Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

At least leo umefunguka wapi hasa unasimamia. Membe. Kelele zote kumbe ni kumpigania mgombea wako, kitu ambacho hakina ubaya wowote.
Nisichoelewa ni kwa utaratibu gani JPM atamuachia Membe. Unakumbuka juzi kwenye ufunguzi wa Ikulu mpya Mzee Mkapa alisema nini? "Mbele kwa mbele, wala hakuna kurudi nyuma"
Sio kwa bahati mbaya. Membe sijui kama atawahi kuja kuwa Rais. Sio kwa Tanzania hii, maana naona chances zinazidi kufifia siku hata siku
WENGI WANAJIANDIKIA TUU hawajui Tanzania ni kitu gani wapo wapo tuuu. Kushughulisha bongo hawataki wanabaki kuishi kwa matumaini.Wangejua Tanzania ni kitu gani wangeweza kujua nini tafasiri ya" mbele kwa mbele hakuna kurudi nyuma". Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Hatutaki Rais wa kujaribisha uongozi tunataka Rais asie wanyenyekea wakoloni
Sio tu tume huru, hata kama kwa kupanga mistari au kunyosha vidole Lisu hatoboi, agenda ya kukumbatia wazungu na kushtaki ulaya yeye na zito zimewatupa bora hata Mbowe
Akagombee udiwani tu Chato ndipo anaweza shinda kihalali Nani anahamu ya kuumizwa tena
 
WENGI WANAJIANDIKIA TUU hawajui Tanzania ni kitu gani wapo wapo tuuu. Kushughulisha bongo hawataki wanabaki kuishi kwa matumaini.Wangejua Tanzania ni kitu gani wangeweza kujua nini tafasiri ya" mbele kwa mbele hakuna kurudi nyuma". Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
Matendo ya uonevu ya ccm mpya kwa miaka 5 yamechangia Sana kuujenga upinzani nchini.
Kama wakiyatumia vizuri Makundi yote yaliyoumizwa ccm wakatafute kazi zingine.
 
Pesa zao ni za mkopo na zinalipwa kwa riba.Wanajua ukiathiri TZ basi utaathiri na nchi nyingi za maziwa makuu amabazo ni vibaraka wao.TZ ndo hurb ya nchi za maziwa makuu.
Si kweli,Hub ni Kenya.
 
Ukweli mchungua Lissu ni maaarufu sana kuliko Magufuli, Lissu amesoma na kuelimika kuliko Magufuli, Lissu anaijua Tanzania na tatizo la nchi hii kuliko Magufuli, Lissu anaijuwa siasa ya ndani ya Tanzania na nje kuliko Magufuli, Lissu hana hata tuhuma moja ya ufisadi kama Magufuli.

Lissu anaelewa mizizi ya ufisadi wa taifa ili kuliko Magufuli, Lissu amekuwa akiwatetea watanzania hata kabla ya Magufuli kuanzia miaka ya 2000 uko.

Muda bado upo angalau ungemuachia Membe au Makamba angalau wangejenga hoja, Ila ukiendelea kutumia nguvu kupambana na Lissu utaenda Chato na mwenzio ataenda Ikulu.

Ukitaka kushinda jenga hoja ila kwa kutumia nguvu utaanguka na wapambe watakukimbia hakuna watu wanafiki kama watanzania hasa wapambe wa rais.
Ushauri wa namna hii niliwahi kuusoma katika visa vya zamani sana kabla ya zama za Kristo (BC).
 
Upuuzi huu usipojibiwa mapema aliyeutoa anaweza asielewe kuwa kamwaga pumba!
Lisu alikuwa anaheshimika sana ila kwa sasa ameshajipambanua kuwa anatumikia mabeberu! Hana ubavu wa kupambama na jembe la afrika Dr. Magufuli. M*mbe ni fisadi MASKINI, akipata nafasi twafa!!! Hatafanya "makosa"!! Atahakikisha anakomba vyote vinavyokombeka, atabeba vyote vinavyobebeka na atafisadi vyote vinavyofisadika!! Ana njaa ya ufisadi kupita mfalme Jeta!!!
Asilimia 70 ya watanzania wapo brainwashed na utawala uliopo kuwa sio mafisadi anyway kwa vile ndiyo mnapopatia msosi ni sawa
 
Ukweli ni makosa tumefanya wenyewe CCM kuacha kufanya kazi tumekaa kupammbana na maneno na wapinzani kwa gharama kubwa. Tumeacha kuwafanyia watu kazi tumeruhusu vikundi ndani ya Chama na kutengeneza wezi wapya wanaolindwa. Safarii hii wapinzani wana hoja kuliko zilizopita. Sisi CCM asili tunasema ili tushinde tena lazima TUTUMIE DOLA na ndivyo itavyokuwa.
Shida kubwa CCM haieleweki wanachama au washabiki wake ni wa mrengo upi. Wafanyakazi miaka mitano "no increment" pamoja na kukosa amani kazini (muda wowote unaweza tumbuliwa), wakulima tuna mfano wa wakulima wa korosho, wafanyabiashara zilizorasmi wamepigwa sana na "interest and penalty" zisizohalisia.

CCM wanachama na washabiki wetu ni kundi lipi miongoni mwa hayo matatu hapo juu? Ni makosa chama kutegemea watumishi wa serikali na taasisi za serikali kutetea uwepo wake madarakani badala ya umma wa wananchi ambao ndio huipa serikali madaraka
 
Back
Top Bottom