Rais Samia aagiza kushushwa tozo kwenye bidhaa za mafuta

Rais Samia aagiza kushushwa tozo kwenye bidhaa za mafuta

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zinazoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Imeelezwa, Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini.


FA7ULdxWYAEoEC_.jpg


FA7ULdvXoAMmC8I.jpg

 
Tanzania mafuta yakipanda leo Duniani, bei inapanda siku hiyohiyo ila mafuta yakishuka bei huko Duniani Tanzania tutaambiwa kuna shehena ya zamani ilinunuliwa kwa bei ya zamani.

Unajiuliza mbona kwenye kupanda hatuambiwi kuna shehena ya zamani tusubiri iishe?

Magenge ya wauza mafuta wameweka pale mawakala wao huko ewura, tunaokamuliwa ni sisi choka mbaya.

Sheria za tozo si wamezipitiaha juzi kwenye bajeti kwa mbwembwe na kusema watanzania tumezikubali, leo wanasema waziondoe zitupunguzie ugumu wa maisha, hayo maisha magumu yumeyapata lini wakati juzi waliona kama tuna maisha mazuri wakaziweka?
 
Kutoa maelekezo ni jambo moja, na kutekeleza ni jambo la pili.

Alisha agiza kuacha kubambikia watu kesi je Siro kaacha? Alisha agiza wasio na makosa watolewe mahabusu je? /vitengo wamewaachia?

Aliagiza mikutano ya ndani isibughudhiwe. Majibu na vitendo vya Siro na watu wake wamefikia wapi? Alisema vifurushi virekebishwe hebu tumuulize Mwigulu huyu watakae gombea nae urais kwenye chama chake kama alitii amri ya Mh Rais? Maana nakumbuka alituambie tusio taka tozo tuhamie Burundi
 
Wamajitekenya wenyewe wanacheka wenyewe, jamani wekeni tosa ya asilimia tano au kumi kwa chochote kile,waTanzania wengi wataweza kulipa bila ya kuongopea, yaani hata wale wamachinga mamantirie wote watatoza kodi kwa mteja, kazi nyepesi tu lakini weziwetu wanatukamua kisha wanalegezea kisha wanazukia kwengine wanakamua.

VAT ni kitu simple sana ila hawa weziwetu wanatuchezesha foliti.
 
Wamajitekenya wenyewe wanacheka wenyewe ,jamani wekeni tosa ya asilimia tano au kumi kwa chochote kile,waTanzania wengi wataweza kulipa bila ya kuongopea,yaani hata wale wamachinga mamantirie wote watatoza kodi kwa mteja ,kazi nyepesi tu lakini weziwetu wanatukamua kisha wanalegezea kisha wanazukia kwengine wanakamua.

VAT ni kitu simple sana ila hawa weziwetu wanatuchezesha foliti.
Hao watu hawana maana! Maneno mengi!
 
Back
Top Bottom