Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

WENGI WANAJIANDIKIA TUU hawajui Tanzania ni kitu gani wapo wapo tuuu. Kushughulisha bongo hawataki wanabaki kuishi kwa matumaini.Wangejua Tanzania ni kitu gani wangeweza kujua nini tafasiri ya" mbele kwa mbele hakuna kurudi nyuma". Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Hatutaki Rais wa kujaribisha uongozi tunataka Rais asie wanyenyekea wakoloni
Sio tu tume huru, hata kama kwa kupanga mistari au kunyosha vidole Lisu hatoboi, agenda ya kukumbatia wazungu na kushtaki ulaya yeye na zito zimewatupa bora hata Mbowe
Akagombee udiwani tu Chato ndipo anaweza shinda kihalali Nani anahamu ya kuumizwa tena
 
Matendo ya uonevu ya ccm mpya kwa miaka 5 yamechangia Sana kuujenga upinzani nchini.
Kama wakiyatumia vizuri Makundi yote yaliyoumizwa ccm wakatafute kazi zingine.
 
Pesa zao ni za mkopo na zinalipwa kwa riba.Wanajua ukiathiri TZ basi utaathiri na nchi nyingi za maziwa makuu amabazo ni vibaraka wao.TZ ndo hurb ya nchi za maziwa makuu.
Si kweli,Hub ni Kenya.
 
Ushauri wa namna hii niliwahi kuusoma katika visa vya zamani sana kabla ya zama za Kristo (BC).
 
Asilimia 70 ya watanzania wapo brainwashed na utawala uliopo kuwa sio mafisadi anyway kwa vile ndiyo mnapopatia msosi ni sawa
 
Shida kubwa CCM haieleweki wanachama au washabiki wake ni wa mrengo upi. Wafanyakazi miaka mitano "no increment" pamoja na kukosa amani kazini (muda wowote unaweza tumbuliwa), wakulima tuna mfano wa wakulima wa korosho, wafanyabiashara zilizorasmi wamepigwa sana na "interest and penalty" zisizohalisia.

CCM wanachama na washabiki wetu ni kundi lipi miongoni mwa hayo matatu hapo juu? Ni makosa chama kutegemea watumishi wa serikali na taasisi za serikali kutetea uwepo wake madarakani badala ya umma wa wananchi ambao ndio huipa serikali madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…