Rais Magufuli ni Dikteta anayetoa Ruzuku kwa vyama vya siasa!

Rais Magufuli ni Dikteta anayetoa Ruzuku kwa vyama vya siasa!

Hoja Tope tupu...magufuli hatoi ruzuku ni sheria ndio inatoa na kaikuta


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Dam55,
Ungejiuliza kwanza Je hiyo ruzuku ni Pesa ya MAGUFULI. Sheria inayosema Opposition wapewe ruzuku alitunga Magufuli. Hivi ninyi akili zenu zinahama mbona mmechanganyikiwa. Sheria zipo wazi rais ni kiongozi kwa kufuata katiba yetu. Huyo Magufuli wako hana uwezo wa kuzuia ruzuku. Anayoyafanya kwa sasa ni kinyume cha katiba yetu ndio maana ANAITWA DIKTETA. Na siyo uongo Magufuli ni dikteta ila muda wake inakuja soon. Mtamkimbia nyie vigeugeu
 
Dam55,
Nakumbuka Magufuli akihutubia Zanzibar alimshangaa Dr Shein kwanini anasaini stahiki za Maalim Seif wakati anampinga,anasema angekuwa yeye asingeambulia chochote!

Hapa unaona jamaa yuko tayari kumnyima mtu haki yake ambayo ipo kisheria kisa tu wana tofauti!Huo sio udikteta?
 
MATAGA siku hizi mmmepotea?
mlikuwa jandoni nini?

akili zako zipo chini sana, sawa na kichaa, tangu lini raisi akatoa RUZUKU? sijui umeishia la ne au la saba? RUZUKU IPO KWA MUJIBU WA SHERIA NA INATOLEWA KISHERIA, huko kwenu mkoani sijui kwanini mnakuwa wajinga namna hii, yani mkoa wako umekuwa wa 25 kitaifa, bado hata mambo madogo hujui, kila kitu unahisi ni hisani ya rais, hadi mkeo akipata ujauzito utakuja kumshukuru raisi
 
Ruzuku sio kipimo cha udikteta na hakiwezi kutumika kama vyama vya siasa vinaendelea kuwepo!! Lakini dikteta atahakikisha vyama za siasa vinakuwepo ili kuhalalisha dhana kwamba sio dikteta. Kuna vyama vya siasa Rwanda na Uganda, Sudan na Gabon!!

Ukitaka kupima udikteta kuna kipimo kimoja tu - ni nani anafanya maamuzi ya nini kifanyike!! Dikteta hasikilizi wa kukubali wengine waamue au wajadili kitu chochote. Maamuzi ni yake mwenyewe na hayapingwi wala kujadiliwa.

Madhara ya dhana hiyo ndio husambaa kwa walio chini katika maeneo yao ya kikazi na hivo kuonekana kuna mambo mengi au si ya haki, huenda bila kufuata taratibu nk. Mifano;

a) Vyama vya siasa vifanye siasa wakati wa uchaguzi tu wakati yeye akipokea wanachama wa CCM kwenye kamisheni za majeshi, kusema “CCM Oyee” kwenye maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar (jambo la kitaifa)
b) Manunuzi ya ndege bila kufuata taratibu na bila kuweka uwazi.
c) Serikali kuamua kununua korosho na huku ikiwa haina uwezo. Kutokea kwa dhuluma katika jambo zima.
d) Majeshi ya usalama kuingia katika siasa na viongozi wake kutoa matamko ya kisiasa. Wote hao ni wateule wa Rais.
e) Wakuu wa wilaya na mikoa kuzuia shughuli za kisiasa katika maeneo yao kwa kisingizio kuwa watu wafanye maendeleo.
f) Viongozi wa CCM kuonesha kuwa maendeleo ya maeneo mbalimbali yanahusiana na viongozi wa maeneo hayo wanatoka vyama gani. Utasikia sentensi “maendeleo hayana chama” ikitamwa wakati mmoja na “mkitaka maendeleo chagua CCM”

Kama unashindwa kuona hata mambo haya machache, kuna walakini na uwezo wako wa kutambua mambo. Na sishangai huenda wewe ni mmoja wa viongozi wetu waheshimiwa.
 
Retired, Ndio maana mnaonekana ni kama vimbwa vinavyobweka hovyo!

Sasa kama ni kwa mujibu wa sheria, huyo unayemwita dikiteta si ndio anaesimamia hizo sheria?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ndiyo tatizo kubwa la Watz wengi.Wanadhani "ruzuku na huduma" mbali mbali zitolewazo na serikali kwa raia ni hisani. Ni umbumbumbu wa waliosoma na wasio soma!

Kwa wenye kutambua haki,wajibu na Katiba rais ni raia aliyepewa jukumu la kusimamia na kuongoza shughuli za nchi na siyo kila kitu. Ruzuku kutolewa ni "takwa la Katiba" yetu ya sasa (licha ya mapungufu na kukanyagwa/kusiginwa) wakati mwingine. Tutambue HAKI NA WAJIBU kwa kila mmoja wetu kwa nafasi tulizonazo ktk jamii.
Dikiteta anaheshimu sheria? Kama hizo ulizoelezea hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dam55,
Ruzuku haitolewi kwa chama kipya au cha zamani kisicho na mbunge, na mtoaji si Magufuli ni serikali. Maji ya Tabora havipewi vyama vya upinzani ni wananchi, na bila wananchi Rais hana kazi.
Uwezo wako wa kufikiri na kutoa hoja bado ni wa kitoto.
 
Back
Top Bottom