Uchaguzi 2020 Rais Magufuli muombe Rais Mstaafu Kikwete akusaidie kupiga kampeni

Subiri mwaka huu uone unafikiri mbinu ya CCM kujitangaza washindi hata Kama wameshindwa kwenye sanduku la kura kupitia nec watu hawaijui wameandaa dawa yenu mwaka huu .
Mbona wale wabunge 20 hiyo dawa haijafanya kazi?
 
CCM ni chama cha mikakati. Hawa wastaafu inajua itawatumia wapi na wakati gani? Subiri kampeni bado hazijaisha ndo kwanza kumekucha asubuhi. Wapinzani wao haijulikani kama hata kampeni zao watazimaliza kabla pumzi haijakata.
Wapinzani wa Burundi???
 
Huyu bwana Petro unabii wake bado kidogo (5%) kutumia kwa asilimia zote. Yaani Lisu kuingia ikulu tu.

Hawa Mataga walisema akirudi tu tutamtia ndani [ IGP SIRRO} ; wap, huyo anayoyoma huku JIWE pressure ikimpanda anapoona nyomi inamsikiliza Lissu nchi nzima! Hawataamini watakapoambiwa ameshindaaaa!!
 
Nkifikiri unamshauri Lisu aombe msaada kwa Slaa kumbe unamshauri Magufuli?
 
Mzee Warioba aljyepigwa ngwara(aliyechotwa mtama)?
 
Kinana, Kikwete na makamba utawaona jukwaani soon...

Wanaingia dakika za mwisho kusafisha uchafu.....

Hata asaidiwe na nani, sisi wananchi ndio tushaamua. Nchi si mali ya Kinana, Kikwete wala Makamba. Wenye nchi (sisi Watanzania), tunamuweka Lissu madarakani. Msiwape watu fulani fulani umiliki wa nchi yetu. Wao ndio watapiga kura?

Kwa taarifa yako hao wazee hakuna rangi nao wameacha kuona kwa huyu bwana. Hata wakijitokeza itakuwa ni unafki tu. Lissu hazuiliki aisee, imekula kwenu Mataga na Jiwe wenu.
 
Magufuri hata asipopiga kampeni atashinda tu... Hamna mtu anayeweza kuwapa chadema nchi. Mbona haitaji hata elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo. Watu wengine vichwa vyenu vina nini? Mbona hamuelewi?
Wananchi ambao ndo wapiga kura hawawezi?
 
Magufuli kila akisimama kwenye majukwaa ya kisiasa alikuwa lazima aukandie utawala wa baba yetu mtukufu Daktari Jakaya Mrisho Kikwete utafikiri hakuwahi kwenye cabinet ya Jk, zee ni linafki la kutupwa.

Jiwe ni mbinafsi sana na anajikuta ndio mwenye akili na uwezo kuliko Watanzania wote. Kwa kweli Watanzania sasa wanamfunza ya dunia, haamini kuona kwenye picha kuwa kuna watu wanakanyagana na kukimbiza misafara ya watu wengine ukitoa yeye. Anapenda iwe yeye tu kila kitu.
 
Magufuli na ujuaji ni chanda na pete
 
Karata ya mwisho hiyo mkuu,vitani unaanza na migambo kwanza na magobore.........
 
Wakati huu ni vizuri na ingependeza awasaidie Mama Salma na Mh Riziwani kampeni za ubunge. 'Charity begins at home.'
 



Kuliko JK akamsaidie Jiwe, bora tu hata akawe campaign manager wa TAL tena kwa kujitolea.

Bado hajasahau alipoambiwa amestaafu halafu eti anawashwawashwa mdomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…