Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kauli hii kabambe imetolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan huko Tanga, wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kwenye Chuo cha Boma Kichaka Miba Mkoani humo .

Mh Rais amesema kwamba ili kurejesha Ukakamavu kwa Askari wa Uhamiaji inapaswa wote wenye vitambi kurejeshwa kuhenya ili kupukutisha Vitambi na kurejesha Ukakamavu.

Chanzo: SwahilTimes

Toa Maoni yako
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji, Boma Kichakamiba mkoani Tanga amewataka askari wa uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni kuviondoa ili kuwa wakakamavu na wepesi zaidi katika kutimiza kazi zao.

"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia

Kwa uzoefu wako, ukiacha askari wa Uhamiaji waliosemwa na Rais Samia, ni Askari wa kikosi gani wanaongoza kwa vitambi hapa nchini?

Picha: Kwa hisani ya mtandao (Haihisuani na Habari)

Kitambi.jpeg
 
Hapo ndiyo umuhimu wa Sheria Je,ni sheria gani inayokataza mtu Kuwa na kitambi?

Hata ikitungwa Leo bado haitawahusu Wale ambao walikuwa na vitambi kabla ya kutungwa Kwa sheria.

Kwa upande mwingine inanifurahisha kwasababu Mimi sina Kitambi lakini Nina Shaka kama Hapo Haki za Binadamu zimezingatiwa hasa katika eneo Ubaguzi au ndiyo maana wote wanaungana ili kuwe na katiba Bora?
 
Back
Top Bottom