Rais Samia aagiza waliokuwa wanaishi Bonde la Mto Msimbazi kinyume na sheria kulipwa Tsh. Milioni 4 kila mmoja

Rais Samia aagiza waliokuwa wanaishi Bonde la Mto Msimbazi kinyume na sheria kulipwa Tsh. Milioni 4 kila mmoja

Hiyo nne mbona ni nyingi tu, hiyo no zawadi wamepewa na mama mwenye huruma kwa kuishi bondeni kinyume cha sheria.
Dar Haina bondeni, its a matter of drainage system basi......wakazi wa karibu na mto Sinza watanielewa.

Hapa Mama atakuwa ameshauriwa na mafisi madhulumati, wawaondoe wanyonge bila fidia kisha wagawe maeneo upya.

Kumbuka mradi wa DMDP una mpango wa flood control Kwa mto Msimbazi, kuujengea mto na kujenga mabwawa ya kupunguza speed ya maji, baada ya hapo mafuriko yatakuwa historia.

Mama asikubali machozi ya wanyonge yamuelekee yeye kisa mafisi wachache, milioni 4 ni pesa gani?
 
Ni vizuri,ila Ingependeza kama wangeamriwa kuhama kwa lazima .
Uko sahihi kabisa,hawa watu miaka nenda rudi wako hapo licha ya serikali kuwashauri kuhama,kila mwaka yakitokea mafuriko wanaathirika na msimu wa mvua ukipita wanarudi tena kuishi. Kuwapa hela na kuwaambia wahame kwa hiari ni sawa na kutupa tu hizo fedha kwani watazipokea na hawatahama.
 
Kiwanja Dar ni shs ngapi? yeye akipewa 4M anaweza kujenga nyumba ya kuishi na kununu kiwanja Dar? wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi? ni kutafuta sifa za hovyo bila sababu za msingi.
Walishawahi pewa hadi viwanja mabwepande na mifuko ya simenti bure waliuza viwanja hadi simenti

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kipindi hicho Yusuf Makamba akaenda kubomoa vijumba vya wasambaa wenzie pale jangwani na akashika bomoleo mwenyewe akaanza kubomoa kwa mikono yake wakamloga aliumwa karibu afe Akawacha

Wale hawataki kuhama jangwani wanasema karibu na mjini utafiiiri wao ndio wamiliki wa jiji la Dar wakizidiwa mafuriko serikali ikituma uokozi wanakubali maji yakikata wanarudi serikali ikisema kukitokea janga tena hatuji kuwasaidia wanasema kwani tuliwaomba mje kutusaidia? Tuacheni msije kukitokea tena

Wale watu ni shida
 
Mama anaupiga Mwingi, hongera kwake Kwa roho ya ubinadamu alioionyesha, walipaswa kuhamishwa Kwa lazima bila kupewa chochote na kufunguliwa mashtaka maana walishaonywa ujenzi wa mabondeni ni Hatari. Kisheria kuhatarisha Usalama wako na wa raia wengine Kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai..
Baada ya Hatua hii Hilo eneo libaki wazi ama wapewe wakulima wa Mboga mboga na matunda wafanye Yao.
 
Washauri wake ni hopeless, alipaswa awaambie JKT/NHC wawaajengee nyumba za bei nafuu na wakopeshwe kwa riba ndogo kwa muda hata wa miaka 10 tena kiangazi.
Africa hii hii au nyingine mkuu!hapo ukoo wa kina marope ndio utakaojiandikisha majina mengi hata walengwa wenyewe huo msaada usiwafikie,ebu ulizia ilivyokua pale machinga complex kama hata kuna machinga aliewahi kupata frem
 
Mama anaupiga Mwingi, hongera kwake Kwa roho ya ubinadamu alioionyesha, walipaswa kuhamishwa Kwa lazima bila kupewa chochote na kufunguliwa mashtaka maana walishaonywa ujenzi wa mabondeni ni Hatari. Kisheria kuhatarisha Usalama wako na wa raia wengine Kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai..
Baada ya Hatua hii Hilo eneo libaki wazi ama wapewe wakulima wa Mboga mboga na matunda wafanye Yao.
Wamuulize Yusuf Makamba akiwa mkuu wa mkoa wa Dar essalaam na uzoefu wake kipindi chake kuhamisha hao watu

Ana kitu ambacho hawezi sahau aweza sahau yote lakini sio hao wakazi wa jangwani
 
wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi?

