Rais Ruto wa Kenya asema uongo juu ya chimbuko la mabaki ya binadamu wa kale. Akanywe kidiplomasia

Hiyo Olduvai Gorge ni kwa mujibu wa vitabu vya historia ya nchi yako. Labda useme Tanzania wana haki miliki ya mtu wa kale kuanzia hapa duniani. Ndio maana nakuuliza kama hivyo vitabu sio vilikuwa vinakupotosha, mwarabu na mzungu walianzia wapi na lini?
 
Manaki usemayo ni vipande vya nyani, vilikuwa dissed na ma anthropologist wabobezi.

Imi siamni kuwa Adam ni mtu wa kwanza, Niliwahi kuchokonoa hilo kwa kuanzisha mjadala lakini sikupata challenges, upo hapa 👇🏾


Nakaribisha vhallenges 👆🏾


Mama anaupiga Kimataifa.
 
Hapo ndipo tunakwama Mkuu!
Inabidi vijana tuwape. Mbinu za kutumia hizi fursa kibinafsi.


Kama kuna wasomi wa Historia humu na wenye kuweza kufanya tafiti, naweza kuwaunganisha na mtu ambae ana idea ya biashara za "anthropological, historical and cultural tourism" miaka kama mitano nyuma alinieleza idea yake ikaniingia vizuri sana.

Yaani aliponieleza nikawa nazikna fedha hizoooo. Ma shaa Allah kuna watu wamejaaliwa ubunifu.



Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Mtu mzima kama wewe kupost ujinga kama Huu JF ni kujidhalilisha. Stori zenyewe za kuungaunga.
Dah!
Bila shaka atakuwa ameelewa.
Lengo la kuwasahaulisha waTanzania swala la Bandari haliwezekani kabisa.
 
Unapotezea watu muda wao tu kwa mambo ya msingi.
 
Huyo Rais huwa ni muongo sana 😃, uliza raia wa Kenya
 
Dah!
Bila shaka atakuwa ameelewa.
Lengo la kuwasahaulisha waTanzania swala la Bandari haliwezekani kabisa.
Hilo. Mimi mbona ndiye nnaelifufua kila siku ili watu wasizisahau fursa tulizoletewa.

Kama kuna mada nazipenda humu kwa sasa basi za bandari.

Na kama kuna Rais aliyefanya la maana kuhusu bandari basi hakuna kama Mama Samia.

Nafahamu Kikwete alilianzisha la Bagamoyo lakini mwendazake akaona donge. Naamini na lenyewe sasa hivi Litachipua tena kama uyoga.


Mama Samia kufunguwa lango la bahari na. Matajiri wa Dubai, elewa kuwa kafunguwa milango million moja ya fursa Tanzania, kwa wenye kuelewa tu.


Nawaambia ngojeni kama
Hamjasikia mtu ananunuwa block zima la Kariakoo au Ilala au Kinondoni anaweka vitu vya kisasa.

Wenye exposure za investments za duniani watanielewa.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Unapotezea watu muda wao tu kwa mambo ya msingi.
Nafahamu sana mambo kama haya yanataka vichwa vilivyotulizana vyenye kuona miaka 30 mbele, kama Ruto, siyo vyenye stress kama wewe.

Mwandiko wako tu unaonesha una stress za maisha ile mbaya.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Haya nayo bado ni ya kuyataja kuwakoga watu juu yake enzi hizi?
Kwani utani imehama? Na wapi bandari ya Dar unaweza kuiona vizuri zaidi bila kuingia ndani kama siyo utani? Labda upande floor ya nane Kilimanjaro Kempinski, zikutoke.

Zamani tunanunua mihogo yetu ya kuchoma na mapilipili ya kusaga, mnakamulia na ndimu juu yake, pale opposite na St Joseph School, pembeni ya mihogo kulikuwa na mpemba ana uza juice, unabeba juice yako unasogea utani unakumbana na viti vya zege, sijuwi vya Habib Punja vile? Mnajituliza hapo. Mnatazama meli bandarini kwa raha kabisa. Mara mkungu umedondosha kungu tunaikinbilia.

Wakuja na mwenge mmeiharibu sana Dar yetu. Nendeni Dodoma huko, tuwacheni na DP World yetu tujifaraguwe.


Mama Samia anaupiga mwingi sana Kimataifa.
 
Ukiwa nje, Afrika mashariki inakuwa kama nchi moja
Mipaka si waliiweka wazungu, tunaowaona wa maana, walipogawana sfrika kama keki ya basiidei juu ya meza "divide and rule".

Wakati wanatawala himaya ya Zanzibar, yote ilikuwa moja kutokea Somalia Mpaka Msumbiji.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
binafsi, lile fuvu la sokwe la mtu wa kale, bora lionekane halipo Tanzania, wacha tu wakenya wachukue, kwasababu ni uongo na ushetani. tangu awali wanadamu wameumbwa hivi hivi tulivyo, hatukuwa sokwe namna ile, hata mambo ya olduvai gauge ni ushetani uliopandikizwa ambao hautakiwi kuendelea kufundishwa kwa watoto wetu mashuleni. kwahiyo faiza fox, tuliza tu mshono, wengi wetu hatupendi kuungana na watu wa imani hiyo ya olduvai
 
Wewe inakuuma nini ilhali hilo chimbuko la mtu wa kale halipo Zanzibar?! Singida na Manyara wapi na wapi na huko Makunduchi?

Au nalo mnataka kuwapa waarabu?!!!!

Tunataka bandari yetu na koma kututoa kwenye mstari.
Tena akomae kwelikweli.
 
Chimbuko la binadamu ni Ethiopia na alipewa jina la bandia LUCY.
 
Kama tumeuzia watu bandari kwasababu hawawezi kuendesha,tuwauzie Olduvai Gorge waKenya maana wao wanaweza kuitangaza. Au mnasemaje? Tuko kwenye biashara ya kuuza uza
Mimi nalala nikiomba Mama auzee Vivuko vyote vya TEMESA kwa Waarabu kuanzia na kile cha pale Ferry-Kigamboni,kina maudhi, Mara mashine zina feli,Mara kadirisha kamoja ka kujazia pesa kwenye kadi! Yaani mradi shida tupu!!!
 
Wewe inakuuma nini ilhali hilo chimbuko la mtu wa kale halipo Zanzibar?! Singida na Manyara wapi na wapi na huko Makunduchi?

Au nalo mnataka kuwapa waarabu?!!!!

Tunataka bandari yetu na koma kututoa kwenye mstari.
Duh! Watu mnahasira sana na Bandari yenu! Kosa lenu la kwanza mlipo iuwa team ya Bandari Daraja la kwanza! Sasa Wajanja wamepita na Bandari yenyewe!![emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Chimbuko la binadamu ni Ethiopia na alipewa jina la bandia LUCY.
Inawezekana, mimi naongelea palipoitwa na ma anthropologists "cradle of human kind" ni Olduvai Gorge.

Ambalo ndilo hilo alikuwa anawadanganya wstu Ruto kuwa ni Kenya.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…