Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Rais Samia aagiza askari wenye vitambi kurejeshwa mafunzoni

Hii ingefanywa kuwa Sheria kama ambavyo wanaelekezwa namna ya kunyoa pia hawa paswi kuwa na vitambi hata kwa bahati mbaya,

lingine ni hawa askari wa kike waambiwe lile ni jeshi sio maonyesho ya mitindo ya nywele, yani kuna mmoja nilimuona aliinama tuu kofia ikaanguka, kama wakiwa mafunzoni wote wanapigwa vipara kwa nini kwenye kazi wakiume wabanwe na maelekezo ya namna ya kunyoa alafu wao waachwe ?

Jeshi letu la polisi linapaswa kutazama upya muonekano wa askari wake
Mbona reference unafanya kwa polisi tu?
Sema hilo suala litazamwe kwenye majeshi yote,kama ambavyo baadhi ya wachangiaji walivyochangia kuhusu vitambi.
 
Umesoma wapi hayo maneno ya "jeshi limekuwa dhaifu/Hali mbaya", kumbe hata hujui kusoma na kuelewa yaliyoandikwa?

Kiujumla ni kwamba, watu kama wewe ni washangiliaji tu wa kila jambo bila ya kuwa na uhakika mnachokishangilia au kusifu. Yale yale ya ushabiki wa Yanga na Simba.

Kiufupi, watu kama wewe ni mashabiki tu, hata mkijua mlisemalo hamna uhakika nalo.

Mbaya zaidi ni hapo mnapoweka ushabiki katika mambo yasiyohitaji ushabiki, kama unavyofanya hapa.
Kama humaanishi jeshi limekua dhaifu/Hali mbaya then mjadala ulikua wa nini!?
 
Supu ya vitu gani mkuu 'Erythro."! Ya makongoro?

Inategemea na kiasi cha mafuta yaliyomo kwenye supu yenyewe.
Nyama na mambo yake havijawahi kusababisha unene , shida kubwa iko kwenye Wanga
 
Kauli hii kabambe imetolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan huko Tanga, wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kwenye Chuo cha Boma Kichaka Miba Mkoani humo .

Mh Rais amesema kwamba ili kurejesha Ukakamavu kwa Askari wa Uhamiaji inapaswa wote wenye vitambi kurejeshwa kuhenya ili kupukutisha Vitambi na kurejesha Ukakamavu.

Chanzo: SwahilTimes

Toa Maoni yako
Kitambi kinakuja kutokana na mtindo wa maisha na hakitoki kwa kufanya kwata. Hata akifanyishwa 'Extra drill' maisha yote ya skari utatokea uasi............kupenda maisha ya fahari, kula vitu vitamu bila uwiano, kujipatia kipato bila kuitolea jasho halali na kupotoshwa na pesa zinazoingia mfukoni kila siku hivyo kuacha kufikiri kesho haina rangi sawia na ya leo ndio chanzo.

Hata hivyo mkuu wa kaya ajiandae na changamoto za chini kwa chini kutoka kwao hao the so called 'cops'

AINA KUU ZA TUMBO KUFURA

1. KITAMBI MVIRINGO – The tumbo hili limekaa kama herufi 'O' linapatikana kwa kula protini nyingi (kimito)

2. KITAMBI MCHUCHUMIO – tumbo la aina hii limekaa kama herufi 'D' na husababishwa na kula juisi nyingi na bia maalumu

3. KITAMBI MBONYEO – uvimbe wa tumbo huatamia kitovu kwa kiwango ambacho hufanya kisichoonekana. Hivi ndivyo mafisadi wanavyokuwa, lakini mtu huyo akisimamishwa kazi au kujihusisha na mazoezi ya muda mrefu ya kazi, huisha haraka sana.

4. KITAMBI MTEPETO – Uvimbe wa tumbo hauonekani kama nguo pana zinavaliwa, husababishwa na kula kupita kiasi

5. KITAMBI MFUMANIO - Huyu ni mtu ambaye hana pesa, lakini tatizo linatokana na minyoo na utapiamlo mkali

6. KITAMBI MTUNGUO – aina hii ya uvimbe wa tumbo ni maarufu kwa akina dada na wanawake; tumbo linakuwa na umbo la mayai linalosababishwa na chakula kisicho na uwiano.

Kwa kawaida mwili wa binadamu una seli za mafuta kati ya bilioni 50 na 200 zinazosambazwa katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.

Kwa wanawake, seli hizi zipo zaidi katika maeneo ya matiti, makalio, kiuno na nyonga.

Kwa upande wa wanaume, seli hizi hupatikana sana kifuani, tumboni, na nyonga pia.

Mafuta ya tumbo hujilimbikiza kwa njia kuu mbili:

i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii. Njia ya pili ni kutoka viungo vya ndani kama moyo, kongosho, n.k.

