Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Nikiri kwamba mimi ni muislamu kwa kuzaliwa.

Ukiwa mpenda haki lazima uwe na uwezo wa kusimama katikati na kusema kweli.
Iliripotiwa kwamba kuna mtumishi mmoja kachana MASAHAF Huko Morogoro.

Hatua zilizochukuliwa dhidi yake ni kama ameua yaani mwamposa aliyekusanya watu na kusababisha wakanyagane akaonekana katenda jambo dogo kweli kuliko la kuchana MASAHAF.

Kama tunakumbuka vizuri hapa jukwaani kuna mtu aliitwa DIBAGULA. Huyu bwana alitokea huko huko Morogoro. yeye alisema YESU SIO MUNGU. Hukumu ya case yake inajulikana ukweli ni kwamba alishinda?

Leo kuna mzalendo mmoja huko Kigamboni amemfukuza huyu bwana kazi. Ni amma hajui sheria, kanuni na taratibu za utumishi au ni mihemko tu ya kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Nitaeleza:

1) Kwanza jamaa hajapewa nafasi ya kusikilizwa. Hapo anashinda mchana kweupe, hakuna mashtaka yoyote ya kiutumishi yaliyofunguliwa dhidi yake. Mkuu wa nchi kaingia chaka.

2) Imani yake haiamini kwenye utukufu wa qurani, yeye mkristo, unaposema kitabu kitakatifu sio kwake

3) Kosa alilofanya halimuathiri mwajiri wake kwa namna yeyote ile, amelifanya nje ya kazi zake.

Tujifunze kuheshimu Sheria
 
Rais hajakosea lolote tena ameacha nafasi ya mahakama kutoa hukumu. Shida ya wapenda siasa wengi wakimchukia mtu wanaamini kila atakalofanya ni kosa.
 
Ndugu yangu kweli hata huzitambuwi alama za nyakati? Tangulini mahakama ikaingiliana na serikali kuu?
Amesema amemfukuza kazi ya serikal kuu hana kazi huko mahakaman ashinde au asishinde ila hana kazi.
Alie muajiri hamtaki sasa amevunja sheria wapi?
Tumekuwa hater wa serikal kiasi hakuna jema tunaliona.
Ulitaka amwache mtu anaye taka kulipuwa taifa letu kwa mambo kidini?
Huyu nimtu hatari sana
 
Mbona haja mzungumzia na yule alie chana Biblia? Ambayo yeye ana iamni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe Magufili kuimeza mihimili mingine...ila hilo la Eti taifa lilipuke maxhafuko kisa kuchanwa hicho kįtabu....ni upumbavu kufikiri hivyo.
 
Soma hii kitu
Administrative law is the body of law that governs the activities of administrative agencies of government. Government agency action can include rule making, adjudication, or the enforcement of a specific regulatory agenda.
Judicial review of administrative actions
Zaidi ya hapo, soma hii... c&p

 
Kinoamiguu,
1:Cha kwanza acha unafiki wa kijinga ww siyo muislam,muislamu hawezi kumtetea mtu aliye kidharirisha kitabu ambacho anaamimi ni kitukufu.
2:Kwa hiyo kumbe siku hizi ukiua au ukiiba nje ya kituo chako cha kazi ni halali?unapo onesha kitendo chochote kisicho faa ndani ya jamii haufai kuwa kiongozi au mtumishi.
3:Kitendo alicho fanya huyu jamaa ni inshara tosha ya chuki yake dhidi ya uislam na waislam, kwa mujibu wa sheria ni kosa kuonesha chuki hadharani dhidi ya jamii yeyote haijalishi unakubaliana na maono yake au la.
4: huyo aliye sema yesu sio mungu hana kosa kwa sababu yeye alitoa maoni yake jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, ya kwamba unaruhusiwa kuamini chochote kwa imani yako Lakini usingilie au kukiharibu anacho amini mwenzio eti kwa sababu hukubaliani nacho,na ndio maana serikali imeruhusu midaharo mbali mbali kati ya dini tofauti hata hapa jf kuna jukwaa la dini.
5:kingine muajili wako ndio mwenye uwezo wa kukwambia sikuhitaji kwa sababu ndio kakuajili.
 
mahakamani ana kesi nyingine sio ya kiutumishi.....
mwajiri mkuu ameamua kwa nafasi yake.

Ukimpiga mkeo na kuna ushahidi wa video mahakamani utakuwa na kesi ya kumsababishia mkeo maumivu etc.. na mwajiri anakuona pimbi anakutimua kazi hata kabla ya hukumu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesha fukuzwa kazi kabla ya sheria kuchukua mkondo wake, sheria ingeanza kisha kufukuzwa kazi. Turejee pongezi kwa Rais alizotoa Mufti Mkuu akiwa Tanga ndizo zilizotoa muelekeo wa adhabu naye alikuwepo Kigamboni.
 
acting stupid ni kosa tayari... kuna kifungu cha sheria kinaingilia maisha na muonekano wa mtumishi ndani na nje ya mazingira ya kazi.

Mfano...Ukimrekodi mtumishi wa serikali kalewa na anakojoa kwenye kundi la watu inatosha kufukuzwa kazi

Huyu video ya kuchana kitabu kitakatifu kinamfutia sifa ya kuwa mtumishi wa serikali
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani sheria na maadili vinapingana??

Sheria inasimamia maadili wewe

Unafikiri kulewa sio kosa kisheria kwa mtumishi? Wacha uongo.

Rais amekosea ndio maana kasema ashinde sheria asishinde mi namfukuza.

Anaweza shinda kesi ila wa kumrudisha kazini ndio kizungumkuti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbagala na Kagera makanisa yalichomwa moto lakini taifa halikulipuka.
 
Naungana na rais Kama mpenda amani wa nchi hii. The executive order inamlinda magufuli katika baadhi ya maamuzi anayochukua.wafanyakazi wapumbavu Kama hawa hakuna hajaya kusubiri maamuzi ya mahakama wakati video recorder imeonesha ushenzi wote alokuwa anaufanya. To hell
 
Nampongeza rais kwa uamuzi huo,huyo jamaa alichotaka kufanya ni kuivuruga amani yetu,niseme amepata alichokitaka.

Na amani ikiharibika zigo lote lingemwangukia Magufuli,
Na hii iwe lesson kwa wengine
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari ameishawishi mahakama itoe adhabu anayoitaka yeye.
 
Raisi amejiridhishaje kama iliyochanwa ni Quran?. Kwamba karidhika tu kwa kuona clip ya video na maneno ya Watu mitandaoni? vipi kama hiyo ni clip iliyohaririwa?

Kama tunaziheshimu Mahakama basi ndio chombo sahihi cha kutuambia huyo Bwana kweli alichana Qurani au la.

Alitakiwa kuchukua hatua baada ya hukumu ya muhimili husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…