Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Aisee. Kwa hiyo na wewe uliamini na bado unaamini kabisa hiyo kauli ya baba yako kwamba ukimwona mtu ana kitambi ujue huo ni mzigo wa dhambi za watu na mwenye nacho anakuwa kaadhibiwa na Mungu?
Mzee ni mtu mwenye utani mwingi wenye ukweli ndani yake
 
Kweli kabisa haileti picha nzuri mpiginaji tunayekutegemea ukawe Frontline unaanzaje kuwa na kitambi?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji, Boma Kichakamiba mkoani Tanga amewataka askari wa uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni kuviondoa ili kuwa wakakamavu na wepesi zaidi katika kutimiza kazi zao.

"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia

Kwa uzoefu wako, ukiacha askari wa Uhamiaji waliosemwa na Rais Samia, ni Askari wa kikosi gani wanaongoza kwa vitambi hapa nchini?

Picha: Kwa hisani ya mtandao (Haihisuani na Habari)

View attachment 2324500

Picha ndiyo jibu.Jeshi la polisi wanafata.
 
Mambo mengine yapo kiusalama zaidi.

Wenyewe wanajua tusiwaingilie.
 
Aanzie huku
Wewe humtakii mema!
Lakini hata kama ingepaswa kuwa hivyo, hana uwezo wa kuanzia popote.

Wee ona hata hotuba zake zilivyokaa kimipashopasho tu; hakuna anayezichukulia kwa uzito wowote ule.

Hii mipasho yote aliyosema hapa, unadhani nani atahangaika na lolote alilosema. Shughuli imepita, na tunaendelea na mipasho mingine kama kawaida.

Hii miaka minne Tanzania itakuwa imepoteza bure kabisa.
 
Hao wasio na vitambi watuombe Vita vya kirafiki
Achana na hizi fikra. Tumwombe tu Mungu azidi kutupa amani na majirani zetu.

Kwa watu kama wewe, utani wa Simba na Yanga unauweka katika kila jambo.

Huu si wakati wa kujivunia lolote, hata kama tulijitambua na kujiamini huko tulikotoka.

Kumbuka, hayo unayojibaraguza nayo, hayawahusu hao unaoamini wanao uwezo peke yao. Uwezo wao unatokana na hali yetu sote kama nchi, na siyo wao peke yao.

Kwa hali ilivyo sasa hivi, mambo hayo ni kuyanyamazia tu na kubaki tukiomba kuwa hali yetu mbovu itabadilika kabla hatujalazimika kuwekwa majaribuni na hao majirani.
 
Back
Top Bottom