Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Ndio wajue Magu hafai kabisa!!

Wacha wavurugane, ila usishangae wakaja kuikana hii taarifa wakiona inawaletea hatari huko mbele ingawa utekelezwaji utafanywa kama ulivyopangwa hata wakilalamika.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] akina bia yangu na mgonjwa mtambuka huwez kuwaona humu maana hii kwao ni maumivu mnoo
 
Binafsi sioni kosa as far as na wao ni watanzania. Kuwepo vyama vya upinzani haukuwafanyi wao kutopewa kipaumbele pindi wanaporudi CCM.
 
Ccm ni saccos binafsi na mmiliki wa chama ndie mwenye maamuzi, wasugua bench asilia wakafie mbele,teuzi zote ni za waunga juhudi,watakaokosa ubunge watateuliwa,ni mwendo wa ccm ya ndio ukiwa mtu wa ndio utazikimbia pesa zitakufata Hadi uvunguni, mwafrika ni dhaifu Sana mbele ya pesa maadamu anashibishwa huwa hajali kuhusu utaifa kwake tumbo kwanza.Hawa ma ndio,ndio wanaokwenda kubadili katiba ili washibishwe milele huku Jamii nzima ya wengi wakiteseka.
 
Rais Magufuli akijibu swali la Sojo, MNEC kutoka Songwe aliyesema kwamba ametumwa na wanasongwe kuwasemea kuwa wanasononeka pale ambapo wapinzani wanapohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kuwaacha wanachama ambao walikipigania chama kufa na kupona 2010-2015, wanavunjika moyo wanapoona wageni wanapita bila mbadala.

Pia soma > Rais Magufuli: Cecil Mwambe moyo wake uko CCM, Chama kilifanya makosa makubwa kumfanyia figisu 2015


Rais Magufuli amesema hilo lilipaswa kuzungumziwa kwenye kamati ya vikao vya CCM Wilaya au Mkoa kwamba wanaokuja kule huwahitaji. Lakini chama hiki ni cha watu, kina misingi yake, kinameza watu wote. Suala hilo lizungumziwe kwenye kamati za wilaya na mikoa na mlitafutie ufumbuzi.

Rais ameongeza kuwa CCM ina watu wengi ambao walikuwa vyama vingine kama Makongoro Nyerere na Mzee Wassira ambao walikuwa NCCR Mageuzi lakini sasa hivi ni CCM damu damu. Amewataka wanaccm kuwa na mioyo ya kuvumiliana ya kumtanguliza Mungu.

Amesema labda wana wasiwasi huyu aliyekuja huenda akawashinda na ndiyo maana amekuwa aliwashinda kila mara, otherwise mngekuwa mnamshinda, sasa kwa sababu anawatandika na mlikuwa mmejiandaa na akipigiwa kura za maoni atachaguliwa na wananchi.

Rais Magufuli ameendelea kusema kuwa Tatizo moja la siasa zetu tunajiwekea vizingiti kwamba akija huyu atashinda lakini mkiachiwa ninyi hamshindi. Nafikiri meseji umenipata.

Lakini Chama hiki kinapokea watu wote ilimradi wanazingatia masharti ya chama. Sasa mkiingia kwenye grupu zenu za kuanza kubishana mbona amerudishwa huyu! Amerudishwa kwa misingi kwamba mlimzuia njia akapitia dirishani, amerudi sasa apitie mlangoni mnataka tena mumzuie!! Muwe na uvumilivu. Ningependa huyo aliyeingia aendelee kushinda ili siku moja aingie kuwa mjumbe wa NEC.


Kwani mwanamke au mme wako akikosea, siku nyingine akaja kukuomba msamaha kwani utakataa? Siyo ajabu akaja na mapenzi mazuri mazuri kuliko ya zamani amejifunza huko mbinu nyingi na mbadala, Sasa unakataa uhondo huo? Rais amemaliza kwa kusema CCM oyeee
Hii ni fake kama
View attachment 1502731
Nashauri Pole Pole azungumze Ni kwa Sheria gani, vinginevyo awajibike
 
Wanachama wenyeji wa CCM mpoooooh? Sauti inatosha au? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwahiyo wakina Waitara,Mtolea,Mwembe,Lijuakali n.k wanaserereka kama mlima kitonga.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka hadi mbavu zinauma kwa kweli lol, wanamiminika kuelekea kolongoni khaaaaaah
 
Magufuli hajajibu swali. Amekwepa swali.

Kwa sababu, hakutakiwa kulisukuma hilo swali vikao vya chini wakati hata yeye kapokea wapinzani na kuwapa vyeo vikubwa vya ukatibu muu na unaibu waziri wizarani.

Hakujibu swali.

Kalikwepa tu.

Ww ndio umeona ukweli. Huu ni udhaifu wa wazi wa Magufuli pale anapopswa kujibu swali la uvunjwaji wa kanuni, sheria na katiba. Huwa anatoa majibu ya kebehi yasiyokidhi swali husika. Hii ndio sababu wanaccm wote na Magufuli mwenyewe hawako tayari kushiriki mdahalo wowote, na Magufuli binafsi kutokupenda kuhojiwa na waandishi wa habari.
 
Binafsi sioni kosa as far as na wao ni watanzania. Kuwepo vyama vya upinzani haukuwafanyi wao kutopewa kipaumbele pindi wanaporudi CCM.
Umeongea kama Mimi mkuu, sjiu kama upojirani na soft drinks, agizia soda na pepkon bili nitumie mkuu

Tanzania ni ya wote
 
Back
Top Bottom