Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Yule ni Sheikh wa "kazi maalum" , walikuwepo watu wa aina yake toka zamani, kwa lugha ya waislam huwa wanaitwa wanafiki
Sasa ndiyo tutaona umuhimu wa watu kama marehemu Hassan Ilunga
(Allah amrehemu).
katika uislamu,hawa viongozi wa kibakwata wanatuaibisha Sana Sisi waislamu
 
Wakati wa ufunguzi wa kanisa huko miaka ya nyuma kijijini Butiama Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alitangaza rasmi kuwa angependelea kuona pale kijijini Butiama panajengwa Msikiti mkubwa. Kwa maombi yake kwa kiongozi wa Libya hayati Ghaddafy fedha za kujenga msikiti huo ulipatikana na msikiti huo ulijengwa kwa usimamizi wa ofisi ya Rais huyo mstafuu. Leo kwa mheshimiwa Rais Magufuli kuchangisha fedha ya kujenga msikiti pale sio kosa.
Mwache kupotosha vitu.
Nyerere alichangisha kanisani?
 
Kumbe wale maustaadhi wanaoombaga michango mbalimbali wanakosea kuomba kwa wakristo?!


Mfano tuwapo safarini kwenye mabasi, pale mkata Handeni kuna jamaa anaombaga mchango ya ujenzi wa msikiti sijui madrasa n.k

Leo umesaidia wengi aisee hawatakua wanachangia maswala yahusuyo dini ya kiislam.

Any Islamic related contributions,

Nazani na michango ya vituo vya watoto yatima wenye mlengo wa dini ya kiislam itabidi kuacha kuchangia maana kumbe mnakwazika!


Aisee hii siyo nongwa kweli jamani ?!


Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi!
 
..nadhani tunazunguka-zunguka bila kwenda kwenye MSINGI/KIINI cha tatizo.

..mimi nadhani Jpm ni mwanasiasa asiye na hoja na haiba ya uongozi, hivyo amekuwa akitumia makanisa na misikiti kufanya siasa.

..ili Jpm akubalike ni lazima apitie kwenye "uchochoro" wa imani za watu, akipitapita makanisani na misikitini huku akimwaga MAPESA.

..inawezekana kuna kasoro ndogo-ndogo namna ambavyo harambee iliitishwa, lakini msingi na kiini cha yote haya ni Jpm kutumia DINI na FEDHA ktk siasa.

cc tindo, Phillipo Bukililo , Kilatha, Nguruvi3
Ingelikuwa Magufuli hiyo tabia ya kuingia kanisani kaanza miezi miwili nyuma sawa. Lakini ana historia ya kwenda kanisani tangia utoto ndio maana kila alipoishi anawajua mapadre waliokuwa wakimsalisha.

Magufuli yeye mwenyewe anadai ilikuwa awe padre sema kanzu aikumtosha.

Ushiriki wa dini na Magufuli ni kwa sababu he is somewhat genuinely religious (but not pious) ushahidi huo upo tangia siku za mwanzo anaingia kwenye public eyes, ata jambo serious kama Corona yeye alitaka twende na Mungu badala ya sayansi inaonyesha ni namna gani alivyokuwa mtu mwenye imani kali isiyo na mashaka kwa mungu.

Kuomba harambee ya msikiti ndani kanisa inaweza kuwa ni self guilt tu kama raisi baada ya kuona kuna kanisa limepatikana kwa sababu ya harambee aliyoanzisha yeye.

Ni katika kujistukia tu baada kupewa habari kuna msikiti na wenyewe Chamwino unahitaji kuboreshwa. As a guesture of being neutral kama kiongozi wa nchi yenye watu wa dini zote ndio motive ya kuitisha harambee.

The whole thing is petty labda useme lime coincide na kipindi cha kutafuta support za watanzania na CDM kwa sababu hawana sera ndio wameamua kulikuza bila ya kufahamu kwa kufanya ivyo wanamjengea mileage Magufuli kila mtu kaona harambee was done innocently, with good intentions and nothing else.
 
Watu wa kitabu??? Hahahahaahahahahaha

Ahlul kitaab ni watu wa zaburi (ya kweli), injili (ya kweli) na tauraat (ya kweli).

