Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Mbona siku hizi hapigi simu CLOUDS tena ?
Apige ili iweje??
FB_IMG_15239867002388431.jpg
 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.

Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii

==========
Kutoka Gazeti la Mwananchi:
Salary slip iko wapi?
 
Sasa huu mshahara analipwa wa nini wakati kila kitu kuanzia mavazi, chakula, ulinzi, malazi, afya, usafiri nk yeye na familia yake wanapata bure?
 
Ni kwanini apunguze mshahara wake tofauti na waliomtangulia kutawala nchi?
Rais ni lazima alipwe mshahara wa daraja lake analostahili kulingana na cheo chake cha ukuu wa nchi.
Kisheria Raisi haruhusiwi kujiongezea au kujipunguzia mshahala tofauti na kanuni zilizowekwa.
Namshauri mlipaji mkuu, amrudishie mshahala wake wa awali anaostahili kwa madaraka yake aliyopewa na wananchi tuliomchagua kwani ni haki yake kikatiba.

Haiwezekani wenzake walipwe vizuri na yeye alipwe chini ya daraja lake.
Hata kama atakataa, awekewe kwenye akaunti yake ya malipo kama anataka kuigawa mahali basi hilo ni jukumu lake na hakatazwi. Mlipaji Mkuu, hebu timiza wajibu wako kwa Mheshimiwa Rais mara moja.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Likizo haijaisha tu mpaka leo tuone hiyo salary sleep ndio sleep
 
Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.

Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12.

Leo kwenye hafla ya kumwapisha Naibu waziri wa Madini, Mheshimiwa Rais alijikuta akitaja kiasi anacholipwa wakati akiongelea suala la mishahara ya watumishi waliokuwa TMA baadae kubadilishiwa sekta, watumishi hao ambao Rais alidai waliboronga huko TMA wanapaswa wasilipwe mil 10 tena mishahara yao ipunguzwe na kuongeza kuwa asiyetaka aache kazi. Maana kuna wengine wanalipwa mishahara ya ajabu sana.

Kwa mshahara huo wa Magu watumishi wengi mno wenye mshahara kumzidi, nashawishika kusema kuwa Rais Magufuli ana mabaya yake lakini ni Rais bora sana kwenye mambo mengi.
 
Back
Top Bottom