Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Yeriko Nyerere give us a break
Fimbo na sime za kina Ole Ngurumwa zinahatarisha Muungano?🤧
Hivyo Wamarekan/Watanzania wasizuiwe kutembea na AR-15 machine guns barabarani
Maasai sio watu exceptional zaidi ya WaTz wengine
Sheria ikigusa masai watu wanalalamika balaa,
Wanapinga masai kuhamishwa ila watu kibao hii nchi wamehamishwa na watu wapo kimya,
 
We mwenyewe ndio unajenga hoja ktk msingi wa ubaguzi. Zanzibar nayo ina utamaduni wake, ukifika Roma fanya km waRoma, wakiinama nawe inama. Pili we huwajui vizuri wamasai, hizo sime na fimbo za nini huko mjini Zanzibar? Sime na fimbo zina mantiki kule porini, eti wametumia kujihami. Ni kwamba hizo ndiyo silaha wanazotegemea ukitofautiana nao. Wapigwe marufuku vinginevyo warudi kule porini kwao.
Zanzibar mibaguzi sana,, nimefurahi Kwa kichapo walichopewa wajukuu chotara wa mwarabu
 
Mbona ukeketaji watu wameelimishwa, wakaacha,na ilikuwa utamaduni wa baadhi ya jamii.

Sasa kwa dunia ya artificial intelligence, hayo mafimbo na marungu, na mavisu yana faida gani? Ni sawa na kukomalia kulala porini Ngorongoro, bila nyumba eti utamaduni

Hizo fimbo ni za kuchungia ngombe, wana ngombe huko zanzibar hao wamasai? Kuna simba zanzibar kwamba watakutana naye wapambane naye kwa kutumia hizo silaha?

Utamaduni wa konyo
Utamaduni wa hovyo tu
 
Serikali ya mapinduzi inapotoshwa kwa hili la wamasai. Kuna chuki kubwa za kidini dhidi ya jamii Za watanganyika
Ila kwa ajili ya siasa watakanusha , wafute tangazo lao kimyakimya dhidi ya wamasai.
Mangi.. SI Kila kitu chuki ya dini nyingine ni taratibu na Sheria zinazolinda usalama wa raia
 
Utamaduni wa Wamasai kutembea na Visu na virungu ni wanapokuwa Kwao ambako kiasili ni Mbugani so wanapigana na Wanyama na wadudu wengine hatari

Sasa kwenye nchi iliyostaarabika kama Zanzibar unatembeaje na Rungu na Sime mitaani kwa wala urojo?

Wamasai waache uporipori🐼
 
Nina laani kwa nguvu zote kitendo cha vurugu za mgambo na watu wa jamii ya kimasai kwakupigana hadharani, Nina laani Masai kushambulia Mgambo, Nina laani kwa nguvu kubwa Mgambo wa Zanzibar kushanbulia watu wa jamii ya kimasai! Jambo hili halikubaliki kwa mjibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza kupigana hadharani au kificho.

Lakini naomba nitofautiane na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Zanzibar, Amri kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime/visu vyao, Ni Kauli Haramu na ya kibaguzi inayohatarisha muungano wa Tangabyika na Zanzibar.

Ifahamike kuwa Fimbo na Sime kwa Jamii za kimasai ni sehemu ya “vazi lao la asili”, ni Sehemu ya utamaduni wao, Ni Identity yao, na hivyo kujaribu kwa aina yoyote kuondoa kimoja wapo katika hivyo vinavyokuwa ndani ya mwili wa Masai ni kutangaza kuwafukuza Wamasi Zanzibar, Hili ni tangazo la kijinga limekurupukwa na mamlaka za Zanzibar!

Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo, hakujawahi kuwa hatari kwa raia yoyote, Kwanini iwe leo baada ya Masai kujihami waliposhambuliwa na mgambo wa mji? Serikali ya Rais @dr.hmwinyi itafute jawabu la kumaliza mzozo huu sio kufunika kwakuwafukuza Wamasai, Tatizo liko kwa mamlaka za jiji, Tatizo liko kwa Wakuu wa Mikoa, na mamlaka zingine za jiji.

