Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Mbona mafisadi wamechota mabilioni ambayo hawakuyatolea jasho na wamesamehewa.

Vyeti feki walipwe walivuja jasho kulitumikia taifa hili. Pengine jasho walilovuja ndio hilo mafisadi wamelila.

Hata hivyo pesa watakayolipwa vyeti feki hafikii ile ya ufisadi escrow 230bilioni
Mafisadi gani wamesamehewa?
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Mkuu, mamlaka zilizotakiwa kuwahakiki ndizo zimefanya makosa.

Ukishamkubali mtu, ukakubali kazi anayokufanyia, ukampa mshahara, ukamkata mshahara kwenye mafao, unatakowa umlipe ukimuachisha kazi.

Kama.m vyeti vyake feki unatakiwa usimuajiri in the first place.

Zoezi zima halikuwa kuhusu vyeti feki, lilikuwa kuhusu kupunguza wafanyakazi kibabe bila kuwalipa malipo stahiki yao.
 
Maana yake ameruhusu wanafunzi wajitwalie vyeti feki
 
Mmerithi uSadist kutoka kwa mungu wenu mfu wa chato
Wahalifu ni marafiki wa awamu ile.

Mashehe wa Uamsho nje.

Mwenyekiti gaidi nje.

Wazee wa Escrow account nje.

Wauza madawa maarufu nje.

Maskini wamachinga hawatakiwi hata kuonekana.

Hivyo sishangazwi hata na hii hatua ya kulioa wale waliopaswa kuwa jela kwa kufoji credentials ili waajiriwe.

Mtu kaidanganya mamlaka ili aajiriwe halafu anadai malipo yatokanayo na kazi aliyopata kwa njia za udanganyifu??

Tunatengeneza mazingira ya kulea uhalifu na itakuja kutugharimu pakubwa.
 
Mkuu, mamlaka zilizotakiwa kuwahakiki ndizo zimefanya makosa.

Ukishamkubali mtu, ukakubali kazi anayokufanyia, ukampa mshahara, ukamkata mshahara kwenye mafao, unatakowa umlipe ukimuachisha kazi.

Kama.m vyeti vyake feki unatakiwa usimuajiri in the first place.

Zoezi zima halikuwa kuhusu vyeti feki, lilikuwa kuhusu kupunguza wafanyakazi kibabe bila kuwalipa malipo stahiki yao.
Ni kama mtu anavyoweza kwenda dukani na hela feki na mwenye duka asimgundue, huwezi kumlaumu victim
 
Ameagiza walipwe 5% walizokatwa. Zile 5% na kwa wale waliobakiza mwaka mmoja kustaafu serikali itakaa iangalie gharama ione itafanya nini.
Afadhali umefafanua maana washaanza kutunga ya kwao
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Aliyewaruhusu waingie kazini ni nani? Ameshughulikiwa?
 
Mbona mafisadi hayafungwi
Mimi naona katika hoja nyingi humu,hii yako ndiyo hoja nzito zaidi,
Yani unamaanisha kuwa kwa kuwa jamii karibia yote ishakuwa corrupt,mabilioni ya umma yanaporwa na hakuna kinachofanyika,basi na Hawa (hata Kama hawakuingia kazini kihalali) wapewe tu malipo maana hayo ndiyo yashakuwa maisha yetu
Yani unamaanisha zaidi kuwa "hauna haja ya kuwa mtu mwema peke yako katikati ya jamii iliyokengeuka"
Hizi hoja zingine wanazosema et "Hata Kama wana vyeti feki lakini walifanya kazi na kulitumikia Taifa" kwangu Mimi naona ni hoja za kilaghai tu
 
Punguza porojo Mkuu,kughushi nyaraka za Jamhuri ni kosa la jinai.Hawa kwa Magufuli aliwasamee,walipaswa kushitakiwa na kufungwa.Kama walikuwa na haki mbona hawakuishitaki serikali?
 
Atakuja Rais mwingine baada ya huyu utasikia, Kuna watu walikuwa na vyeti feki,wakalipwa fedha za serikali wakaziita 5%,wazitapike kupitia matundu yoteee
 
Umefoji vyeti. Umetumia laghai kazini na kwenye biashara. Hujafungwa. Bado wataka kulipwa?! Au walipwe?!
Bongo kweli banana republic…
 
Mimi naona katika hoja nyingi humu,hii yako ndiyo hoja nzito zaidi,
Yani unamaanisha kuwa kwa kuwa jamii karibia yote ishakuwa corrupt,mabilioni ya umma yanaporwa na hakuna kinachofanyika,basi na Hawa (hata Kama hawakuingia kazini kihalali) wapewe tu malipo maana hayo ndiyo yashakuwa maisha yetu
Yani unamaanisha zaidi kuwa "hauna haja ya kuwa mtu mwema peke yako katikati ya jamii iliyokengeuka"
Hizi hoja zingine wanazosema et "Hata Kama wana vyeti feki lakini walifanya kazi na kulitumikia Taifa" kwangu Mimi naona ni hoja za kilaghai tu
Mbona majeshini awakufukuzwa na Kazi wanafanya si dabo standard hii
 
Mkuu; Swali lako hapo mwisho kama likizingatiwa kwa mujibu wa maneno yako ni HATARI kweli-kweli. Kama HAKI itazingatiwa basi ni vizuri waanze na waliowaajiri au tuseme wale walioridhika na Documents zao na kuwaingiza kazini. i.e. Waziri/Katibu mkuu/DED e.tc. wote wawajibishwe kwa pamoja wao na walioingia kazini.
Ni haki yao walipwe makato yao yaliyopelekwa kwenye mifuko ya Jamii, na kwa wale waliotumikia zaidi ya miaka 15 walipwe mafao ya kustaafu- Hii ni kwa Mujibu wa Taratibu za ki-Utumishi Serikalini.
Lakini yote kwa yote Mkuu; Ingefaa uzingatie kwamba ufanyaji / utendaji wa Serikali (sio Tz. tu, bali serikali au Taasisi zingine) mambo yote na maagizo yote ya ki-Serikali ni kwa Maandishi na ni kutoka kwa Mtu au Ofisi yenye Dhamana hiyo. Huku jukwaani tunalumbana tu. Ukiona limetoka Tangazo/Agizo Rasmi ujue ndo imepitishwa. Raisi kuzungumza katika Hotuba (Kama ni kweli) haijawa Agizo. Je, Mh. Raisi wa JMT alisema "Naagiza....."?? Endapo hakusema hivyo, basi Tusubiri kwanza kwani hujapewa hiyo kazi ya kutoa Tangazo.
Rais akitamka kitu hata kama ni mkutanoni uelewe hilo tayari ni agizo ! Vinginevyo labda aamue tena kutengua agizo lake yeye mwenyewe !! Ameshasema walipwe maana yake watalipwa tu !! Lini ndio haijulikani !!
 
Back
Top Bottom