Wakati wa Mwalimu hata waliofuata dini ilikuwa ni 'taboo'' kuizungumzia katika mazingira ya kisiasa.
Sasa hivi tunaambiwa watu wasichanganye dini na siasa, lakini wanasiasa ni haki kuchanganya na dini.
Kiti kimoja cha ubunge wa Kawe hakina sababu zozote zile za kuweka amani ya nchi katika mstari.
Hili ni kosa kubwa sana na sijui huko ndani ya CCM hakuna mwenye jicho la kuona na uthubutu wa kukemea
Kinachotokea sasa hivi, Wagombea wote wa CCM bila kujali imani zao, kila wanaposimama mbele ya jamii wanasoma nyuso za wananchi hasa Waislam zikiwa na swali moja '' Haya ya Gwajima mumeyakubali''?
CCM hawana jibu, hawawezi kumkubali Gwajima na kukataa ujumbe wake.
Kauli zimetoka kwenye kinywa cha Gwajima! Zipo mitandaoni zinasomeka, ni chuki tu iliyothibitishwa na CCM
Kibaya zaidi CCM imefungua ''floodgate'' Utakmakamata vipi Sheikh Ponda kwa uchochezi halafu umzawadie Gwajima kwa Ubunge na jamii ikuelewe!!!
Kwa maneno mengine Sheikh Ponda amepata 'natural immunity'' Atasema chochote
Ukimkamata Sheikh Ponda utaulizwa, vipi Ponda enede Ukonga , Gwajima aende Dodoma?
Kuna tatizo kubwa sana sijui kwanini CCM hawalioni!
JokaKuu Pascal Mayalla