Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo Novemba 16, 2020 anamuapisha Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia atawaapisha Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango na Prof. Palamagamba Kabudi Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Kwa gesture ya Dkt. Mwinyi pale alipokaa ni kama ana woga au hofu fulani hivi, kama haamini kinachotokea maana muda wote anasugua viganja huku akitupa jicho huko na huko.

Kweli damu za watu si mchezo, lazima zikuamishe kimawazo!
 
Huwa ninacheka kwa nguvu nikisikia kuwa serikali hii inabana matumizi, unakuta shughuli ya kuapishwa kama hiyo wanakwenda mpaka mawaziri wakuu wastaafu mfano Melecela, Lowasa nk. Hao wote wanalipwa kuhudhuria hiyo hafla, ni kipi cha maana wao wanaenda kukifanya?
 
Wasipoenda utasikia mkisema wastaafu wamesusa.
 
Wasipoenda utasikia mkisema wastaafu wamesusa.

Tafuta popote nilipowahi kusema wastaafu wamesusa. Nilitarajia ungeniambia tija ya hao wazee kuwepo kwenye hizo hafla, mfano Melecela na umri alio nao na hali yake kiafya. Ni kweli JK alikuwa anafuja fedha za umma kwa safari zisizo na tija huko ng'ambo, je hiki kinachoendelea sasa chini ya awamu ya tano ukiacha style ya ufujaji, tofauti ya ufujaji iko wapi?
 
Back
Top Bottom