Rais Magufuli, umewadhalilisha sana wanawake weusi nchini

Rais Magufuli, umewadhalilisha sana wanawake weusi nchini

Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Hamna cha utani
 
Ni kweli. Lakini watu hawawezi kuacha kusema kisa tu huwezi kubadilika. Kama unakojoa kitandani, utasemwa siku zote. Kibaya zaidi, tabia hiyo watu wanaweza kuichukulia kama kigezo cha kufanya maamuzi fulani, mfano akina mama kuamua kumnyima kura kwa kuonekana kuwa anawanyanyapaa.
Hao kina mama ndio wanaompa kura nyingi sana kwani kajenga zahanati nyingi mikoani.

Pia msaidizi wake mkuu ni Samia ambaye ni mama mwenye kuheshimiwa.

Ni humu mitandaoni ambapo tunajifanya hatumuelewi JPM lakini huko mitaani masuala Haya ni ya kawaida sana yakichukuliwa kama ni masihara ya mwanasiasa.

Kura nyingi za CCM ni kutoka kwa kinamama kuliko wanaume.

Kinamama ndio watumiaji wa visima vya maji, ndio wajasiriamali wenye vitambulisho vya kufanya biashara. Ndio wapiga kura.
 
Nawashangaa wale wote mnaosema huu ni utani!,Bila shaka mnaweza kuwa wendawazimu,Hebu fikiria kauli hii angeisema Donald Trump mbele ya kadamnasi kama huko Marekani kungekalika na uenda isingekuwa Marekani tu bali mpaka nchi zetu hizi zingeongea sana kuhusu kumdhalilisha na kumbagua mwanamke mweusi,Hakuna mtu anayekataa utani maana nchi yetu na makabila yake yamebaki kama utani lakini hakuna utani kwenye rangi za ngozi za watu katikati ya dunia ambayo watu weusi tunapambana na ubaguzi kwa ndugu zetu wanaoendelea kubaguliwa duniani kote!,Hii kauli imewaudhi watu wengi sana ikiwemo hata hao viherehere wa kusifu na kuabudu kil a kitu!,ni basi tu hawawezi kusema lakini hakuna aliyependa na sidhani hata mke wake kajisikia vizuri,Hata hivyo yule mama always hakuna ambacho huwa kinampa furaha kutoka kwa huyo mzee ni basi tu keshakuwa mke wa rais hana cha kufanya zaidi ya kujipatia maumivu ndani kwa ndani huku akionyesha tabasamu feki!.

HEBU FIKIRIA HII KAULI INGESEMWA NA MPINZANI WAKE WA KISIASA NDUGU TUNDU LISU!,BILA SHAKA TUNGESIKIA KAKIKUNDI KA AKINA MAMA FULANI WANAITISHA PRESS CONFERENCE NA KUMTAKA AOMBE RADHI NA ISINGEISHIA HAPO TU BALI WANGEANDAMANA NA KUWEKA MASHINIKIZO KADHAA!

Bora JPM anayeishia kwenye kauli kuliko Mbowe aliyesababisha bavicha kanda ya kusini walalamike kuwa wale wa kaskazini wanapendelewa.

Trump ni Trump na Magu ni Magu, ni watu wawili tofauti wenye majukumu tofauti ya kiuongozi.

Nongwa haziwezi kumsaidia mtu hata siku moja. Yaliyoongelewa pale uwanja wa taifa kulihusu jiji la Dar yana umuhimu wa kujadiliwa kuliko hizi inferiory complex za mtu mmoja mmoja.
 
Mjinga mmoja, kwa watanzania ambao ni wengi na wasokua na elimu... Watamtafasiri km mwenye utani???

Unadhan mwanamke wakijijin kauli kama hii kaisikia, anaweza kupiga hatua kuelekea Ofisin kwake ????

Mnatetea mpaka na upuuuzi
Wewe ndiio mjinga kweli alikwambia kijijini watu ni weusi Nani?rangi ya ngozi NI character ya kurithi
Au wewe mwenzetu unarumia mkorogo,
Eti mwanamke was kijijini
Labda kijijini kwwenu
Mshamba mkubwa
Halafu hv mwanamke gani mweusi ajshindwe kumuona magu?labda wewe usiejiamini
 
View attachment 1595438

Kauli yako uliyoitoa leo hii, eti huyo mgombea wako cheupe akija Ofisini mwako utamuhudumia haraka kuliko hata wanawake weusi.

Ni Udhalilishaji na Unyanyasaji wa kijinsia, umeonyesha wazi kuwa wewe ni mbaguzi wa rangi.

Kumbe ndo maana wanawake weupe weupe wanakula Mema ya nchi huku wachache weusi ukiwateua sababu ya Elimu zao?

Umewaumiza Kihisia, umewaumiza kiakili wanawake Weusi.

Hivi Leo mwalimu wa shule ya msingi atakuonaje?
Mama Janeth ni mvumilivu kuliko Wanawake wote wa Tanzania
 
Hivi Kwa mfano mwanamke mwenye mme awe flat screen halafu mumewe aongee hadharani kwamba anapenda chogo tv halafu axeme huu ni utani sidhani kama itakuwa imekaa vizuri.

Tatizo la Magu hajui angle za kutania ni Sawa na umkute mwanamke kazaa watoto wengi halaf umwambie kuwa anazaa kama panya kisha useme ni utani sidhani kama atakuchukulia poa.

Au kumwambia mama Samia kuwa yeye ni mweupe na ni mzuri hivyo anapofanya naye kazi hapati stress huu si utani wenye afya nzuri.
 
