Rais Samia aahidi kupandisha mishahara watumishi wa serikali

View attachment 2207381
===
Rais Samia Suluhu Hassan leo tarehe 01|05|2022 ambayo ni siku ya "Mei Mosi "

Rais wetu ametangaza neema kwa wafanyakazi wa Serikali anayoiongoza,

Mtakumbuka ni miaka sita sasa Wafanyakazi wa Serikali ya Tanzania hawakupandishwa mishahara significantly,

Tunakumbuka, Rais Samia alipokuwa Jijini Mbeya katika Mei Mosi yake ya kwanza ya 01|05|2021

Rais Samia aliwaahidi Wafanyakazi angewaongeza mishahara mwaka huu wa 2022,

Hatimaye Rais huyu anayetajwa kuwa msikivu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania ameongeza mishahara kwa kiwango kitakachotolewa hapo baadae

Mtakumbuka TUCTA walipendekeza kuwa kima cha chini kiwe TZS 1,010,000,

Hongera Rais Samia, Hongera Wafanyakazi, Hongera Tanzania,Hongera CCM,

Alichosema Rais Samia;
===

“Lile jambo letu lipo. Ndugu zangu jambo letu lipo ila sio kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwa sababu mnajua hali ya uchumi wa nchi yetu na hali ya uchumi wa dunia. Hali si nzuri sana uchumi wetu ulishuka chini mno. "

"Tumejitahidi sana na kwa sababu nilishatoa ahadi mwaka jana, kwa hiyo nimeagiza jambo liwepo, mahesabu yanaendelea, tutajua lipo kwa kiasi gani. Lakini jambo lipo”
===

Lazima tuelewe kutaja ongezeko la mishahara ya watu hadharani ni kuchochea mfumuko wa bei nchini,Sasa tukachape kazi kwa bidii,
Toka mwaka jana alikua hajakamilisha utafiti mpaka sasa?
Nimeona raisi wa kenya kaongeza 12% ya kiwango cha chini ila wa kwetu bado anafanya utafiti.
Alafu kuna watu wanashangilia kama hazimo.

Je amewambia utafiti utakamilika lini?

Na kam kwenye mshahala wako wakiongeza asilimia 12 kama kenya unadhani utapata sh ngapi kama mshahara wako ni wa chini ni laki tatu?

Je kiwango hicho kitakusaidia kwa mfumuko wa bei uliopo kama kipande cha sabuni cha mia moja leo kinauzwa 700?
 
Watu Wa Pwani Wametushinda Tabia
Kusema Lile Jambo Letu Lipo Ndiyo Nini
 
Mama huyu ni msikivu sana, Hongera wafanyakazi wa Tanzania

Uhuru Kenyatta sio msikivu lakini Kapandisha mshahara maradufu hadharani. Nyie bakini na mbwembwe za kijinga.
 
Mimi nashangaa sana tunahangaika kuzungumzia mishahara ya watumishi serikalini halafu tunasahau kuwa wafanyqkazi wengi wapo sekta binafsi na serikali haizungumzii kabisa kubadili kima cha chini cha mshahara cha kisheria ili kulazimisha waajiri kuongeza mishahara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
01 May 2022
Nairobi, Kenya

Mshahara wa chini kabisa sekta ya umma waongezwa kwa asilimia 12

Mshahara Wa Chini Kabisa Sekta Ya Umma Waongezwa Kwa Asilimia 12​

NA SAMMY WAWERU

SERIKALI imetangaza Jumapili nyongeza ya asilimia 12 kwa wanaolipwa mshahara wa chini kabisa katika sekta ya umma.

Tangazo hilo limetolewa na Rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Nyayo, Nairobi wakati wa sherehe za Leba Dei, Mei 1, 2022.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta amesema serikali yake inaelewa changamoto ambazo wafanyakazi wanapitia hususan kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

“Hayo yanatushawishi kutathmini kiwango cha mshahara wa chini kwa nyongeza ya asilimia 12, kuanzia Mei 1, 2022, yaani leo,” kiongozi wa nchi akatangaza.

Mabadiliko hayo ya malipo hata hivyo yatatekelezwa kwa wafanyakazi walio katika sekta ya umma pekee, walioajiriwa na serikali.

Nyongeza hiyo inaashiria, mfano, anayelipwa mshahara wa Sh50, 000 kwa mwezi, atapata nyongeza ya Sh6, 000.

Hii ina maana kuwa atapata jumla ya Sh56, 000, kabla kuondolewa kwa ushuru wa PAYE, malipo ya mafao ya uzeeni (NSSF), bima ya afya (NHIF) na makato mengine ya serikali.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini (Cotu) ni Francis Atwoli.

Tangu janga la corona lilipotua nchini Machi 2020, gharama ya maisha imeendelea kupanda, bidhaa muhimu za kimsingi kama vile vyakula vikiandikisha mfumko wa bei.

Mafuta ya petroli yamepanda mara dufu, licha ya mzigo mzito unaozidi kulemea mlipa ushuru.

Kufuatia tangazao la Rais, wachangiaji wa mitandao walielekeza hisia mseto kwenye majukwaa ya mitandao.

“Kwa nini nyongeza hiyo iwafae wafanyakazi wa umma pekee?” Peter Wangodi akaandika katika Faceebok.

Naye Dave Idewa, kupitia mchango wake ametaka kujua wasio na ajira watafaidi vipi?

“Na kwa Wakenya wengi wasio na ajira Mtukufu Rais?” Idewa akasaili.

“Pesa za kupunguza gharama ya mafuta ya petroli na mbolea zilitoka kwanza? Tufahamishwe,” Silver Kipchumba akahoji.

Kwenye hotuba yake kwa taifa, Rais Kenyatta hata hivyo alisifia hatua ambazo serikali ilichukua 2020 na 2021 kuondoa na kupunguza ada na ushuru (VAT) kwa baadhi ya bidhaa muhimu za kimsingi.

“Kwa ground, nyongeza iliyotangazwa nina uhakika haitatekelezwa,” Oscar Ozil Njeru akaandika katika Twitter, naye Okoth wuod Okech akiuliza “Wenye hatuna kazi faida ni gani?”

“Hongera Rais wangu,” @Chizanodo msafiri akapongeza Rais Kenyatta.

@OtienoFelixOtienoz vilevile amesifia nyongeza hiyo
 
Back
Top Bottom