Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Ahaaaa tutaona mengi huwezi kupata wazo kanisani na hela ya kutoa mfukoni hapo hapo. Labda tuwaambie wasio jua mnakumbuka kipindi cha kikwete na mkapa kulikuwa na hoja nyingi bungeni wabunge wakihoji ahadi ya rais mbona haijatimizwa. Nini kina tokea rais anaweza kufika sehemu akakutana na changamoto fulani kitu anachotakiwa Kufanya nilutoa ahadi mimi nitasaidia au kuchangia kiasi fulani cha fedha hiyo huchukuliwa ni kauli ya serikali na kwamba serikali imeahidi na na waziri husika wa hicho kitu au wasaidizi wa rais huchukua hilo na kulifanyia kazi. Huwezi kukuta mkapa au kikwete wakatoa fedha hapo hapo kwa jambo hata hawakutarajia kukutana nalo.Ndio maana kipindi hiki watu tunafika mahali tunaona vitu vya ajabu kutokea rais anaongea na mtu au raia ana sema mimi nitachangia milioni kadhaa halafu anamwambia msaidizi wake nipe millioni tano hapo msaidizi anakuwa na milioni tano za nini? Na zinatoka kama zilivyo zimefungwaa wala hakuna mda wa kuhesabu kama zimetimia au zilizidi zipungue hizi kweli hapo unahitaji uwe na diploma kujua hicho kitu?
Mbona wengi tu wametoa walizokuwa nazo na kuahidi kutoa zilizosalia? Naona mkuu unahangaika na pesa chini ya millioni moja. FYI hizo watu wanatembea nazo mfukoni. Mimi nikiwa bongo mfukoni sitembei na chini ya millioni tatu. BTW mapadri wa Tanzania hili nakupa kwa uzoefu wangu hawatembei bila kuwa na pesa kwa sababu huwa wanakuwa na pesa za chap chap kwa ajili ya kusaidia mara dharura inapotokea. For JPM anatembea na pesa nyingi tu hiyo ni tabia yake kama hupendi nenda kajinyonge.
 
Ndugu Rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inayofaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
 
BAKWATA ni kama taasisi ya serikali. Na Magufuli ni kiongozi mkuu wa serikali. Sio vibaya kiongozi wa serikali kuisaidia taasisi yake

Wale waislam wenyewe kabisa, wataiunga mkono hoja yako. Ila IslamCCM watakupiga madongo sana bwana mleta hoja...

Jaribu kupiga picha msikiti unajengwa na mchango wa mgalatia kwa fedha alizopata faida kwenye biashara ya kitimoto...
 
Rais, Askofu Mkuu na Katibu wao TEC ni full maigizo. Wameleta kinyaa. Watumie hizo fedha sasa kununua vifaa vyao kanisani Kama kinanda kikubwa, viti, mabenchi na hata Noah ya Paroko kuliko kuharibu Sunnah ya misikiti wa kiislamu.

Noah ya paroko? Mtumbaa? Paroko gari ya chini ameendesha Toyota hilux 2020 millioni 150.
 
Kingine sina Hakika kama Mungu wa waislamu ndo Mungu wa Wakristo.

Hapa mtu unaweza ukajikuta unachuma dhambi bila kujua.

Sisi wakristo tunajua Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu. Siwezi kuchangia ujenzi wa msikiti au ujenzi wa shaulin temple ili Mungu mwingine aka abudiwe. Kwa imani yangu iyo ni dhambi.
 
Nikifikiria jinsi waislamu wanavyotuonaga wala kitimoto halafu ndo tunawachangia kujenga msikiti, nacheka sana aisee

Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kuwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!

Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!
 
Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kiwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!

Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!
Japo kuchangiana ni jambo jema ila muktadha wa tukio haukua sahihi.

Ni aibu sana kwa waislamu
 
Back
Top Bottom