Rais Samia aagiza Waziri wa Biashara kudhibiti Wageni kufanya biashara za Machinga, ahoji vijana wetu watafanya kazi gani?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia, amesema haiwezekani wageni kuingia nchini na kufanya biashara za machinga, huku akieleza kuwa vijana wetu (Kitanzania) watafanya nini? na kuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo kuhakikisha suala hilo linasimamiwa ipasavyo ili kulinda fursa za ajira kwa wananchi wa ndani.

Your browser is not able to display this video.
Pia, Soma: Samia: Msiruhusu Wageni Kufanya Biashara za Wenyeji
 
Hii inawahusu wachina moja kwa moja maana washaanza hadi kufanya kazi za vinyozi, gareji, mama ntilie na bodaboda
Mkuu wachina wameshapewa nchi hii kama nchina anaweza kumiliki mgodi kwa shilingi laki tano kwanini Raisi ana shangaa Mchina kufungua kibanda cha MIX by yash
 
Zama za kutoa maagizo zimeikwisha.
Ni zama za utendaji na matokeo.

Hapo, inatakiwa itolewe ripoti kwamba kwa mwaka 2023-2024 Wizara imewarudisha wachina machinga labda 2000.
 
Siku zote alikuwa hawaoni?
 
Sikuelewa kama hii kazi ya wamachinga iko reserved kwa ajili ya sisi wazawa. Aibu sana
 
Ana waagiza au anasaoma risala aliyoandikiwa na mwandishi akakumbuka kuwa tuko kipindi cha uchaguzi aanze kuzungumzia suala la ukosefu wa ajira wageni waondolewe.
Tofautisha neno AMESEMA na AMESOMA. hapo amesoma hajasema mkuu
 
Sikuelewa kama hii kazi ya wamachinga iko reserved kwa ajili ya sisi wazawa. Aibu sana
Sio machinga tu. Kila taifa lina utaratibu wake kwenye fursa zinazopatikana inchini mwake na kipaumbele huwa ni kwa wazawa ,so sio sawa mchina au msomal au mnaijeria kuwa na duka kariako , wanapaswa wawekeze kwa ukubwa na teknolojia ambayo hatuna si kuuza viatu na protector,, mitaji ya kufanya hivo wazawa wanayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…