Unawazuia Wamasai wasibebe fimbo unataka Wabebe Vikapu vya Nazi na vigemeo vya Litembo? Unataka wabebe Usinga? Unataka wabebe karafuu? Noooo nooo tukatae unyanyasaji huu kwa jamii ya kimasai! Ukamilifu wa Masai ni fimbo na sime. Sasa unaka awe na shuka tu kama dera?

Kesho yataibuka Bara Wapemba watashambuliwa, Je serikali iweke amri wapemba wasizaliane kwa Wingi Bara ambao ni sehemu ya utamaduni wao? Nooo Nooo! Tukatae ubaguzi huu.

Mh Rais @dr.hmwinyi ili kunusuri maafa zaidi na kuoondoa hii taswira mbaya ya ubaguzi iliyotengenezwa na mamlaka za mji hapo Unguja, Ninakuomba na kukusihi Mh Rais, tengua hii kauli ya kibaguzi, Haifai kutolewa na kiongozi wa serikali katika ulimwengu wa leo! Madhara yake ni makubwa zaidi mbeleni.

Serikali ijifunze kutatua migogo kwa hekima na busara, Majibu ya hasira ya kiserikali yanaweza kuleta maafa zaidi kuliko kutatua, Nimeisikiliza kauli ikitolewa na yule kiongozi wa mjinibZanzibar (Unguja) ni wazi alitawaliwa na ghadhabu zaidi kuliko hekima ya kiuongozi, Amewahukumu Wamasai bila kujaribu kujua undani na kutafuta jawabu, Badala yake ametafuta jibu ambalo ni la hovyo zaidi!,

Nimesikitika sana kwa kauli hii ya serikali ya Zanzibar katika zama hizi za utandawazi na utandaridhi! Utengamano wa taifa letu ni muhimu kuliko hizi chuki zinazokolezwa na namlaka za nchi!

Na Yericko Nyerere
View attachment 2890368
Kweli watu wanabadilika! Huyu si ndiyo 'YERICKO NYERERE' aliyekuwa anaonekana kama 'Great thinker' kwa makala zake mbalimmbali zenye akili hapa JF? Mimi nadhani kuna mtu atakuwa anatumia ID yake.

Sikutarajia makala ya namna hii yaandikwe na mtu kama YERICKO NYERERE mtu ambaye wakati fukani alionekana kama 'Great thinker hapa JF! Yaani wamasai kukatazwa kutembea na fimbo na masime baada ya kufanya 'tukio la kihalifu' iwe sababu ya kuhatarisha muungano? Hivi nyinyi watu mnauelewa muungano vizuri lakini?

Kama hamuelewi waulizeni Wazanzibari, 'walipambana kwa jasho na damu' na wameshindwa!

Wamasai lazima wafuate sheria ili waendelee na shughuli zao za kimaisha, mimi naamini, hata ukiona mmasai yupo Zanzibar, ujuwe huku Tanganyika alisha kosa hiyo fursa na hata akirudi wewe huna kazi ya kumpatia

Jengine ni kwamba hata nyinyi mnaoshabikia 'upuuzi' na kujifanya kuwa na huruma na wamasai ni waongo tu, sisi tunaoishi na wamasai kwa karibu huku tunayaona mateso yao!
 
Watanganyika tuna upole uliochanganya mpaka kufikia kilele cha ukilaza.

mfano:kwa ilo tukio la masai na polisi wa Zanzibar raia wa tz wangekua ndio raia wa South,Nigeria n,k wazanzibari wangechezea kichapo huku bara mpaka huo muungano ungejuta.
 
Huu wote ni upumbavu tu, wote hao wanapaswa wachukuliwe hatua kama watanzania wengine.

Hatuwezi kuwa na sheria ambazo zinawabeba group la watu na zinakandamiza wengine.

