Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Mkuu katika hili umesoma vizuri? Au mimi kuna sentensi sikuziona? Sijaona akizungumzia suala la kanisa kuwa karibu na msikiti. Hii ipo hata Daslama pale Magomeni ambapo upande wa pili kuna kanisa. Nilichokiona anzungumzia Magufuli, rais wa jamhuri, kuwaombea waislamu mchango wa kujenga msikiti. Maombi yenyewe yaliyofanywa kwa wakristo ndani au katika maeneo ya nyumba yao ya ibada na zaidi wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Mleta mada anao ujumbe uliojificha, nimeutambua ndio maana maoni yangu yapo hivyo kama ulivyoyasoma.
 
Mi naona rais hajakosea kitu maana anapofanya harambee za ghafla iwe kumsaidia kwa mfano yule mama kilema pale ubungo flyover kila msaidizi wake anachangia. Akichangisha kanisani wote wasaidizi wake bila kujali dini wanatoa. Kama rais amejihusisha kujengwa kanisa eneo la ikulu hivyohivyo amejihusisha kuchangisha kwa msikiti wa eneo la ikulu. Utamaduni wa watanzania kuchangiana kwa ujenzi nyumba za ibada umeanza siku nyingi na hii ni moja ya sifa za watanzania.

Asante kwa maoni yenye kuongozwa na ubinadamu 🙏🏿.
 
Mi naona rais hajakosea kitu maana anapofanya harambee za ghafla iwe kumsaidia kwa mfano yule mama kilema pale ubungo flyover kila msaidizi wake anachangia. Akichangisha kanisani wote wasaidizi wake bila kujali dini wanatoa. Kama rais amejihusisha kujengwa kanisa eneo la ikulu hivyohivyo amejihusisha kuchangisha kwa msikiti wa eneo la ikulu. Utamaduni wa watanzania kuchangiana kwa ujenzi nyumba za ibada umeanza siku nyingi na hii ni moja ya sifa za watanzania.
Kilema[emoji3582]
Mlemavu[emoji3581]
 
Ukisoma between lines - mwandishi - Ana chuki isiyopimika dhidi ya wakatoliki.
Mwandishi anaumia sana kumuona Rais anatoa sadaka kanisani.
Hili la kuchangiana si hoja yake ya msingi. Ila imempa upenyo tu kuventi chuki yake dhidi ya wakatoliki.
Rais ni kiongozi wa nchi. Anaongoza wakristo, waislam na hata wasio na dini.
Ana jukumu la kuwaunganisha wote waishi kindugu, kuthaminiana, kuheshimiana na kusaidiana.
Mwandishi asingetumia chuki yake dhidi ya ukatoliki angeweza kuiona dhamira njema ya Rais kutuunganisha na kutufanya tuishi kitanzania - tukipendana na kushirikiana bila kujali tofauti zetu kiimani, kikabila nk.
Sisi ni WATANZANIA na ni NDUGU.

Nyerere aliongoza shughuli nyingi tu za waislam.

Mkapa akahakikisha wanakuwa na chuo pale Morogoro.

Magufuli akichangisha sadaka maalum tayari inakuwa nongwa!.
 
Nimesoma hadi mwisho sijaruka kipengele chochote, japo sikujua kinachoendelea lakini umeelezea vizuri nikapata mwanga,

Binafsi nakazia kwa msumari yote uliyoyaandika, Dini isichanganywe na Siasa.
Rais angeitisha harambee msikitini kisha angalia rafiki zake waislam na wasio waislam nakutumia platform ya waislam(jukwaa la waislam) hapo angekuwa sahihi
 
Sasa John, imagine wakiristo waombwe kanisani kujenga nyumba ya ibada ya "wapagani", huoni kuwa hilo nalo pia ni kuwakwaza wakiristo?
Yesu alitutaka tumuahidi kwamba arudipo mara ya pili aikute amani duniani, ujenzi wa nyumba za ibada ni sehemu ya kuitengeneza amani!
 
Msikiti upi hapa nchini ulijengwa kwa michango ya wakiristo ukiachilia mbali huu ambao Magufuli anataka kiki za kisiasa?
Yani mingi sana mimi binafsi nimechangia, kuna msikiti Muhimbili, Kijitonyama Masjid Kuba, Mwananyamala kwa mama Zakaria, Mwenge kijijini huo nilichangia pesa ya harambee.

