Rais Samia aagiza kushushwa tozo kwenye bidhaa za mafuta

Rais Samia aagiza kushushwa tozo kwenye bidhaa za mafuta

Tengeneza tatizo

Unajifanya mjuzi wa kitatua

Unapigiwa makofi

Tanzania hii magu alikili kweli tumedhurumiwa vyakutosha
 
Si alipandisha juzi tu [emoji28][emoji28][emoji28]
Leo anataka asifiwe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na kuna wajinga wanatoa pongezi na kumsifia
Hujaelewa kuna tozo karibia 10 za ajabu ajabu kwenye kila lita moja ya mafuta inayoingia nchini,kitu ambacho kinasababisha mafuta hayo hayo kutoka bandarini kwetu Dar yakifika Zambia wao bado bei kwa lita ni chini ya 1800. Kuna tozo sijui EWURA, Bandarini, TRA, wakala wa vipimo, TBS na zingine kibao!! Hapa ilitakiwa zingine siyo kupunguza bali zifutwe kabisa na tungenunua petrol kwa 1500 kabisa hapa.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zinazoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Imeelezwa, Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini

View attachment 1963765

View attachment 1963769
Jambo jema.
Hivi ile habari ya aliyekuwa anavuta mafuta huko Kigamboni na kila kitu kiliwekwa wazi Polisi wetu wakatuambia wanafuatilia kwa karibu na wahusika kupelekwa mkono wa sheria! Hili liliishia wapi wakuu?

Tuamini nini kama sio mradi wa watu wenye jina hivyo mambo yameendelea kama kawaida?
Benki kuu tuliaminishwa pia kimya.
Wizara ya fedha wakajichotea wakapewa siku kadhaa kimya.
Tanzania yangu nzuri sana

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Aidha, Rais Samia pia ameagiza ufanyike mchakato wa haraka wa kupeleka marekebisho ya Sheria Bungeni zinazohitaji marekebisho ya haraka katika kukabiliana na kupanda kwa bei za mafuta hapa nchini, ili kumlinda mtanzania na gharama za maisha zinazotokana na kupanda kwa bei ya mafuta.
 
Wanatengeneza tatizo alafu baadae wanakuja kulitatua wenyewe ili tuwasifu wanatujari kumbe ni mbinu za uraghai tu
 
Washatuumiza wanaona sawa unapopandisha mafuta gharama za maisha zinaongezeka hata kwa vitu vya kawaida Tanzania sio Nchi ya kununua mafuta bei kubwa zaidi ya Zambia ambao tunawapelekea kwa Bomba na maroli tujitafakali kuna sehemu kuna tatizo kubwa sio dogo..
 
Hakuna jipya na hilo. Ukweli ni kwamba mafuta yatapanda bei/yameshapanda.
Naamini marekebisho ya sheria hayata mgusa mwananchi wa kawaida kama tunavyopenda.
Serikali kwa sasa ipo kweye mchakato wa kuongeza wigo la ukusanyaji wa kodi na hivyo basi,ongezeko la bei la mafuta lita kwaruzana na hiyo hatma. Hilo ndio korofi.
Ningependa kuona sheria hiyo ya marekebisho inaunganishwa pamoja na sheria ya mazingira na kutafuta mbinu za kupunguza utumiaji wa mafuta ya petroli na kwenda kwenye gesi. Ikiwezekana malori yote ya mizigo yawe yanatumia gesi asilia kufikia 2025 na sio 2050,
Malori yote ya mizigo mizito yatakayoagizwa yawe na injini hizo. Bila kutafuta njia zingine, hakika, tutakua tuna kurupuka kila bei hizi za mafuta zikipanda na kukimbila marekebisho ya sheria tu.
Tupo pamoja.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zinazoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Imeelezwa, Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini.

Tanzania mamlaka zake hazina uwezo wa kubuni vichocheo vya uchumi wanachojua in tozo tu
 
A great move if seriously and positively implemented.
Similar initiatives should be taken towards investments and moves aiming at reducing and curbing the Costs of Electricity.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zinazoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Imeelezwa, Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini.

Naona Mh Waziri kaamua kujilipua kivyakevyake....na kwa vile ni "Good Communicator" basi atakuwa anawaacha wenzake mbali Kabisa kujenga na kutetea hoja.....

Yakifanikiwa tutashukuru WATZ.
 
Si alipandisha juzi tu [emoji28][emoji28][emoji28]
Leo anataka asifiwe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na kuna wajinga wanatoa pongezi na kumsifia
Wajinga mnaopinga kila kitu anachofanya Rais SSH mupo na mojawapo ni wewe Usher-smith MD. Wewe hata Serikali ikitaja jinsia yako utaibishia tu alimradi umebisha.
 
Si alipandisha juzi tu [emoji28][emoji28][emoji28]
Leo anataka asifiwe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na kuna wajinga wanatoa pongezi na kumsifia
Ni Kama mabeberu tu unatengeneza Ebola halafu unatengeza chanjo.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zinazoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Imeelezwa, Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini.

Kuumia kote huku tulikuwa tunasubiri asimame jukwaani, mbona angeweza kuandika kimemo tu akawapa
 
Hawa jamaa hawa..
Yani km wanataka kupandisha bei ya mafuta toka 2300 to 2700.. wanachokifanya wanapandisha mpaka 3000 .... Halafu anakuja Chifu wa maChifu anajifanya kupnguza mpaka 2700 (ile waliyoilenga)

Wananchi wanashangilia.. Usanii mtupuu
C unakumbuka ishu ya tozo walivyoicheza kisanii sasahv kimyaaaa baada ya kupunguza 30%
 
Back
Top Bottom