Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Nikikumbuka kuanzia bunge la katiba. Mara kwenye serikali ya JPM alivyobadilika. Unafki unalipa. Hivi nyie mnaolalamika hamna kazi mbona fursa zipo pale Lumumba. Au hamna number ya Magufuli niwape ????Hongera Polepole ukale keki ya taifa waziri wa utalii na maliasili.
Wanakula cake bila furaha.Sitaki aina hiyo ya maisha.
 
Riziki Lulida Naibu atateuliwa kuwa Naibu Waziri ofisi ya Rais Kazi ,Sera uratibu na bunge anae shughulikia Watu wenye ulemavu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
View attachment 1637284
Hapo chura kapigwa teke!
Sasa Polepole aione siasa live.
 
Nilitegema hii nafasi atapewa Hamisi Mwinjuma, Mwana FA. Kwakuwa kama kusoma kasoma, na alikuwa kwenye mfumo huo huko Basata na ni msanii pia

Kwenye hiyo Wizara muziki ni sehemu tu, kuna mengi zaidi, kuwa mwanamuziki siyo kila kitu, ...
 
Kwenye hiyo Wizara muziki ni sehemu tu, kuna mengi zaidi, kuwa mwanamuziki siyo kila kitu, ...
Lakini kasoma kama Juliana Shonza aliweza kuwa naibu mwana FA uwaziri atauweza
 
Wameanza kugawana madaraka Kama njugu.
Wale waliomkaribisha lisu kwao wakamruhusu alale wasahau.
 
Back
Top Bottom