Tanaambiwa Tanzania tuna Rais Dikteta, mnyanyasaji, anae ua upinzani, katili n.k
Sasa tujiulize kitu hivi Kama kweli hayo yasemwayo je inawezekana vipi Dikteta akawa anatoa Ruzuku kwa vyama vingine vya siasa jambo ambalo ni haramu katika utawala wowote ule wa Kidikteta duniani.
Vyama vya siasa vipya kila siku vinasajiliwa kisheria na vinapata stahiki zake. Hapa kuna udikteta kweli?
Hivi hili likoje hasa, serikali inayo ongozwa na Dikteta inatoa Ruzuku mabilioni kwa vyama vya siasa?
Ni Tanzania pekee ndio kuna udikteta wa hivi au kuna mifano mingine kwingineko duniani.
Au hii ni sera mpya ya upinzani??
Kama ni sera mpya je wameifikilia vizuli hii sera kuwa itakuwa na nguvu gani kwa jamii.??
Je wananchi wa Tabora ambao wameletea maji toka ziwa Victoria hadi Tabora kukomesha adha ya maji sera hii wataielewa kweli hii.
Kama ikiwa hivi basi ninahakika porojo ya kuibiwa kura itajirudia tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Na tamko la kuto kumtambua Rais aliyeko madarakani na serikali yake litajirudia tena.
Huku wakiwa kwenye majukwaa watasikika wakisema tunaomba Rais utende hili na lile.
Hapo watakuwa wamesahau kuwa walisema hawamtambui
=====