Rais Magufuli amteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi nchini Uingereza

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

04 Mei, 2016
 
Ilishavujishwa humu lakini kukubali nafasi hii kwa Prof ni kujishushia heshima
 
Reactions: Gut
Hawa jamaa hawana hoja kabisa. Hata Putin alitoka uraisi na kumuachia Medvedev, yeye akawa waziri mkuu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

04 Mei, 2016
 
Kila la heri katika makazi yake mapya.
 
Hivi balozi anayerudishwa nyumbani maana yake ni nini??
Kuna majukumu mengine anapewa au ndio kustaafu moja kwa moja??
 
Kasalia dau kuwa balozi segerea,migiro kapewa ili kapunguza upupu kamati kuu CCM,magufuli ni mjanja atapokabidhiwa CCM rasmi atakuwa amewamaliza wote,kaa mzee wa nyara keshajipoteza mwenyewe
 
huyu mama amefanya kazi toka enzi za nyerere kwani hamna wana CCM wengine.ifike hatua watu wawe wanapumzika
 
hiv balozi akirudishwa nchin ina maana kuwa utumishi wake umekoma au? Mana baloz wetu nchin uingereza amerdishwa nyumban na leo hii nimeskia Dr. Asha migiro kateuliwa na kesho ataapishwa kuchukua nafasi hyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…