Wasukuma ambalo ndilo kabila lenye watu wengi ufugaji ni sehemu ya utamaduni wao, ila wananyanyaswa kila kukicha na ng'ombe zao na wanaambiwa wauze mifugo yao Kwasababu hakuna sehemu za malisho. Ila kuna kabila limeachiwa hifadhi wanafuga bila kusumbuliwa na mamlaka.

Ifike mahali huu ujinga ufike kikomo na watanzania wote wawe na haki sawa
Huo upumbavu ni wewe unao sio wao dunia yote kuna jamii flan flan utazikuta hazibadiliki na kutaka kulazimisha unakuwa wewe ndio mjinga. Kenya watu wapokot Turkana na Maasai ni the same uganda wapo Namibia wapo Botswana wapo marekan wapo Scotland wapo Australia wapo nk. Hiz jamii kwanza ndizo wa
Ila bana, tuache utani, hizo sime kwa karne hii waachane nazo tu,
Kesho kutwa mm nikiwa natembe na AK47 mtaniruhusu kwa kuwa sipigi nayo mtu?
Karne gan aisee. Hiv ukimuona mwarabu kavaa kanzu unamuona ni mjinga flan sio. Au ukienda Yemen wanavyovyaa yale majambia unahc vichaa sio.
 
Huo upumbavu ni wewe unao sio wao dunia yote kuna jamii flan flan utazikuta hazibadiliki na kutaka kulazimisha unakuwa wewe ndio mjinga. Kenya watu wapokot Turkana na Maasai ni the same uganda wapo Namibia wapo Botswana wapo marekan wapo Scotland wapo Australia wapo nk. Hiz jamii kwanza ndizo wa

Karne gan aisee. Hiv ukimuona mwarabu kavaa kanzu unamuona ni mjinga flan sio. Au ukienda Yemen wanavyovyaa yale majambia unahc vichaa sio.
Ngoja nikuache akili zako ni za kijinga, hao pokot kwa kufanywa special saivi wanamiliki siraha za moto hadi wanapambana na Jeshi.

Endeleeni kuwaza kijingajinga majibu ya huu upumbavu mtayaona
 
Unajaribu kuwafokea wazenji,we kama Nani kwamfano.
Ile ni Serikali kamiri.
Tena usirudie ujinga wako huo.
Ukitaka kumjua kama wewe sio mmoja wao,nenda na hela zako ukanunue eneo tuone kama utauziwa.

Msiwapangie Cha kufanya.

Nyie kama hamna Serikali kaeni kimya.
Mzanzibari ana haki bara,kumpata au kufanya chochote,Sasa nnajizima DATA kuwa nyie sio Watanganyika😄.
By the way,CCM mbele Kwa mbele.
 
Jamani sime,rungu na fimbo sio silaha. Sime kwa ajili ya kukata nyama,fimbo na rungu ni kwa ajili ya ulinzi(self defence)
 
Kanzu ni vazi takatifu,Yesu pia amevaa.Mapadiri,maaskofu,

Hawa wamasai sio wabantu,ni wakutoka pembe ya Afrika.Na hao wenye asili ya pembe ya Afrika kama wasomali,waarabu,wa Ethiopia,wameacha mila za kutembea na silaha kama sime,visu,majambia,bakora na fimbo.Mila za kutembea na silaha ni hatarishi na zimepitwa na wakati.
Wale wanavaa majoho
 
Wewe Yeriko Nyerere, hata ukiwa Rais na ukanda serikali lazima utaipinga tu serikali yako uliyoiunda. Kama Lisu, hata akiunda serikali ataipinga tu serikali.
Fimbo za nini mjini? Kule tarime wakurya walikuwa wanatembea na sime, rungu na mapanga yakawa yanahatarisha amani. Serikali ikaona hapana. Ikakataza. Leo hii Tarime wakurya wamezoea hawatembei na silaha hizo.
Hao wamasai wasiambiwe kitu kisa wamasai. Wanyamganywe tu maana hakuna sheria inaruhusu watu kutembea na silaha.
 
Back
Top Bottom