Bukoba mjini hamgembe huu sijui kama ulijengwa tayari, maana eneo walilotaka kujenga lilikuwa na migogoro.

Kuna ki msikiti Bunju B kule Mbatia aliuza viwanja nilichangia.

Hahaha ukiwa unaswali hiyo misikiti kumbuka nami niliichangia.
 
Mi naona rais hajakosea kitu maana anapofanya harambee za ghafla iwe kumsaidia kwa mfano yule mama kilema pale ubungo flyover kila msaidizi wake anachangia. Akichangisha kanisani wote wasaidizi wake bila kujali dini wanatoa. Kama rais amejihusisha kujengwa kanisa eneo la ikulu hivyohivyo amejihusisha kuchangisha kwa msikiti wa eneo la ikulu. Utamaduni wa watanzania kuchangiana kwa ujenzi nyumba za ibada umeanza siku nyingi na hii ni moja ya sifa za watanzania.

Waislamu wao wenyewe hawajashindwa kujenga msikiti huko Ikulu ya Chamwino.
Haihitajiki harambee za kanisani kujenga msikiti wa waislamu!. Yeye atoe tu eneo kisha awaachie waislamu wenyewe wafanye mchakato wa ujenzi, wskitaka kumshirikisha watamshirikisha

Mbona wakati anajenga kanisa hilo hakuomba harambee za waislamu?

Au anataka baadae, Waislamu wasimangwe kuwa hata huo msikiti wenu ndani ya Ikulu yetu ya dodoma ulijengwa kwa sadaka za Wakiristo?
 
Yani mingi sana mimi binafsi nimechangia, kuna msikiti Muhimbili, Kijitonyama Masjid Kuba, Mwananyamala kwa mama Zakaria, Mwenge kijijini huo nilichangia pesa ya harambee.

Bukoba mjini hamgembe huu sijui kama ulijengwa tayari, maana eneo walilotaka kujenga lilikuwa na migogoro.

Kunavki msikiti Bunju B kule Mbatia aliuza viwanja nilichangia.

Hahaha ukiwa unaswali hiyo misikiti kumbuka nami niliichangia.

Harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti mliifanyia kanisa gani na ilisimamiwa na padri au baba askofu gani?
 
Amabao hatuna mungu wala uchawi tutaishi vibaya sana hii nchi
 
Msaidizi wake ni Alhaj na kiubinadamu anajisikia vibaya kuwa na waislam kadhaa kanisani halafu wasiwe na msikiti katika eneo lao la kazi.

Samia Suluhu, Kassim Majaliwa na wengine wasaidizi wa karibu ni waislam hivyo mkumbuke umuhimu wao kwake kimaisha.

Msiongozwe na chuki mpaka mkapoteza uwezo wa kuyatafakari masuala ya kawaida kabisa ya kiubinadamu.

Hapo Chamwino ni sehemu ya Dodoma na ni makao makuu kutakuwa na ongezeko la waislam miaka ijayo.
Wenye dini yao wala hawana tatizo na hilo suala la michango. Nchi yetu sote hii na wala sio mara ya kwanza kuchangiana ujenzi wa makanisa na misikiti. Tatizo kila jambo linachanganywa na siasa.

Ni juzi tu Joketi Mwogelo Mkuu wa Wilaya Kisarawe amechagua ujenzi wa Msikiti na Waislamu wenyewe wamechagua kuwa mlezi wa kamati ya ujenzi.
 
Harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti mliifanyia kanisa gani na ilisimamiwa na padri au baba askogu gani?
Hahaha wewe unatafuta vita sasa, mwisho utaomba na cheque number ya mchango wangu.

Nimekwambia mimi nimechangia hiyo misikiti niliyokutajia.

Punguza jazba sito dai pesa yangu, nilitoa mchango kujenga nyumba ya ibada.

Nakumbuka msikiti wa mwenge kijijini tulichangia hadi zulia, waislamu wakampiga sheikh wa ule msikiti kwamba kala pesa iliyotoka uarabuni, tafrani lile hadi FFU walikuja kutuliza ghasia.

Hahaha huwa naguswa tu nachangia mkuu, usije susa kuswali bure.
 
majuzi TAG, sasa RC, bado bakwata na KKKT yote ni kuomba kura.
Lissu akienda utasikia kelele zitakavyopigwa na ccm na waliowaalika watasakamwa kwelikweli.
 
Back
Top Bottom