Sio watu wa biblia mkuu hahahahaahahahhah
🙂🙂🙂
Maalim, niweke sawa hapa, ninachojua nikuwa Biblia imejumuisha zaburi, injili na tauraat za kweli. Sasa kunaubaya wowote watu wa biblia kuitwa watu wa "Ahlul kitaab"!?
 
Maoni yako ni sahihi ila jitahidi kupanua uelewa wako. Few months ago huko ujerumani waislam waliwaomba wakristu wawaruhusu waislam kufanya ibada ya ijumaa kanisani kwakuwa misikiti ilikuwa midogo kuruhusu social distancing because of covid. Waislam waliswalia kanisani
Ibada Ya Kiislam inaweza kufanyika popote alimradi YAFUATWE masharti ya swala!!
 
Mkuu,

Ya mzee Suleiman Takadir tuyaache ni machache mno na mengi yapo yanayoonyesha au kuthibitisha chuki za wakristo mbele ya waislam.

"Binafsi nadhani sio vizuri kujikita kwenye vitu tunavyohisi vinatugawa kwa kigezo cha dini hasa kwa vizazi vyetu vya sasa." Kuhusu hili mkuu sikubaliani nawe, hili tatizo ni lazima kuli-address ili litatuliwe. Kujifanya hatulioni na kupeana matumaini hewa kwamba hatuna ubaguzi nchini wetu haisaidii chochote. Linazidi kuziimarisha hizi chuki.

By the way nina marafiki wengi tu na wazuri ambao ni wakatoliki na tumesaidiana sana hapa duniani.
Ili kuli-adress inabidi hizo issues ambazo zinaonesha chuki ziwe outlined.
Sasa hizo issues zinazoonesha chuki ni zipi?
 
Ni malaya tu anae weza kuhoji hoji na kupinga pinga kila jambo wakati moyoni anapenda kwa dhati kabisa.

Enyi wanasiasa uchwara acheni tabia ya umalaya malaya.
 
Ndugu zangu , Amani iwe juu yenu pamekuwepo na madai na majitapo mengi kutoka kwa baadhi ya political laymen tangu jana baada ya baba mwenye nyumba kutembeza bakuli kanisani kuomba fedhwa za kujenga msikiti,

Hapo nina maswali mawili matatu.

Moja, Baba mwenye nyumba alitumwa na masheikh kuwaombea michango kanisani, bila shaka mamlaka za waislamu zitatujulisha.

Pili, Je ni upendo wa baba mwenye nyumba kwa wapangaji wake kutaka kuonesha religious equilibrium katika kipindi hiki cha kutafuta political pasture?, sina hakika sana kama iko hivyo.

Tatu, Ni uumini na uchamungu wa kiwango cha juu cha baba mwenye nyumba?, nadhani hili ni jibu sahihi.

Nne, Ni ipi hukumu ya kisheria katika dini ya uislamu kujenga msikiti kwa fedhwa ambazo yakinani zimetokea kanisani bila wasiwasi wowote?

Hapo maulama watatusaidia

Tano, Je hili halina athari yoyote kisiasa khasa wakati huu wa uchaguzi?

Sita, Ni lini msikt wa mfalme wa Moroko utazinduliwa nao waislamu wachangie kanisa?
Ni maswali muhimu na rais anahitaji kuongozwa sana, kama anaambilika. Yeye ni mwanasiasa na siyo vizuri kusaka umaarufu kupitia dini. Kama kweli ni mutafuta haki angewachangia ACT, CHADEMA, CUF TLP, nk. kwa wanachama wa CCM! Hii hadithi ya kusimama kanisqani na kujidai eti wakristu wana upendo wa kuwasaidia waislamu, ni uzembe wa kiwango fulani.
 
BAKWATA ni kama taasisi ya serikali. Na Magufuli ni kiongozi mkuu wa serikali. Sio vibaya kiongozi wa serikali kuisaidia taasisi yake

Wale waislam wenyewe kabisa, wataiunga mkono hoja yako. Ila IslamCCM watakupiga madongo sana bwana mleta hoja...

