Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Hawalazamishi wala hawana uwezo wa kulazimisha. Ongea na Diwani wako, na Mbunge wako, waambie kuwa hutaki aongezwe muda. Hayo ni maoni yako, wewe mpiga kura mmoja, Diwani naye atakusanya mwoni ya wapiga kura wote.

Na mbunge hivyo hivyo, watakwambia maoni ya walio wengi. Ukiona wengi wanataka aongezwe, nenda kwa tundulissu, ema kule aliko EU, au kupitia kwa Mnyika Ufipa Street Kinondoni.

Watakupongeza, watakupokea kwa mikono miwili. Sasa tuvumiliane hadi 2025 Uchaguzi Mkuu wapambanishe Ilani. Mkishinda, mmeshinda, hatoongezwa. Lakini mkishindwa tafuta shoka uanze kukata tamaa ukisubiri 2030,
 
Kwani katiba inasemaje jamani? Nahao wanao shadadia kuongeza Muda hawajuwi wana vunja katiba na wanaweza kushitakiwa? Last kwani hawaja msikia akisema hataki kuongeza hata siku moja?
 
Tanzania hii ni kubwa, ina watu wa kila aina...kwa kuwa hiyo kura unayoisemea itahusisha wananchi wote na siyo kikundi kidogo cha watu,unaweza shangaa anaibuka na uungwaji mkono wa 100 kwa 100..usikute hata wewe ukamuunga mkono
 
Tanzania hii ni kubwa,ina watu wa kila aina...kwa kuwa hiyo kura unayoisemea itahusisha wananchi wote na siyo kikundi kidogo cha watu,unaweza shangaa anaibuka na uungwaji mkono wa 100 kwa 100..usikute hata wewe ukamuunga mkono
Hata kwa mtutu wa bunduki,siwezi kuunga mkono wazo hili.
 
Magufuli katu hataongezewa hata siku moja, yeye mwenyewe analitambua hilo na ameshalikubali.

Kwasasa atajaribu kufanya yote anayoyatamani ndani ya muda uliobaki.

Na karata ya mwisho ni kujaribu kumwachia nchi mrithi anayeamini ataendeleza pale alipoishia.
 
Kwani Magufuli huwa anategemea kura halali?Zitachakachuliwa kama kawaida kwa manufaa ya matumbo ya wachache!
Kabisa, nimeshangaa hata salary slip anapendekeza njia ya kura! Linapokuja suala la njia ya kura, ni wazi Magufuli atapata 100% na hakuna kura hata moja itaharibika, maana huwa hategemei kura, bali huagiza kuwa anataka kura kiasi gani.
 
Maghufuli ameona miradi yake ya kukurupuka haitaisha na mda unayoyoma , na ameliingizia hasara Taifa, anataka ajiongezee mda , Ila kama Mungu angekuwa anasikia huyu jamaa hatakiwi kabisa kujiongezea mda , miaka yake 10 ya mateso imetosha aiseee..... Mungu si utusikie Tu hili ombi jamani , huyu mtu arudi Tu kwao......Hili Taifa linahtaji huruma za Mwenyezi Mungu kuliko wakat wwte
 
Hapo mtoe butiku na makamba
 
Hata m7 alisema hivyo
 
anasema uwongo ndio wanasemaga ivyo ivyo anataka aonekane alilazimishwa ila yeye hakupenda waongo sana hawa msidanganyike na maneno yake
 
HABARI: Rais John Magufuli amesema hawezi kukaa kwenye urais miaka 20 kama alivyoombwa na Mbunge, Steven Ngonyani kwa kuwa ni kinyume na katiba.

Mh Rais anahutubia muda huu hapa Korogwe Stand,Tanga.

mbona magufuli na ccm wanavunja sana katiba ? anasemaje atalinda kitu anayoivunja ??
 
Magufuli hawezi kupata hata 5% kama kuna uchaguzi wa huru na haki.... say uchaguzi usimamiwe na EU kila ngazi, hatoboi
 

Na hata wapambe wake wanajiuliza wataficha wapi nyuso zao pindi hasara aliyoingiza nchi hii itakapoanza kuwekwa wazi. Hivyo wanataka aendelee kukaa madarakani ili ukweli usifahamike.
 
Hayo maneno atakuja kuyajutia tu siku za usoni wakati tamaa ya kuendelea kutawala itakapo endelea kumuwakia moyoni mwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…