Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Hii ingefanywa kuwa Sheria kama ambavyo wanaelekezwa namna ya kunyoa pia hawa paswi kuwa na vitambi hata kwa bahati mbaya,

lingine ni hawa askari wa kike waambiwe lile ni jeshi sio maonyesho ya mitindo ya nywele, yani kuna mmoja nilimuona aliinama tuu kofia ikaanguka, kama wakiwa mafunzoni wote wanapigwa vipara kwa nini kwenye kazi wakiume wabanwe na maelekezo ya namna ya kunyoa alafu wao waachwe ?

Jeshi letu la polisi linapaswa kutazama upya muonekano wa askari wake
 
Ameongea ukweli mtupu mh Rais, Askari anatakiwa awe mkakamavu aliyejengeka vyema mwili, kutokanaa na kujiweka sawa na tayari muda wote, siyo Askari anakuwa anakitambi Hadi unaona anapata shida hata anapotembea, ,Askari lazima awe shapu kimwili na kiakili pia
 
Shida ni kipimio cha vitambi. Kuna watu wanavitambi vya urithi hata apigwe kwata vipi hakitoki.Kuna vitambi vya umri n.k Km kipimio ni macho pekee kuna watu wanaenda kuonewa.
 
Mama Samia mwenyewe ni oveweight inabidi apunguze mwili...
Embu acha uongo wako hapa, humuoni namna mh Rais wetu alivyo shapu na mwepesi, wewe unafikiri angekuwa na huo uzito uusemao hapa angeweza kufanya kazi ya Royal Tour na ikakamilika kwa ufanisi mkubwa ule, Kama unakitambi wewe nendaa kakitoee huko, hutaki acha kazi waingie vijana wazalendo na wachapa kazi
 
Unajua mwili wa binadamu haswa mtu mzima, tena wa bara hili la Afrika...tumezoea kuridhika..vitambi, huja tu na sio hao askari hata mtaani?? Hata wanawake wana matumbo ya uzazi yanawashinda kuyatoa..kwani yeye hana tumbo, alitoe kwanza lake..

Mimi sio askari, ila tuishi kwa mipaka kidogo.
Acha ujinga wewe
Askari hatakiw kuwa na kitambi
Huo ni uvivu wa kufanya mazoez na ulaji ovyooo ovyooo wa vyakula na bia

Wanakula kama wanahama dunian

Tena warudi mafunzoni na viboko juuu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mazaa ajielewi asimamie nn baada ya kutoa matamko ya maana anatoa matamko ambayo sio logic kabisa. Yeye mbona anakitambi.

..sio sahihi kuanza kumkosoa maumbile yake. Yule ni mama mtu mzima. Tukosoe hoja zake na utendaji wake.
 
Shida ni kipimio cha vitambi. Kuna watu wanavitambi vya urithi hata apigwe kwata vipi hakitoki.Kuna vitambi vya umri n.k
Wewe nenda ukatoe kitambi hayo utakwenda kuelezwa huko kuwa huo urithi wa kitambi uliupata ulipoajiliwa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya askari 818 wa Jeshi la Uhamiaji, Boma Kichakamiba mkoani Tanga amewataka askari wa uhamiaji ambao wana vitambi warudi chuoni kuviondoa ili kuwa wakakamavu na wepesi zaidi katika kutimiza kazi zao.

"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia

Kwa uzoefu wako, ukiacha askari wa Uhamiaji waliosemwa na Rais Samia, ni Askari wa kikosi gani wanaongoza kwa vitambi hapa nchini?

Picha: Kwa hisani ya mtandao (Haihisuani na Habari)

View attachment 2324500

Rais Samia mtumie Raila Odinga salam Za pole kuelekea 2025​

 
Sijaamini kama kapitisha hili agizo maana hakuna uthibitisho kutoka ofisini, hii ni moja tu ya ngonjera za viongozi wanafiki.

Kwanza hata yeye ana kitambi kwa nini asiwe mfano kwa hao aanze yeye kupunguza hicho kitambi?

Aache kuimba taarabu.
 
Sijaamini kama kapitisha hili agizo maana hakuna uthibitisho kutoka ofisini, hii ni moja tu ya ngonjera za viongozi wanafiki.

Kwanza hata yeye ana kitambi kwa nini asiwe mfano kwa hao aanze yeye kupunguza hicho kitambi?

Aache kuimba taarabu.
Pot toa kitambi hicho
Amesha sema kauli ya rais ni Sheria mzee hujui??

Tena mtakitoa na viboko juuu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Embu acha uongo wako hapa, humuoni namna mh Rais wetu alivyo shapu na mwepesi, wewe unafikiri angekuwa na huo uzito uusemao hapa angeweza kufanya kazi ya Royal Tour na ikakamilika kwa ufanisi mkubwa ule, Kama unakitambi wewe nendaa kakitoee huko, hutaki acha kazi waingie vijana wazalendo na wachapa kazi
Acha ujinga wewe, Mheshimiwa Rais ni obese
 
Back
Top Bottom