Makosa haya ya wengine ndio yamemfanya aingiwe na huruma na kuamuru hivyo, maana asingefanya hivyo bado swali lako hili lipo palepale. Kwahiyo wasirudi tena, watafute pa kwenda.
Zoezi hilo likishamalizika, DC, RC, na timu nzima inayodili na usalama wa watu na mazingila ikizembea kwa kuwaacha raia kuendelea kuishi humo, wasilaumu mtu kitachowakuta.
 
Kiwanja Dar ni shs ngapi? yeye akipewa 4M anaweza kujenga nyumba ya kuishi na kununu kiwanja Dar? wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi? ni kutafuta sifa za hovyo bila sababu za msingi.
Jamaa Hamas wanakuchanganya au?
Hao walikuwa wanaishi hapo kimakosa ,yaani walitakiwa watolewe baru bila hata Mia!! Sasa wamepewa zawadi ya milioni 4 wasepe bado unaona haitoshi!!
Kuwaongoza watanganyika Bora upewe kundi la mbuzi uwachunge
 
Walishawahi pewa hadi viwanja mabwepande na mifuko ya simenti bure waliuza viwanja hadi simenti

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kipindi hicho Yusuf Makamba akaenda kubomoa vijumba vya wasambaa wenzie pale jangwani na akashika bomoleo mwenyewe akaanza kubomoa kwa mikono yake wakamloga aliumwa karibu afe Akawacha

Wale hawataki kuhama jangwani wanasema karibu na mjini utafiiiri wao ndio wamiliki wa jiji la Dar wakizidiwa mafuriko serikali ikituma uokozi wanakubali maji yakikata wanarudi serikali ikisema kukitokea janga tena hatuji kuwasaidia wanasema kwani tuliwaomba mje kutusaidia? Tuacheni msije kukitokea tena

Wale watu ni shida
wahihama inatakiwa pavunjwe na wajengewe nyumba za bei nafuu kwa mkopo wa riba nafuu
 
24 November 2022
Mradi wa Bonde la Msimbazi Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania

Humphrey Kanyenye mratibu wa miradi ya benki ya dunia - TAMISEMI akifafanua kuhusu mradi wa Bonde la Msimbazi. Mkopo umesaini 17 November 2022 ukiwa na masharti, vigezo, kanuni na makubaliano, baina ya wafadhili na serikali ya Tanzania.

View: https://m.youtube.com/watch?v=FA9v1qOKiwc

New Jangwani Bridge jijini Dar es Salaam Tanzania kuwa na urefu wa mita 390 na ujenzi unatazamiwa kunaanza January 2023.

Eneo hilo la bonde la Msimbazi jijini Dar es Salaam hadi Pugu lina kaya 3800 zenye watu 11,000 ambao watafidiwa kwa mujibu wa sheria na pia kama masharti, vigezo na kanuni zilizokubaliwa na World Bank -( Benki ya Dunia) anasema afisa mratibu wa miradi ya benki ya dunia wizara ya TAMISEMI Bw. Humphrey Kanyenye
 
Kiwanja Dar ni shs ngapi? yeye akipewa 4M anaweza kujenga nyumba ya kuishi na kununu kiwanja Dar? wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi? ni kutafuta sifa za hovyo bila sababu za msingi.
of course, it's a Joke, Kibaya zaidi wamemvuta mpunga wa WB alafu wamewaambia WB Pale hakuna Raia wanamiliki hapo kwahiyo hamna fidia, Kikwete alipeleka watu mabwepande wakauza wakarudi tena hapo hapo
 
Kwanza kulikuwa hakuna haja ya kuwalipa. Ila KWA huruma ya Mh Rais (Madame president) milioni 4 ni kuwafanyia uungwana kwasababu maeneo waliyojenga ni hatarishi Kwa usalama wa makazi na afya zao, Wala sio eneo la serikali kusema serikali wana project na hilo eneo JIBU ni hapana .

Hivo ni heri wahame kwa hiari yao
 
Back
Top Bottom