Kauli hii kabambe imetolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan huko Tanga, wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari wa Uhamiaji kwenye Chuo cha Boma Kichaka Miba Mkoani humo .
Mh Rais amesema kwamba ili kurejesha Ukakamavu kwa Askari wa Uhamiaji inapaswa wote wenye vitambi kurejeshwa kuhenya ili kupukutisha Vitambi na kurejesha Ukakamavu.
Chanzo: SwahilTimes
Toa Maoni yako
Kitambi ni matokeo ya ugonjwa unaoitwa insulin resistance.
Ni ugomjwa kama magonjwa mengine ya kibiolojia.Mazoezi hayautibu,ila yanaondoa kwa muda tu hali ya unene.
Ugonjwa huu unatibiwa kwa kuacha kula vyakula vya wanga na kupunguza stress huku mtu akifanya maziezi moderate.
Kudhania kwamba askari wenye vitambi matokeo ya uvivu ni makosa yanayoletwa na ignorance au ujinga.
Kitendo cha kutolewa amri hiyo ni kitendo cha unyanyapaa na hakistahili kushangiliwa.
Wengi kwa sababu ya chuki wanashangilia na wakiamini kuna uhusiano wa rushwa na kuwa na kitambi.Bahati mbaya hata wale wanaojiita wasomi wamo kwenye mkumbo huu.Ingawa hata askari wembamba wasio na vitambi wapo wengi tu wanaokula rushwa.
Dhambi hii ya ubaguzi haitaacha kuwatafuna.Siku hizi wapo wadada na akina mama wananenepa sana kwa sababu ya matatizo ya kutokuwepo uwiamo wa homoni na si uvivu na ulafi kama jamii inavyoaminishwa
Chakula cha protini ni gharama kubwa kwa wengi kukifanya chakula kikuu.Ndiyo maana wanalazimika kula tu wanga kwa wingi kuliko protini
Wananchi wenzangu acheni kudhihaki na kudhalilisha watu wenye vitambi.Wengi hawapendi kuwa hivyo.Ni ugonjwa.