Uvimbe wa tumbo unaosababishwa na lishe ya chakula kisicho na uwiano lishe sawa

Chanzo kikuu cha unene kupita kiasi ni kukosekana kwa uwiano wa nishati (kalori) katika mwili wa binadamu, hali inayosababishwa na mtu kula vyakula vinavyotoa nguvu zaidi kuliko kile anachoweza kutumia na kuachia kama taka.

Vyakula vinavyochangia kuvimbiwa ni pamoja na :

i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe imechemshwa, kukaangwa, au kuchomwa), nyama nyeupe ya kuku (iwe ya kuchemshwa, kukaangwa, au kuchomwa), mafuta ya kupikia , (hasa yale yanayotokana na bidhaa za wanyama, kama vile siagi, na jibini ), viazi vya kukaanga (chips) na pizza.

ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile wanga wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.

iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyoongezwa

kama vile soda na keki.

iv. Vyakula vilivyotengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, vidakuzi, chapatti, pastries, mkate mweupe n.k.

v. Pamoja na vinywaji vinavyotengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na n.k.

Vyakula vilivyotajwa hapo juu, vikitumika bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia tatizo la kuvimbiwa.

vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo kwa muda mrefu ambavyo huongeza kasi ya kuweka mafuta karibu na tumbo au moyo unaoathiri hatari ya saratani au upanuzi wa moyo au ujenzi.

vii. Msongo wa mawazo

viii. Kuongea sana bila kipimo

Kitambi ni mafuta ambayo yanaweza kuwa chini ya ngozi yako au ndani kabisa kuzunguka moyo,, mapafu, maini na viungo vingine. Mafuta haya ya ndani (visceral fat) ndiyo yanayoweza kuwa tatizo kubwa kwa afya yako hata kama mwili wako ni mwembamba kiasi gani. Mwili huhitaji mafuta haya ndani kwa ajili ya kutenganisha viungo vya ndani ya mwili visigusane na kusuguana, lakini yakizidi huleta matatizo ya kiafya. Ukiwa na mafuta mengi yaliyopitiliza kipimo cha uhitaji utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya ‘Shinikizo la damu, Kisukari (Kisukari hatua ya 2), magonjwa ya moyo, kansa (utumbo na maziwa) na mengineyo.

Kuacha mwili kunenepeana na kuongeza uzito kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta ya ziada na mengine kuyachoma kuongeza joto hivyo kusababisha mwili kutafuta sehemu nyingine za kutunzia kama kuzunguka moyo ambapo ndipo matatizo yanapoanzia kukusumbua.

Kumbuka uzito wa mtu mwenye siha safi unatakiwa uwe sio zaidi ya nusu ya urefu wake wa kimo akiwa amesimama wima. Upana wa moyo wa mtu mwenye sifa njema unatakiwa usiwe zaidi ya kipimo cha kukunja ngumi mkono wake mwenyewe.
 
Vitambi ni tatizo kubwa kwa watu wengi wa mjini na pwani, wanawake kwa wanaume,.vijana wa makamo na wazee.
 
Hapo ndiyo umuhimu wa Sheria Je,ni sheria gani inayokataza mtu Kuwa na kitambi?

Hata ikitungwa Leo bado haitawahusu Wale ambao walikuwa na vitambi kabla ya kutungwa Kwa sheria.

Kwa upande mwingine inanifurahisha kwasababu Mimi sina Kitambi lakini Nina Shaka kama Hapo Haki za Binadamu zimezingatiwa hasa katika eneo Ubaguzi au ndiyo maana wote wanaungana ili kuwe na katiba Bora?
Jeshini hakuna kitu kinaitwa haki za binadamu. Askari anatakiw akuwa fit 24hrs..
Kitambi ni ishara ya kulegea mahali, uzrmbe fulani. Lazima wakumbushiwe
 
Hao wasirudishwe mafunzoni,wapewe vile vimbegu vya wamasai tu.Wataharisha mpk puru watakua wanairudisha kwa kidole.
 
Toa Maoni yako
1660770555636.png
 
"Nilikuwa naangalia gwaride, waliokuwa wakiongoza vikosi ni maafisa wazoefu, kati yao kuna wenye vitambi, nimeviona vitambi hapa. Nadhani hatutakiwi kuwa na maafisa wa vitambi, warudi tena hapa (Chuoni) waje watoe vitambi ili wawe wepesi zaidi kutimiza kazi zao." Ameeleza Rais Samia
1660770963234.png
 
Kauli hii kabambe imetolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan huko Tanga, wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kwenye Chuo cha Boma Kichaka Miba Mkoani humo .

Mh Rais amesema kwamba ili kurejesha Ukakamavu kwa Askari wa Uhamiaji inapaswa wote wenye vitambi kurejeshwa kuhenya ili kupukutisha Vitambi na kurejesha Ukakamavu.

Chanzo: SwahilTimes

Toa Maoni yako
Angeaza na mawaziri wenye vitambi then afuate wabunge wake na wakurugenzi kabla hajaenda kwa dc na rcs

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom