Ndio maana nikasema kuna moja kati haya mambo mawili
- Aidha muwekezaji amewekewa figisu, iwe kuna vitu mnaongeza tu ili kumkomoa, bora naye akapewa fursa azungumze na wana habari.
- Na kama ni kweli hayo masharti yalikua yamekubaliwa, basi Kikwete ni mtu asiyefaa hata kuongoza kama mjumbe wa nyumba kumi au kiogozi wa kata, maana hana huruma na nchi yake wala hata punje ya uzalendo, na pia CCM na uongozi wake wote ni hatari kubwa sana kwa nchi yenu, kwa tamaa yao walikua tayari kuiweka nchi rehani.
Maana haiwezekani ukatia saini mkataba unaosema bandari zote ulizonazo zisiendelezwe, hiyo yote kwa ajili ya bandari mpya kubwa ambayo hutakua na mamlaka nayo kwa miaka yote hiyo, hivyo humo watakua na ruhusa ya kufanya yao bila kukuhusisha, watapitisha chochote hum bila ya uhusika wa serikali ya Tanzania, hayo ni maamuzi ya kuifilisi nchi ambayo yenyewe tayari ni maskini.
Ni maamuzi ambayo hata sidhani kama enzi za ukoloni mababu zetu wangeyakubali pamoja na kwamba hawakua na elimu wala ujuzi. Waliohusika kwenye maamuzi ya kihivyo wote wanafaa wakusanywe na kushtakiwa uhaini.
Tatizo kubwa nchi yenu hiyo mumeingia kwenye ubepari kichwa nje nje bila hata kujua mfumo wenyewe unaendeshwa vipi, nyote mumekua na tamaa za kiajabu ajabu, hebu sikiliza hiyo hotuba ya rais, kwamba hata waliofidiwa kwenye ardhi ya Bagamoyo walikua makajanja wa Dar, sio wakazi wa Bagamoyo.