Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Sio kwer Kama ndio hivyo bac sheria hiyo ilisha expaya maana watumish wanafumaniana kila siku na hazchukuliwi hatua Kama hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo jambo la kufumaniana utalilinganishaje na hili? Suala lakufumania halimuhusu mtu mwingine zaidi ya aliye fumania na aliye fumaniwa kwa sababu kama ni mke ni wako tu na sio mke wa jamii fulani.
Lakini kitabu cha dini kinagusa mamilioni ya watu na haitakiwi kukidhihaki ni kosa.
 
Pole sana . Mm ni mwislamu ila siyo DOGMA.
Ungesema kosa alofanya pale kisheria ni lipi.katiba kusema tu kwamba kufanya jambo lisilofaa hufai kuwa Mtumishi ni kuonesha kwahyo MTUMISHI AKIFUMANIWA ANAFUKUZWA KAZI?
1:Cha kwanza acha unafiki wa kijinga ww siyo muislam,muislamu hawezi kumtetea mtu aliye kidharirisha kitabu ambacho anaamimi ni kitukufu.
2:Kwa hiyo kumbe siku hizi ukiua au ukiiba nje ya kituo chako cha kazi ni halali?unapo onesha kitendo chochote kisicho faa ndani ya jamii haufai kuwa kiongozi au mtumishi.
3:Kitendo alicho fanya huyu jamaa ni inshara tosha ya chuki yake dhidi ya uislam na waislam, kwa mujibu wa sheria ni kosa kuonesha chuki hadharani dhidi ya jamii yeyote haijalishi unakubaliana na maono yake au la.
4: huyo aliye sema yesu sio mungu hana kosa kwa sababu yeye alitoa maoni yake jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, ya kwamba unaruhusiwa kuamini chochote kwa imani yako Lakini usingilie au kukiharibu anacho amini mwenzio eti kwa sababu hukubaliani nacho,na ndio maana serikali imeruhusu midaharo mbali mbali kati ya dini tofauti hata hapa jf kuna jukwaa la dini.
5:kingine muajili wako ndio mwenye uwezo wa kukwambia sikuhitaji kwa sababu ndio kakuajili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiri kwamba mimi ni muislamu kwa kuzaliwa.

Ukiwa mpenda haki lazima uwe na uwezo wa kusimama katikati na kusema kweli.
Iliripotiwa kwamba kuna mtumishi mmoja kachana MASAHAF Huko Morogoro.

Hatua zilizochukuliwa dhidi yake ni kama ameua yaani mwamposa aliyekusanya watu na kusababisha wakanyagane akaonekana katenda jambo dogo kweli kuliko la kuchana MASAHAF.

Kama tunakumbuka vizuri hapa jukwaani kuna mtu aliitwa DIBAGULA. Huyu bwana alitokea huko huko Morogoro. yeye alisema YESU SIO MUNGU. Hukumu ya case yake inajulikana ukweli ni kwamba alishinda?

Leo kuna mzalendo mmoja huko Kigamboni amemfukuza huyu bwana kazi. Ni amma hajui sheria, kanuni na taratibu za utumishi au ni mihemko tu ya kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Nitaeleza:

1) Kwanza jamaa hajapewa nafasi ya kusikilizwa. Hapo anashinda mchana kweupe, hakuna mashtaka yoyote ya kiutumishi yaliyofunguliwa dhidi yake. Mkuu wa nchi kaingia chaka.

2) Imani yake haiamini kwenye utukufu wa qurani, yeye mkristo, unaposema kitabu kitakatifu sio kwake

3) Kosa alilofanya halimuathiri mwajiri wake kwa namna yeyote ile, amelifanya nje ya kazi zake.

Tujifunze kuheshimu Sheria
Point ni mtumishi wa umma alafu matendo ya kijinga hayo mengineyo hayana umaana.
 
Rais kama muajiri mkuu wa Serikali na aliyechana Quran ni muajiriwa wa Serikali na serikali imeweka viwango vya nidhamu na maadili ambavyo vingine vipo nje ya sheria ila ndani ya mamlaka ya ajira, kumfukuza mtu aliyefanya hivi si kosa.

