Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Tukisema Magufuli hafai kuongoza hata kijiji mafisi wa Lumumba wanabisha!
Hivi huyu Magufuli anaposema NCHI NI TAJIRI SANA huwa anamdanganya nani?FEDHA ZIKO WAPI? Maana kama nchi ina fedha ni Tajiri sana inakuweje Rais anahamisha Fedha iliyopangwa kwa kazi maalumu na kuipeleka kwengine. What is Budget???
Nini maana ya BAJETI KUU YA SERIKALI inayopangwa na Serikali kupitia Bunge lake??
Huu utawala ni wa hovyo sana kuwai kutokea Tanzania......!!!!!!
 
Intuition sharti itumike wapi na wapi? Dodoma tayari mpango wa serikali ulikuwa kwenye hospitali ya BWM. Yeye rais kaona iongezwe nyingine tena kwa pesa ambayo ingetumika siku mbili au tatu tu! Sasa hapo aliyepotea nani kati yetu.
Hilo ndio tatizo. Unaamua mambo kwa hisia. Hospitali ya Dodoma sio emergency, kwamba ghafla tumekumbwa na tatzizo lazima tupate fedha haraka kwa kuwa hatukuwa tumetenga fedha za kuijenga na tunakabiliwa na ugonjwa hatari ambao utatibiwa katika hii hospitali. Kuongeza hospitali nyingine Dodoma ni jambo sahihi sana tu, lakini kuna emegency gani huko kiasi lazima iongezwe sasa? Kwa wazo hil lisipelekwe Wizara ya Afya ili katika mipango ya budget ijayo ijumuishwe?

Intuition ni jambo zuri, lakini intuition kwenye kitu kama kujenga hospitali ambayo wala sio emergency ni kukosa tu akili ya kupanga. Intuition katika kipindi cha Magufuli imefanya ytuanze miradi mikubwa bila kuangalia tutaimaliziaje, kisha tunaanza kuhangaika kutafuta fedha. SGR, tunajadli mkopo na Standard Chartered Bank BAADA ya kuanza kujenga. Then tunakuwa desparate. Unaamua kushona koti bila kujua ukubwa wa kitambaa ulicho nacho. Akili hiyo? NI udhaifu. Kutafuta kiki za siasa.
 
Umenena vyema sana
Pata soda bariiidi kwanza upoze koo
 
Sawa kwa watu kama wewe, mnataka Serikali ieleze "mipango" yake labda miezi sita au saba kabla ya kuutangazia umma mpango au uamuzi huo? Hivi unadhani Serikali au Rais hakuwa na mpango wa hiyo hospitali? Unadhani kafanya uamuzi tarehe 02/12/2020 na kisha kumueleza Waziri Mkuu akatangaze, kweli!? Mipango ipo na ni suala ya kuujulisha umma tu utekelezaji wake. Hizo Bilioni 2.3/= za ujenzi wa hiyo hospitali baada ya kutoa zile Milioni 900/=+ za walai za sherehe zile za kwanza zilitoka wapi, kama siyo kwenye bajeti ya Serikali na vyanzo vingine kama alivyo elezea PM!? Mbona wapinzani mnakuwa wagumu na wazito kuelewa vitu rahisi rahisi kama hivi!?
 
... nje ya mada; ina maana 09-12-2020 haitakuwa siku ya mapumziko ama?
 
Sawa kwa watu kama wewe, mnataka Serikali ieleze "mipango" yake labda miezi sita au saba kabla ya kuutangazia umma mpango au uamuzi huo? Hivi unadhani Serikali au Rais hakuwa na mpango wa hiyo hospitali?
Kama alikuwa na huo mpango na katika kupanga akaamua ataokoteza fedha mahali, basi ni kweli hafai kuwa raisi.

Angekuwa anajua uongozi huo mpango anagemwagiza Waziri wa afaya aujumuishe katika bajeti ya Wizara

By the way, hii pia ni dalili kwa nini Magufuli hataki mawaziri. Anataka kila kitu afanye yeye. Sasa ni mtu wa aina gani huyo?
 
