Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,669
- 12,044
Tanaambiwa Tanzania tuna Rais Dikteta, mnyanyasaji, anae ua upinzani, katili n.k
Sasa tujiulize kitu hivi Kama kweli hayo yasemwayo je inawezekana vipi Dikteta akawa anatoa Ruzuku kwa vyama vingine vya siasa jambo ambalo ni haramu katika utawala wowote ule wa Kidikteta duniani.
Vyama vya siasa vipya kila siku vinasajiliwa kisheria na vinapata stahiki zake. Hapa kuna udikteta kweli?
Hivi hili likoje hasa, serikali inayo ongozwa na Dikteta inatoa Ruzuku mabilioni kwa vyama vya siasa?
Ni Tanzania pekee ndio kuna udikteta wa hivi au kuna mifano mingine kwingineko duniani.
Au hii ni sera mpya ya upinzani??
Kama ni sera mpya je wameifikilia vizuli hii sera kuwa itakuwa na nguvu gani kwa jamii.??
Je wananchi wa Tabora ambao wameletea maji toka ziwa Victoria hadi Tabora kukomesha adha ya maji sera hii wataielewa kweli hii.
Kama ikiwa hivi basi ninahakika porojo ya kuibiwa kura itajirudia tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Na tamko la kuto kumtambua Rais aliyeko madarakani na serikali yake litajirudia tena.
Huku wakiwa kwenye majukwaa watasikika wakisema tunaomba Rais utende hili na lile.
Hapo watakuwa wamesahau kuwa walisema hawamtambui
=====

Ruzuku sio kipimo cha udikteta na hakiwezi kutumika kama vyama vya siasa vinaendelea kuwepo!! Lakini dikteta atahakikisha vyama za siasa vinakuwepo ili kuhalalisha dhana kwamba sio dikteta. Kuna vyama vya siasa Rwanda na Uganda, Sudan na Gabon!!
Ukitaka kupima udikteta kuna kipimo kimoja tu - ni nani anafanya maamuzi ya nini kifanyike!! Dikteta hasikilizi wa kukubali wengine waamue au wajadili kitu chochote. Maamuzi ni yake mwenyewe na hayapingwi wala kujadiliwa.
Madhara ya dhana hiyo ndio husambaa kwa walio chini katika maeneo yao ya kikazi na hivo kuonekana kuna mambo mengi au si ya haki, huenda bila kufuata taratibu nk. Mifano;
a) Vyama vya siasa vifanye siasa wakati wa uchaguzi tu wakati yeye akipokea wanachama wa CCM kwenye kamisheni za majeshi, kusema “CCM Oyee” kwenye maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar (jambo la kitaifa)
b) Manunuzi ya ndege bila kufuata taratibu na bila kuweka uwazi.
c) Serikali kuamua kununua korosho na huku ikiwa haina uwezo. Kutokea kwa dhuluma katika jambo zima.
d) Majeshi ya usalama kuingia katika siasa na viongozi wake kutoa matamko ya kisiasa. Wote hao ni wateule wa Rais.
e) Wakuu wa wilaya na mikoa kuzuia shughuli za kisiasa katika maeneo yao kwa kisingizio kuwa watu wafanye maendeleo.
f) Viongozi wa CCM kuonesha kuwa maendeleo ya maeneo mbalimbali yanahusiana na viongozi wa maeneo hayo wanatoka vyama gani. Utasikia sentensi “maendeleo hayana chama” ikitamwa wakati mmoja na “mkitaka maendeleo chagua CCM”
Kama unashindwa kuona hata mambo haya machache, kuna walakini na uwezo wako wa kutambua mambo. Na sishangai huenda wewe ni mmoja wa viongozi wetu waheshimiwa.