Rais Samia acha kumbeba Waziri wa Maji Jumaa Aweso. Hakuna cha maana kinachofanyika nchi hii

Rais Samia acha kumbeba Waziri wa Maji Jumaa Aweso. Hakuna cha maana kinachofanyika nchi hii

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Huyu Waziri, anajionesha sana kwenye vyombo vya habari na kila anapopewa mic., lazima ataje jina la Samia Suluhu Hassan kama kibwagizo cha shairi.

Tunachotaka ni matokeo chanya na kukataa wizi kwenye miradi ya maji ktk nchi hii. Huu ni msimu wa mvua baada ya ukame mrefu.

Kipindi cha ukame maji ilikuwa taabu kwa kisingizio cha ukame. Eti hata Mwanza wanasumbuliwa na ukame. Mjini wa Bukoba na Musoma huko ndo usiseme kabisa! Miji ya Morogoro na wilaya zake wao walishakomaza miili kutokuwa na maji.

Naelekea Mikoa ya kusini sasa. Nimepita Morogoro tena. Bwawa limejaa maji, yanfurika. Hata hivyo mabomba hayana maji kama zile enzi za ukame! What a hell is this ministry? Hapo Moro ndo makao makuu ya bonde la wami Ruvu, limalotawala mikoa ya Dar, Pwani na moro yenyewe.

Kinachosikika ni kwamba pesa nyingi ya wizara iko bonde hili na hapa ndo inapigwa kwa ushirikiano. Huu ni mkoa ambao waziri amekuwa akionekana hata mida ya usiku ili kupiga dili zake.

Tuondolee waziri huyu. Kama bunge limeishiwa, kopa serikalini, jamani!
 
Jamaa sijui huwa ana bahati ya NGEKEWA!!ukiangalia hakuna kitu cha maana alichokifanya kwenye wizara hiyo lakini, waliomteua wana muamini sana!!toka enzi za jiwe!!!
 
Huyu Waziri, anajionesha sana kwenye vyombo vya habari na kila anapopewa mic., lazima ataje jina la Samia Suluhu Hassan kama kibwagizo cha shairi......
Anapost Instagram kupita maelezo.

Ukiangalia clip zake unamuona ni mpambanaji kumbe hamna kitu
 
Aliposikia kwamba Wilaya ya Newala mkoa wa Mtwara dumu la Maji limefikia kuuzwa shilingi 2000 alikwenda kupiga mkwara na makashikashi mengi halafu baadaye akawaambia shida hiyo ya Maji kwa sasa anaiondoa lakini jamaa wanadi hakuna cha maana shida bado ipo.

Huyu hakuna cha maana anafanya kwenye Idara hiyo yaani.
 
Kama hakuna kitu Kinafanyika,Kwa hiyo haya hapa unafanya wewe na baba yako sio? 👇

Screenshot_20220207-161158.png


Screenshot_20220206-203437.png


Screenshot_20220206-182131.png


Screenshot_20220203-155715.png


Screenshot_20220202-212405.png


Screenshot_20220129-231540.png


Screenshot_20220129-231604.png


Screenshot_20220129-231423.png


Screenshot_20220129-231247.png


Screenshot_20220118-132731.png
 
Huyu Waziri, anajionesha sana kwenye vyombo vya habari na kila anapopewa mic., lazima ataje jina la Samia Suluhu Hassan kama kibwagizo cha shairi....
Kuna mtu mmoja alisema kibwana Aweso huwa kinapelekewa hela kwenye mabegi! Yaani kifisadi balaa! Kinaongea uzalendo kinatenda madudu!
 
Hapa Bongo ni kawaida mchapa Kazi kuchukiwa si anawanyima ulaji na kuwabana,katimua mainjia wa kutosha ulitaka wapige vigelegele ? Ndio nyie mnamchafua humu ila hakuna mwenye ushahidi.
Wewe Awesome ulizia wafanyakazi wizara ya maji utajua hujui! Dogo fisadi balaa! Sema mama sio rahisi kusikia kilio maana dini ndo inambeba si unaona anaowatoa mama wote ni wakristo!
 
Wewe Awesome ulizia wafanyakazi wizara ya maji utajua hujui! Dogo fisadi balaa! Sema mama sio rahisi kusikia kilio maana dini ndo inambeba si unaona anaowatoa mama wote ni wakristo!
Kama fisadi kwani vyombo havipo? Afu wanaopeleka pesa ni hao hao wafanyakazi na wakandarasi kujipendekeza,huu utaratibu unafanyika Tanroads,Tarura na kokote kwenye tenda..

By the way ndio wateule wa Jiwe hao.
 
Kuna mtu mmoja alisema kibwana Aweso huwa kinapelekewa hela kwenye mabegi! Yaani kifisadi balaa! Kinaongea uzalendo kinatenda madudu!
Acheni chuki zenu kenge nyinyi, Aweso anajitaidi Sana sana
 
Huyu Waziri, anajionesha sana kwenye vyombo vya habari na kila anapopewa mic., lazima ataje jina la Samia Suluhu Hassan kama kibwagizo cha shairi...

JAMAA ANAPIGA KAZI,,MUSOMA MJINI MAJI SAFI TELE TUNAKARIBIA 100%,,COVARAGE na ata Idara ya Maji safi na taka,,(muwasa)awasumbui kuvutiwa bomba km unaitaji,chap Maji yanaingia,,AWESO mchapakazi
 
Huyu Waziri, anajionesha sana kwenye vyombo vya habari na kila anapopewa mic., lazima ataje jina la Samia Suluhu Hassan kama kibwagizo cha shairi...
Morogoro maji yanatoka ya kijani Kama chama Chao☘️ muda mwingine yanatoka Yana udongo, yaan hayafai hata kumpa kuku anywe
Dodoma maji Yana chumvi mpaka Yanachana Koo.

Moshi ndio mkoa pekee nilikaa maji yake ni saf na salama.
 
Back
Top Bottom