Tofauti kubwa kati ya Tanzania na North Korea ni kuwa North Korea hakuna nyumba za matope na nyasi, serikali imejenga nyumba (flats) kwa mahitaji ya raia wote wasio na uwezo wa kujenga au kununua. Huduma zao za kijamii ni bora zaidi.
Hujazungumzia suala la uchumi.
 
dudus,
Well said. Hii nji kwa sasa inaongozwa na mtu asiye na maadili ya Uongozi
Bunge huwa linakaa kila mwaka na kupanga Bajeti ya Serikali kwa kila Wizara,Idara na Taasisi zake.
Inashangaza sana kusikia Rais anahamisha Fedha iliyotengwa kulingana na Bajeti na kuipeleka kule akili yake inamtuma. JE, WIZARA YA AFYA HAIKUTENGEWA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITAL HIYO???Hapa ndipo Maneno ya baba wa Taifa Mwl. Nyerere yanapo jidhihirisha wazi kuwa Rais analala na kupewa ushauri na mkewe halafu anatumia ushauri huo kutawala nji!Hatujui kesho atasema nini!!
 
Napita tu
 
MKuu sasa unaelewa kwa nini hataki mawaziri. Kuna siku atasema BUnge lisifanye mikutano ili tuokoe fedha za kumalizia Stiegler Gorge!
 
Ndio ishakua.
 
Mleta mada uelewa wako wa mambo uko chini sana. Nenda kasome kuna kitu kinaitwa “Mid Year Review” au “Budget Reallocation” vitakusaidia kuelewa. Hivyo vitu unaweza kujisomea kwenye internet au tafuta Sheria ya Bajeti. Hayo mambo Serikali inafanya kila mwaka kama kuna uhitaji wa kuhamisha Bajeti kutoka Activity A kwenda Activity B.
 
Wewe ni Punguani kabisa, hivi hawa watoto wanaokua sasahivi wajifunze nini juu ya Sherehe za Uhuru?

Ikiwa Uhuru hawakuuona na Sherehe zake wasizione?

Inchi inayoghairi Sherehe za kitaifa kwa Mujibu wa Katiba ni Nchi mfu.
Uko sahihi kabisa. Jamani sherehe za UHURU sio japo la kisiasa ni jambo la kihistoria. Nyerere na wenziwe walipoteza nguvu nyingi kuutafuta uhuru wa nchi. Duniani sis ndo wa kwanza kubeza tukio hilo. Watawala eti wata save mil 834. Hizo ni sawa na gharama ya V8 3. Watoto wananyimwa haki yao ya kushuhudia wanachokisoma kwenye vitabu kwa vitendo. Wanaharisha kutafuta political mileage au umaarufu wa kisiasa sio kusave gharama. Tunaua historia ya nchi hii. Nyerere uko alipo anasikitishwa na uimla wa namna hii.
 
MKuu sasa unaelewa kwa nini hataki mawaziri. Kuna siku atasema BUnge lisifanye mikutano ili tuokoe fedha za kumalizia Stiegler Gorge!
Uko sahihi mkuu.
Hapo alipo anaona ataokoa mishahara kwa miezi 2-4 kwa kutoteua Mawaziri halafu mwisho wa siku atajisifu! Akili ya ajabu kabisa!
Huyu Rais ni wa ajabu sana. Huwa ana tamani ASHIKE KILA WIZARA hasa Wizara ya Fedha alikomweka mtoto wa dadake a.k.a mjomba!!!
Miaka 5 mingine tutashuhudia mahoka na vihoja lukuki!
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabu ajabu.
Na wewe uache kufanya sherehe za birth days zako. Unamaliza hela bure! Uwe mfano pia.
 

Kinachoonekana au kujificha kwa huyu jamaa ni Roho mbaya na Uchoyo.
Anajua sherehe za Uhuru zikifanyika watu watalipwa hela za posho kujikimu na yeye hataki!!!
Kama Rais anaweza toa kauli tata kama "....WALE WALIOKUWA WANAPATA MISHAHARA MIKUBWA NITAWASHUSHA WAISHI KAMA MWASHETWANI..." mwisho wa kunukuu.
 
Nchi inaendeshwa kama gari mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…