Rais Magufuli ni Dikteta anayetoa Ruzuku kwa vyama vya siasa!

Rais Magufuli ni Dikteta anayetoa Ruzuku kwa vyama vya siasa!

Ruzuku ipo kwa mjibu wa katiba na sio matakwa ya Magufuli alivyo na roho mbaya kama yangekuwa matakwa yake angekuwa ameshasitisha!
Ni dikteta gani duniani anaye ongoza kwa matakwa ya katiba ya nchi??
 
Dam55,
Uzi wa kijinga sana huu. Kwani kuna uhusiano gani kati ya UDIKTETA na matumizi ya fedha za Serikali. Wengine muwe mnasoma tu threads za wenzetu siyo lazima kila mmoja aandike.
 
Kama ipo kwa mujibu wa katiba na anatekeleza takwa hilo ina maana anailinda na kuiheshimu katiba na ninavyofahamu utawala wà kidekteta hauheshimu katiba. Hapo unasemaje kamanda?
Mkuu hapo ndo panashangaza sasa hebu atupe majibu hapo.
 
Retired,
Mkuu dikteta wa wapi huyo anayefataga sheria na katiba ya nchi husika, madikteta hawafati sheria mkuu.
 
mikedean,
Dah we jamaa asee, mmh hebu tuwekee hapa huo ushahidi wa kura kuibiwa.
 
Hili ndiyo tatizo kubwa la Watz wengi.Wanadhani "ruzuku na huduma" mbali mbali zitolewazo na serikali kwa raia ni hisani. Ni umbumbumbu wa waliosoma na wasio soma!
Kwa wenye kutambua haki,wajibu na Katiba rais ni raia aliyepewa jukumu la kusimamia na kuongoza shughuli za nchi na siyo kila kitu. Ruzuku kutolewa ni "takwa la Katiba" yetu ya sasa (licha ya mapungufu na kukanyagwa/kusiginwa) wakati mwingine. Tutambue HAKI NA WAJIBU kwa kila mmoja wetu kwa nafasi tulizonazo ktk jamii.
Mkuu samahani naomba kuuliza, wewe ni msomi?
 
Tatizo letu sio kutolewa Ruzuku au kutokutolewa Ruzuku tunataka Uhuru wa kujieleza Uhuru Kutoa maoni yetu uenda Mh Rais Ana Nia nzuri kbs ila lazima akubari Kuna kundi la watu wanatumia sera zake za kibabe kuumiza Raia wake hakika mtaani Hali ni Mbaya sana hkn mwenye uhakika wa kuona kesho yke naweza kusema Dhuruma imekuwa kubwa kuliko tawala zote Tanzania yetu ukijaribu kusema tu basi ujue km sio utakajishaji pesa basi Uhujumu uchumi unakungoja hakika Keko Segerea Butimba Maweni Hali ni mbaya sna...

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu, hivi Uhuru wa kutoa maoni na kujieleza unahisisha mambo yepi?
 
Samahani sana kama utakwazika; lakini una miaka mingapi? Inaelekea bado kwenye umri unaokufanya uamini kuwa baba yako ndie mwenye akili na nguvu kuliko mtu yeyote duniani (na dunia kwako ni mtaani au kijijini kwenu).
Samahani Kama utakwazika mkuu, umesoma mada inahusu nini??
 
Back
Top Bottom