Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Mama yuko sahihi askari wamejiachia sana Serikali ya Rais Samia inataka watu wachapakazi sio hao waliozoea kula rushwa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza
katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji, Boma Kichakamiba mkoani Tanga amewataka askari wa uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni kuviondoa ili kuwa wakakamavu na wepesi zaidi katika kutimiza kazi zao

"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia

Kwa uzoefu wako, ukiacha askari wa Uhamiaji waliosemwa na Rais Samia, ni Askari wa kikosi gani wanaongoza kwa vitambi hapa nchini?

Picha: Kwa hisani ya mtandao (Haihisuani na Habari)
View attachment 2324500
Another blunder from inept leader. Hii nchi wanasiasa wanadhani wana uhalali wa kuamrisha kila kitu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza
katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji, Boma Kichakamiba mkoani Tanga amewataka askari wa uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni kuviondoa ili kuwa wakakamavu na wepesi zaidi katika kutimiza kazi zao

"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia

Kwa uzoefu wako, ukiacha askari wa Uhamiaji waliosemwa na Rais Samia, ni Askari wa kikosi gani wanaongoza kwa vitambi hapa nchini?

Picha: Kwa hisani ya mtandao (Haihisuani na Habari)
View attachment 2324500
Kwani hiyo picha ni ya nesi? Si ni ya walengwa waliotajwa?
 
Hakika hii kitu ni nzuri mno. Hivi wewe askali unapata wapi jeuri ya kuota kitambi???
Nani kakuambia kitambi ni pesa.Nenda jela ukaone wafungwa wenye vitambi.
Wengine ni stress free awazipi shida kipaumbele
 
Riziki huwa anatoa Mungu,,,,ila kitambi ni bidii yako tu....

Mama akumbushwe kuwa wapo wana vitambi lakini bado ni wepesi
 
Huu Uzi umenikumbusha mbali Sana ase..
Mzee wangu alinichekesha sn siku moja tumesimama mataa tunasubiri kuruhusiwa tukamwona traffic anaongoza magari Ila ana bonge la kitambi[emoji28][emoji28]..Mzee akasema mwone Yule dhambi za watu zimemwelemea kwenye tumboHadi anashindwa kuhema[emoji28][emoji28]
akaendelea Kusema kijana wangu ukimwona mtu ana kitambi ujue huo ni mzigo wa dhambi za watu MUNGU anamuadhibu.. kitambi kibaya sana mwanangu[emoji28][emoji28]

Kuanzia siku hiyo nilikuwa nikimwona Askari mwenye kitambi huwa nakumbuka hii kauli na kucheka Sana pekeyangu
 
Huku trafiki wengi huku vitambi vingi!
Taratibu mtanyooka tu!
NANI KAMA MAMA?
 
Back
Top Bottom