipingani nawe,nakubali kwamba demokrasia nchini imeshuka....But si sahihi kabisa kuanza kumtegemea na kumpigia magoti US eti aingilie mambo yetu ya ndani... Yaani to the extent rais ainuke ajitetee kwenye media!!! Mimi sikubaliana nalo... Au unasemaje kiongozi?
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kama unafukuzwa na jambazi mwenye jambia ili uawe, mbele ukakutana na jamaa anayelaumiwa kwa ubabe, ana bunduki, akakuuliza unakimbia nini, nawe ukamwambia kuna jambazi ana jambia anataka kuniua. Yule mbabe akasema kaa hapa pembeni yangu, huyo jambazi nitapambana naye mimi, kwa mazingira hayo, utamwonaje yule mbabe? Utamwona kama mkombozi, mkorofi, mwonezi au mdhulumaji?