Rais Magufuli ni Dikteta anayetoa Ruzuku kwa vyama vya siasa!

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,044
Tanaambiwa Tanzania tuna Rais Dikteta, mnyanyasaji, anae ua upinzani, katili n.k
Sasa tujiulize kitu hivi Kama kweli hayo yasemwayo je inawezekana vipi Dikteta akawa anatoa Ruzuku kwa vyama vingine vya siasa jambo ambalo ni haramu katika utawala wowote ule wa Kidikteta duniani.

Vyama vya siasa vipya kila siku vinasajiliwa kisheria na vinapata stahiki zake. Hapa kuna udikteta kweli?

Hivi hili likoje hasa, serikali inayo ongozwa na Dikteta inatoa Ruzuku mabilioni kwa vyama vya siasa?
Ni Tanzania pekee ndio kuna udikteta wa hivi au kuna mifano mingine kwingineko duniani.

Au hii ni sera mpya ya upinzani??
Kama ni sera mpya je wameifikilia vizuli hii sera kuwa itakuwa na nguvu gani kwa jamii.??

Je wananchi wa Tabora ambao wameletea maji toka ziwa Victoria hadi Tabora kukomesha adha ya maji sera hii wataielewa kweli hii.

Kama ikiwa hivi basi ninahakika porojo ya kuibiwa kura itajirudia tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Na tamko la kuto kumtambua Rais aliyeko madarakani na serikali yake litajirudia tena.

Huku wakiwa kwenye majukwaa watasikika wakisema tunaomba Rais utende hili na lile.
Hapo watakuwa wamesahau kuwa walisema hawamtambui

=====
 
Ruzuku ipo kwa mjibu wa katiba na sio matakwa ya Magufuli alivyo na roho mbaya kama yangekuwa matakwa yake angekuwa ameshasitisha!
Kama ipo kwa mujibu wa katiba na anatekeleza takwa hilo ina maana anailinda na kuiheshimu katiba na ninavyofahamu utawala wà kidekteta hauheshimu katiba. Hapo unasemaje kamanda?
 
Dikteta akawa anatoa Ruzuku kwa vyama vingine vya siasa jambo ambalo ni haramu katika utawala wowote ule wa Kidikteta duniani.
Rubbish! Udikiteita unapimwa kwa kutoa ruzuku? Kwani anatoa yeye au sheria inamtaka afanye hivyo! Ndio udikiteita wenyewe kujifanya anatoa fadhila wakati sheria inamtaka afanye hivyo!


10 Ways to Tell if Your President Is a Dictator

1. Systematic efforts to intimidate the media.

2. Building an official pro-president media network.

3. Politicizing the civil service, military, and the domestic security agencies.

4. Using government surveillance against domestic political opponents.

5. Using state power to reward corporate backers and punish opponents.

6. Stacking the Judiciary.

7. Enforcing the law for only one side.

8. Really rigging the system.

9. Fear mongering.

10. Demonizing the opposition.
 
Kabla hujapost jaribu kufuatilia mambo kwa undani ili kama hujaelewa ujuzwe.Kwanza katiba inataka vyama vipewe ruzuku.Hii sio hisani ya magufuli.

Lakin haihitaji kuwa na akili timamu kujua CCM wanaiba kura hata kichaa anajua hayo.Hata wanaccm wenyewe wanajua.Je,unajua yale ya Jecha?Au,unaona yaliyotokea Zanzibar ni ndoto za Alinacha?Ccm haipwendi mjini na vijijini.kilichobaki ni udikteta tu.

Nna ushahidi wa wizi za kura kwa majimbo ya vwawa kwa huyu sijui ni waziri wa kilimo,huyo hata sasa hawezi kwenda kuita hata mkutano wa hadhara pale Vwawa maana hakubariki mashambani hakubaliki mjini.Pia mbeya Vijijini waliiba kura maana Njenza hakubariki hata kidogo.Mifano ipo mingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dam55,

Hili ndiyo tatizo kubwa la Watz wengi.Wanadhani "ruzuku na huduma" mbali mbali zitolewazo na serikali kwa raia ni hisani. Ni umbumbumbu wa waliosoma na wasio soma!

Kwa wenye kutambua haki,wajibu na Katiba rais ni raia aliyepewa jukumu la kusimamia na kuongoza shughuli za nchi na siyo kila kitu. Ruzuku kutolewa ni "takwa la Katiba" yetu ya sasa (licha ya mapungufu na kukanyagwa/kusiginwa) wakati mwingine. Tutambue HAKI NA WAJIBU kwa kila mmoja wetu kwa nafasi tulizonazo ktk jamii.
 
Hakika JF sasa low IQ imechukuwa nafasi. Hill ni jambo LA kikatiba kama vyama vyenyewe vilivyo vya kikatiba.
Haipendi ruzuku na havipendi vyama vya upinzani, lakini hana LA kufanya zaidi ya kufanya ukandamizaji tuu.
Atunge sheria ya kufuta ruzuku uone jinsi chama chake kama hakijawa cha kwanza kufa au aone atakavyo shukiwa na wafadhili wake kama alipo tangaza kuhusu watoto wa kike na kisomo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo letu sio kutolewa Ruzuku au kutokutolewa Ruzuku tunataka Uhuru wa kujieleza Uhuru Kutoa maoni yetu uenda Mh Rais Ana Nia nzuri kbs ila lazima akubari Kuna kundi la watu wanatumia sera zake za kibabe kuumiza Raia wake hakika mtaani Hali ni Mbaya sana hkn mwenye uhakika wa kuona kesho yke naweza kusema Dhuruma imekuwa kubwa kuliko tawala zote Tanzania yetu ukijaribu kusema tu basi ujue km sio utakajishaji pesa basi Uhujumu uchumi unakungoja hakika Keko Segerea Butimba Maweni Hali ni mbaya sna...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dam55,

Samahani sana kama utakwazika; lakini una miaka mingapi? Inaelekea bado kwenye umri unaokufanya uamini kuwa baba yako ndie mwenye akili na nguvu kuliko mtu yeyote duniani (na dunia kwako ni mtaani au kijijini kwenu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…