Mimi hapa mweusi na sijaumia chochote
Labda Kama wee mtoa mada umeumia pole Sana mwanamke mwenzangu

Tena mwisho akasema i mnajua Tena wasukuma!!!!
Alimaanisha wasukuma wanapenda wanawake weupe na aalitania
hebu tupiamo kapicha tukuone weusi wako mkuu 😀
 
Nawashangaa wale wote mnaosema huu ni utani!,Bila shaka mnaweza kuwa wendawazimu,Hebu fikiria kauli hii angeisema Donald Trump mbele ya kadamnasi kama huko Marekani kungekalika na uenda isingekuwa Marekani tu bali mpaka nchi zetu hizi zingeongea sana kuhusu kumdhalilisha na kumbagua mwanamke mweusi,Hakuna mtu anayekataa utani maana nchi yetu na makabila yake yamebaki kama utani lakini hakuna utani kwenye rangi za ngozi za watu katikati ya dunia ambayo watu weusi tunapambana na ubaguzi kwa ndugu zetu wanaoendelea kubaguliwa duniani kote!,Hii kauli imewaudhi watu wengi sana ikiwemo hata hao viherehere wa kusifu na kuabudu kil a kitu!,ni basi tu hawawezi kusema lakini hakuna aliyependa na sidhani hata mke wake kajisikia vizuri,Hata hivyo yule mama always hakuna ambacho huwa kinampa furaha kutoka kwa huyo mzee ni basi tu keshakuwa mke wa rais hana cha kufanya zaidi ya kujipatia maumivu ndani kwa ndani huku akionyesha tabasamu feki!.

HEBU FIKIRIA HII KAULI INGESEMWA NA MPINZANI WAKE WA KISIASA NDUGU TUNDU LISU!,BILA SHAKA TUNGESIKIA KAKIKUNDI KA AKINA MAMA FULANI WANAITISHA PRESS CONFERENCE NA KUMTAKA AOMBE RADHI NA ISINGEISHIA HAPO TU BALI WANGEANDAMANA NA KUWEKA MASHINIKIZO KADHAA!
Hai tamwa sijui tgnp sijui tawla ni vikundi vya kinafki tuuuuuuu
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Acha upimbi wewe, ndiyo maana marais wana mtu wa kuwaandikia hotuba ili kuhakikisha kwamba hata kama kachomeka utani hautakuwa na tafsiri mbaya. Waswahili wana msemo kwamba tuchunge sana kauli zetu kwani zaweza kuleta madhara. Sasa wewe kwa udumavu wako wa akili na mahaba ya kipuuzi wala huwezi kuona.
 
Hajui utani kiasi kuwa anageuka kuwa mropokaji. Utani una tafsida yake. Kimsingi anapenda utani lakini utani haumpendi. Hili tumekuwa tukilisema mara nyingi kuwa huyo jamaa hana uwezo wa utani. Anapatia zaidi kwenye mambo yake ya jazba na sio utani.
Kimsingi rais wetu.anajitahd sana kuwa.na sense of humour lkn hawez. Kwenye communication skills kipengele cha socialization hakukiweza ipasavyo. Atafuta njia ya kuweka tabasamu kwenye nyuso za watu lkn kumbe ndio anasema huzunizaid
 
Mzee wa miaka 61 sidhani kama ni rahisi kumbadili tabia.

Huo ndio “udhaifu” wake. Ndio maradhi yake hayo.
But hilo halifanyi watu wasiseme ama kukosoa. Nyerere alivyowatungia kitabu akina Mzee Mwinyi, Malechela and others hao walikuwa watoto? Jibu ni kwamba walikuwa wazee /watu wazima tayari but bado Nyerere aliamua kuwakosoa.
 
Kukosoa hakukataliwi lakini sidhani kama itasaidia kitu.

Anasema yeye msukuma na wanapenda wanawake weupe, hapo huwezi kubadilisha kitu. Ni suala binafsi zaidi tofauti na Nyerere aliyeangalia mustakabali mzima wa nchi Ali poa mia kukosoa kwa kutunga kitabu.
 
Popoma mwingine huyu hapa...
Popoma ni yule anayechukulia kwa uzito kauli za masihara za mwanasiasa tena akiwa jukwaani.

Kuna mengi sana ambayo ni chanya yalisemwa kuhusu Dar na maendeleo yake na ni ya muhimu kuliko huu udaku wa mwanamke mweupe na mweusi.
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Wewe, Utani anaweza kuzungumza na watu katika setting ya kibinafsi!! Huwezi kuzungumzia rangi kama mgombea katika jukwaa huku ukimpigia kura mgombea na katika matamshi yako ukaihusisha ofisi ya Rais.

Unaweza kumtetea Rais kuwa anafanya utani, na ni kweli alikuwa anafanya utani - shida ni hajui kufanya utani. Anakosea katika utani. Na utani wake hauchekeshi bali kuzua hisia. Angepaswa kuwa ameshajifunza na kujua kuwa hana ujuzi na utani. Anaodhani ni utani, ni mzaha unaoonesha udhalilishaji na hulka ndani yake.

Hivi ni rangi ya mtu ndio inamfanya asikilizwe?? Hivi ni rangi ya mtu ndio inafanya mtu achaguliwe?? Hiyo inaacha ladha gani kwa wagombea weusi??

Halafu urudi tena hapa upinge wanawake wanatumia vipodozi vikali kubadilisha ngozi zao kuwa nyeupe. Ni kwa sababu wakisikia wanaume wanasema ngozi nyeupe ni bora - wanatamani kuwa weupe. Baadae madaktari wawaambie kuchubua ngozi kuna madhara.

Uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo sana na ndio tatizo kubwa la nchi hii. Kiwango cha kupambanua ni kidogo sana. Mambo mengi tunayaona kama hayana maana. Words have meanings, bro!! Words! Words!
 
Back
Top Bottom