Bahati mbaya sana wametuletea mtu ambaye ni 'crude oil'. Jamaa mzuri sana wala sio kidogo lakini hakuandaliwa na hasa kwenye yafuatayo;
1. Emotional Intelligence( tafsiri ya kubahatisha ni uwezo wa kihisia(akili ya kihisia))
2. Kiongozi huongoza na kisha wafuasi wanamfuata (Leadership by influence and not by coercion)
3. Kuwa msikivu zaidi kuliko kuongea. Na kufanya 'informed decision'(maamuzi baada ya kupata taarifa ya kutosha)
4. 'what goes around comes around' (Alichopanda Nape Nnauye, sasa hivi amekivuna, Hata Lowassa amevuna tayari, sasa na yeye atakuja kuvuna tu..)
5. Hatari ya 'double standards', historia itamkumbuka Magufuli kwa kumtetea mtu aliyesoma kwa jina la mtu mwingine baada ya kufeli(Kufoji vyeti) na huku kuna maelfu waliofukuzwa kazi, wengine hawana kazi, wengine wamefungwa kwa sababu ya kufoji vyeti au kutumia majina ya wengine. Akumbuke hotuba yake kule bandarini kuhusu vyeti feki na ndipo azungumzie kuhusu 'msema kweli ni mpenzi waMungu'. Asifikiri Mungu ni Makonda.Mungu hadhihakiwi.
6. "You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time." - Abraham Lincoln
7. Bila kulindwa na Mungu, huyounayemwamini sana kwamba anakulinda ndiye atakayekuua. Hivyo usijiamini sana. Utende haki ambayo ni haki kweli na Mungu atakulinda. Lakini unachofanya sasa, ni hatari sana hata kwako.
CCM wameacha viongozi walioandaliwa, wakatumia kamari kupata Rais. Matokeo yake tuna mgonjwa wa hisia anatutawala. Magufuli sio mgonjwa wa akili ya kawaida kama wengi wanavyosema. Ila ana 0% emotional intelligence.
Kiongozi bora ni yule mwenye si chini ya 70% emotional intelligence.