Mahakàmà itaangalia kosa kwa upànde wa kisheria na serikali imeangalia kosa kwa upànde wa maadili na si makosa yote ya kimaadili yanavunja sheria, mengine yanavunja taratibu za kazi na za kiutumishi.

Mfano mtu kaenda kazini kalewa, hilo ni kosa la kimaadili ambalo sheria haiwezi kumkuta na kosa.

Rais hajavunja sheria yeyote ila katekeleza wajibu kama muajiri mkuu na msimamzi wa maadili wa watumishi wote wa umma

Shida ya kiongozi wetu ni kuongea sana kwa freestyle. Anasahau maneno ya kiongozi yana uzito sana, na hii ya kumchukulia Rais kama mfalme ndio tatizo letu kubwa. Ajira ni mkataba, una masharti yake ya kuvunja. Huyu jamaa anaweza kwenda mahakamani na kushinda kesi na unlawful dismissal. What will happen then?
 
Hiyo ni mifano ya nchi ambayo ni predominantly Christians, kwenye taasisi nyingi za serikari na private zinazotoa huduma kwa jamii mchanganyiko utakuta kuonyesha msalaba kwa mfanyakazi mkirsto airuhusiwi kwa sababu awaamini kwenye ku-promote dini kazini.

Whereas taasisi hizo hizo utakuta kalasinga anaruhusiwa kuvaa turban na wanawake wa kiislamu ushungi; why so? Kwa sababu wanaona ni sehemu muhimu ya dini zao, wakati kuvaa mslaba kwa wakristo inaonekana sio takwa la lazima.

Ndio kama hii kesi ya huyu jamaa kwa wale wanaoona anaonewa ni kwa sababu awali tazami hilo kosa kwa jicho la waislamu bali kwa imani zao wao; hila kwa waislamu hiyo ni adhabu stahiki kwa nchi yetu.

Ingelikuwa nchi ambazo uislamu unetawala na zenye sheria za blasphemy hilo kosa adhabu yake ni death by stoning. Hatua za serikari ni sahihi kabisa Katika kuhakikisha watu wana heshimu dini za wengine.
 
Sijui hata kama watawala wetu wanatambua kuwa nchi yetu kuwa "secural state" inamaanisha nini? Licha ya muhusika kufanya kitendo chenye maudhi kwa watu wenye imani iliyokuwa tofauti na ya kwake, lakini ingetosha muhimili wa mahakama ufanyie kazi suala hilo ambalo kwa mazingira ya wazi yalionyesha kuwa ni la kichochezi.

Ndiyo! Tendo hilo la kuchana juzuu tena mbele ya Waislamu, ni kutaka kuwachochea kwa makusudi ili wapate mihemuko isiyokuwa na ulazima wowote na hatimaye wakose uvumilivu, na pengine ktk kuitetea imani yao wapate sababu ya kulipiza kisasi, jambo ambalo linaweza kuwaingiza ktk kutenda jinai ama uvunjifu wa amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wengi hawajui kuna tofauti kati ya immorality and illegality. Sio kila kitu ambacho ni immoral ni illegal.
 
1:Cha kwanza acha unafiki wa kijinga ww siyo muislam,muislamu hawezi kumtetea mtu aliye kidharirisha kitabu ambacho anaamimi ni kitukufu.
2:Kwa hiyo kumbe siku hizi ukiua au ukiiba nje ya kituo chako cha kazi ni halali?unapo onesha kitendo chochote kisicho faa ndani ya jamii haufai kuwa kiongozi au mtumishi.
3:Kitendo alicho fanya huyu jamaa ni inshara tosha ya chuki yake dhidi ya uislam na waislam, kwa mujibu wa sheria ni kosa kuonesha chuki hadharani dhidi ya jamii yeyote haijalishi unakubaliana na maono yake au la.
4: huyo aliye sema yesu sio mungu hana kosa kwa sababu yeye alitoa maoni yake jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, ya kwamba unaruhusiwa kuamini chochote kwa imani yako Lakini usingilie au kukiharibu anacho amini mwenzio eti kwa sababu hukubaliani nacho,na ndio maana serikali imeruhusu midaharo mbali mbali kati ya dini tofauti hata hapa jf kuna jukwaa la dini.
5:kingine muajili wako ndio mwenye uwezo wa kukwambia sikuhitaji kwa sababu ndio kakuajili.
Kiongozi namba 4 na namba 5 unajikontradikti... umeonyesha uislamu wako na si uhalisia... Yaani huyu kusema Yesu si Mungu umeona ni sawa..!!! Hapo hapo kwa dhana hiyo hiyo usisahau kuwa kwa aliyechama hicho kitabu, kwa imani yake halina tofauti na kile cha historia, kama ambavyo huyo aliyesema Yesu si Mungu anaovyoamini juu ya hilo... HALAFU USISAHAU KUWA KATIBA INATOA UHURU WA KUTOA MAONI, LAKINI INATEGEMEA NA MAONI UNAYOTOA... Hivi ukiona useme utauwa watanzania wote uachwe kwa vile una uhuru wa kutoa maoni.???
 
