Rais Ruto wa Kenya asema uongo juu ya chimbuko la mabaki ya binadamu wa kale. Akanywe kidiplomasia

UWONGO UWONGO WA EVELUTION WA KAZI GANI...TUNAHITAJI BANDARI
 
Kenya haiwezi kuipa Tanzania free promo na hawatakaa wafanye hivyo! Hata Sisi tumewahi kutamka kwamba "Kenya is a man eat man society Wala hatujawahi kuwapa credit kwamba Kenya is the largest economy in EA!

Solution ni sisi wenyewe kuipromote Tanzania world-wide ili waitambue "as an independent quality destination of choice" sio kulalamalalama mitandaoni!
Kazi ya TTB na wizara MNRT ni nini?! Kula Kodi za wananchi na kusangarai na ma-VIEITE tu!

Na kama unasema Mama "Anaupiga mwingi kimataifa", basi hajajafanya ya kutosha, akaze buti to neutralize such cheap Kenyan propaganda!

Watanzania kwa kulialia mko njema sana ndio maana Wakenya wanawaita "maziwa lala"![emoji3525]
 
Nilikuta bango kubwa uwanja was ndege wa Mohamed Muntali uliopo Jiji la Lagosi Nigeria,ukielekeza watali wake Kenya waone mlima Kilimanjaro.
 
Zinjanthropus alikuwa made by Allah & Islam strong? This would make him the first Muslim ever to walk the earth. Tunaomba ufafanuzi wa Kuruani.
 
Uko ouy dated sana wewe bibi' kwa akili zako unaona kakosea? Yeye sio mjinga narudia tena uko over out dated na habari za Dunia
 
Yuko sawa
 
Mleata maada yuko out dated sana
 
Wameanza maigizo yao hawa wajinga tusahau kuhusu bandari yetu, chimbuko linafaida gani kwangu?
Bandari imewashinda wamewapa waarabu waiendeshe millele, tumepiga kelele wametudharau la fuvu ndo wanataka tuwasaidie kupiga ili iweje? Upuuzi mtupu.
 
Ruto anatumia fursa tu, aliyopewa na Samia mwenyewe, sasa unamlalamikia kitu gani? Nchi hii "imefunguliwa," au wewe huelewi maana ya kufungua nchi?
Yeye Ruto kaichukulia kauli hiyo kuwa ni fursa kwa yeyote anayetaka kufaidika na tulivyonavyo hapa, kwa maana kwamba tupo wazi kabisa kama nchi kufanya biashara yoyote na mahali popote.

Ndiyo maana tumewafungulia wafanya biashara wao wa nafaka kuingia na malori yao hadi mashambani kwa wakulima.

Hebu jaribu wewe kwenda Kenya ukafanye hivyo uone kitakachokukuta!

Nchi hii ni "Shamba la Bibi", kwa maana halisi kabisa ya msemo huo.
 
Nilikuta bango kubwa uwanja was ndege wa Mohamed Muntali uliopo Jiji la Lagosi Nigeria,ukielekeza watali wake Kenya waone mlima Kilimanjaro.
view nzuri ya Mlima Kilimanjaro iko upande wa Kenya Ambosel, au eneo wanaita Loitoktok, kule ndio unaipta viewa ya kipekee,
 
Usiwashtue wasije wakaliuza na hilo fuvu mkuu.
 
Siku za nyuma kabla ya kutembea sehemu kadhaa duniani nilikuwa naamini kweli mtu wa kale alitokea Tanzania. Baada ya kutembea nchi kadhaa na kusoma vitabu mbalimbali, nimegundua karibu kila nchi husema binadamu wa kale alianzia kwao.

Kama mama Faizafox unaamini mtu wa kale alianzia hapa Tanzania, waarabu, wazungu nk walitokea wapi? Jitahidi kutoanika elimu yako mbovu uliyokaririshwa hapa Tanzania.
 
Ile Bodi ya Utalii TTB imelala sana,hawana mikakati ya maana ya kutangaza vivutio vyetu,ata juzi kati Professor Kabudi aliwapa darasa juu ya zile nyayo za mtu wa kale na alitaja sehemu nyingi ambazo hazitangazwi.
Tofauti yetu sisi na Kenya kwenye Country Branding ni kwamba sisi tunapenda kupiga siasa sana wakati wenzetu siasa ni siasa na professionalism inapewa heshima yake.Wewe chunguza ata Media za Kenya na Tanzania,uangalie nchi gani wapo serious!!
 
Hilo usemalo lipo, lakini nipo kwenye kigezo alichotumia Ruto cha ""cradle. Of human kind", hakuns palipoitwa hivyo isipokuwa Olduvai Gorge, fuvu la kale, kwa Afrika Mashariki, tunalo sisi National Museum (kama wajinga wajaliuza bado).


Mama anaupiga Kimataifa.
 
Shi
Mary na Louis Leakey kweli waligundua mabaki ya kwanza ya Homo Habilis lakini baada yao yako mabaki mengine yamepatikana Ileret, ziwa Turkana lililopo Kenya. Shida ni kuwa mnadhani Zinjathropus alikuwa ndio Adam wa kwenye maandiko wakati kinachojulikana ni kuwa evolution iliendelea katika sehemu kubwa ya Afrika Mashariki. Na tukumbuke kuwa miaka milioni 2 iliyopita hapakuwa na nchi ya Kenya au Tanzania. Kwa hiyo ni sahihi zaidi kusema chimbuko la binadamu lilikuwa Afrika Mashariki badala ya kukazania lilikuwa sehemu fulani Kenya au Tanzania.

Amandla...
 
Kuna fursa kubwa sana Tanzania kila pembe, lakini "wasomi" wetu waliopo serikalini utafikiri misukule, hawana ubunifu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…