Jaribu kupiga picha msikiti unajengwa na mchango wa mgalatia kwa fedha alizopata faida kwenye biashara ya kitimoto...
Jaribu kujenga picha unaumwa hospitali na unahitaji kuongezewa damu, kisha anayetaka kujitolea damu ni jamaa fulani Mgalatia mla mbuzi katoliki!? Ila honestly anachofanya Rais hakikubaliki hata kidogo. Madaraja , mandege na matakataka mengine aliyonunua asiwe na wasiwasi yatampigia kura.
 
Mtu yoyote mwenye ukaribu na bashite lazima akili zai zifanane.
Muangalie lemutuz,steve nyerere,jerry muro etc..
Akili zao ndo hizi hizi
 
BAKWATA ni kama taasisi ya serikali. Na Magufuli ni kiongozi mkuu wa serikali. Sio vibaya kiongozi wa serikali kuisaidia taasisi yake

Wale waislam wenyewe kabisa, wataiunga mkono hoja yako. Ila IslamCCM watakupiga madongo sana bwana mleta hoja...

Jaribu kupiga picha msikiti unajengwa na mchango wa mgalatia kwa fedha alizopata faida kwenye biashara ya kitimoto...
Jaribu kujenga picha unaumwa hospitali na unahitaji kuongezewa damu, kisha anayetaka kujitolea damu ni jamaa fulani Mgalatia mla mbuzi katoliki!?

Ila honestly anachofanya Rais hakikubaliki hata kidogo. Madaraja , mandege na matakataka mengine aliyonunua asiwe na wasiwasi yatampigia kura.
 
Mwache kuleta fitina na chuki za kidini. Mheshimiwa Rais hakuwa na kosa lolote la kuchangisha pale kanisani
Katumwa na nani? Kama ana upendo na ni mwanasiasa, kwa nini hajaongoza wana CCM kuwachangia TLP, nk.?
 
Wakati wa Mwalimu hata waliofuata dini ilikuwa ni 'taboo'' kuizungumzia katika mazingira ya kisiasa.
Sasa hivi tunaambiwa watu wasichanganye dini na siasa, lakini wanasiasa ni haki kuchanganya na dini.

Kiti kimoja cha ubunge wa Kawe hakina sababu zozote zile za kuweka amani ya nchi katika mstari.
Hili ni kosa kubwa sana na sijui huko ndani ya CCM hakuna mwenye jicho la kuona na uthubutu wa kukemea

Kinachotokea sasa hivi, Wagombea wote wa CCM bila kujali imani zao, kila wanaposimama mbele ya jamii wanasoma nyuso za wananchi hasa Waislam zikiwa na swali moja '' Haya ya Gwajima mumeyakubali''?

CCM hawana jibu, hawawezi kumkubali Gwajima na kukataa ujumbe wake.
Kauli zimetoka kwenye kinywa cha Gwajima! Zipo mitandaoni zinasomeka, ni chuki tu iliyothibitishwa na CCM

Kibaya zaidi CCM imefungua ''floodgate'' Utakmakamata vipi Sheikh Ponda kwa uchochezi halafu umzawadie Gwajima kwa Ubunge na jamii ikuelewe!!!

Kwa maneno mengine Sheikh Ponda amepata 'natural immunity'' Atasema chochote
Ukimkamata Sheikh Ponda utaulizwa, vipi Ponda enede Ukonga , Gwajima aende Dodoma?
Kuna tatizo kubwa sana sijui kwanini CCM hawalioni!

JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu unamaliza kila kitu.

Unaongea kiasi ya kwamba hakuna la kuongezea.

Kama wanataka na wasome, waelewe na wafanyie kazi uandikayo

Salute!
 
Mwana Sacco's yeyote Ni mzao wa Lucifer



MUNGU mbariki magufuli
Ccm saaizi ni mali ya mtu binafsi..... Kila kitu kinaratibiwa kutoka Jamhuri ya watu wa chato na watoto wa dada ndo wanaamua nani awe nani...... Unayoyaona ni maigizo tu...
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Tuliza mshono wewe bwege!
 
Back
Top Bottom