Lazima tuelewe kutaja ongezeko la mishahara ya watu hadharani ni kuchochea mfumuko wa bei nchini,Sasa tukachape kazi kwa bidii,
01 May 2022
Nairobi, Kenya
Mshahara Wa Chini Kabisa Sekta Ya Umma Waongezwa Kwa Asilimia 12
NA SAMMY WAWERU
SERIKALI imetangaza Jumapili nyongeza ya asilimia 12 kwa wanaolipwa mshahara wa chini kabisa katika sekta ya umma.
Tangazo hilo limetolewa na Rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Nyayo, Nairobi wakati wa sherehe za Leba Dei, Mei 1, 2022.
Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta amesema serikali yake inaelewa changamoto ambazo wafanyakazi wanapitia hususan kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.
βHayo yanatushawishi kutathmini kiwango cha mshahara wa chini kwa nyongeza ya asilimia 12, kuanzia Mei 1, 2022, yaani leo,β kiongozi wa nchi akatangaza.
Mabadiliko hayo ya malipo hata hivyo yatatekelezwa kwa wafanyakazi walio katika sekta ya umma pekee, walioajiriwa na serikali.
Nyongeza hiyo inaashiria, mfano, anayelipwa mshahara wa Sh50, 000 kwa mwezi, atapata nyongeza ya Sh6, 000.
Hii ina maana kuwa atapata jumla ya Sh56, 000, kabla kuondolewa kwa ushuru wa PAYE, malipo ya mafao ya uzeeni (NSSF), bima ya afya (NHIF) na
makato mengine ya serikali.
Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini (Cotu) ni Francis Atwoli.
Tangu janga la corona lilipotua nchini Machi 2020, gharama ya maisha imeendelea kupanda, bidhaa muhimu za kimsingi kama vile vyakula vikiandikisha mfumko wa bei.
Mafuta ya petroli yamepanda mara dufu, licha ya mzigo mzito unaozidi kulemea mlipa ushuru.
Kufuatia tangazao la Rais, wachangiaji wa mitandao walielekeza hisia mseto kwenye majukwaa ya mitandao.
βKwa nini nyongeza hiyo iwafae wafanyakazi wa umma pekee?β Peter Wangodi akaandika katika Faceebok.
Naye Dave Idewa, kupitia mchango wake ametaka kujua wasio na ajira watafaidi vipi?
βNa kwa Wakenya wengi wasio na ajira Mtukufu Rais?β Idewa akasaili.
βPesa za kupunguza gharama ya mafuta ya petroli na mbolea zilitoka kwanza? Tufahamishwe,β Silver Kipchumba akahoji.
Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta hata hivyo alisifia hatua ambazo serikali ilichukua 2020 na 2021 kuondoa na kupunguza ada na ushuru (VAT) kwa baadhi ya bidhaa muhimu za kimsingi.
βKwa ground, nyongeza iliyotangazwa nina uhakika haitatekelezwa,β
Oscar Ozil Njeru akaandika katika Twitter, naye Okoth wuod Okech akiuliza βWenye hatuna kazi faida ni gani?β
βHongera Rais wangu,β @Chizanodo msafiri akapongeza Rais Kenyatta.
@OtienoFelixOtienoz vilevile amesifia nyongeza hiyo