Bosi wako anaweza kukufukuza hata kama hapendi harufu ya manukato yako ... kisheria anaweza akawa sahihi mahakama ndiyo itakayo amua ila mwajiri wake kasema hamtaki ... imekuuma sana akitoka mwajiri wewe
 
Haijalishi unaamini nini ila kuchukua kitabu cha wenzako ukakichana na maneno kibao ya dhihaka sio sahihi. Same people mnaomtetea huyu jamaa sidhani mngefurahi ingekuwa kinyume chake. Watanzania tuacheni unafiki. Hivi mfano utajisikiaje wewe kama mkiristo umshuhudie ustadh na kibandiko chake achukue biblia hadharani afungue zipu aikojolee huku akiwadhihaki wakristo kama jamaa wa morogoro alivokua anaongea wakati anachana mas'haf
 
Hakuna mwajiri mpumbavu ambaye anaweza amuajiri yule kichaa ... Mtumishi wa umma mpumbavu ... siujui uislam ila siwezi nikaamka asubuhi nianze kuchana makaratasi yao infront of camera eti kisa siutaki uislam ...
 
Dibagula alichana na kuikanyaga Biblia?

Kusema Yesu siyo Mungu siyo ishu maana imeandikwa hivyo kwenye Quran kuwa Yesu siyo Mungu.

hata Mashahidi wa Yehova wanasema Yesu siyo Mungu.
Huu ndo ujinga ulikithiri... yaani asiye RC aseme Yesu si Mungu halafu mimi nmlazimoshe kusema YESU ni Mungu huku nikijua yeye si wa RC..!!! ASEM WA RC NDO NITASHITUKA.... The fact kwamba hayuko kwenye u RC basi Indirectly anasema Yesu si Mungu... sihangaiki na huyo....
 
Serikali iliyopo madarakani inafanya kazi kwa niaba ya wananchi usiwe mpumbavu.
sasa kama serikali iliyoko madarakani inafanya kazi kwa niaba yako , mbona huwa unashupaza shingo kumpondea magufuli humu jukwaani?
 
Haya yalianza toka ishu ya Nabii Tito,alikamatwa na kudharirishwa pasina sababu ya msingi.
 
Retire wewe ni mnafiki sana. Kama amekuuma nenda kamtolee dhamana ikotokea akishinda kesi muajiri wewe...
 
Haijalishi unaamini nini ila kuchukua kitabu cha wenzako ukakichana na maneno kibao ya dhihaka sio sahihi. Same people mnaomtetea huyu jamaa sidhani mngefurahi ingekuwa kinyume chake. Watanzania tuacheni unafiki. Hivi mfano utajisikiaje wewe kama mkiristo umshuhudie ustadh na kibandiko chake achukue biblia hadharani afungue zipu aikojolee huku akiwadhihaki wakristo kama jamaa wa morogoro alivokua anaongea wakati anachana mas'haf
Wanafanya hayo au yanayofanana na hayo mara kadhaa... na wakristu tunawapotezeaga tu.. umewahi fika kwenye mihadhara yao..?? Yaani hawa watu hata misiba ya kiislamu huwa waziba barabara... hata wakiwa na sherehe huwa wanaweka maturubai kuziba barabara..!! Tunavumiliaga sana...
 
Back
Top Bottom