Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Atakuwa alikwisha jiandaa kisaikolojia...
Its a game of thrones! Leo yuko huyu, kesho yuko yule...
Hizi assumption mimi huwa siamini kama mpo serious wakuu, unakuta mtu labda alikuwa waziri kwa miongo kadhaa (mf Lukuvi) kisha akitumbuliwa tuamini kwamba atakuwa anapigwa mionzi ya jua au kushika bomba la daladala kama sisi?[emoji23]

Huyu Ally Happy pamoja na mahela waliyochota enzi za baba yao wakiwa na akina Sabaya na Makonda, watapigwaje mionzi ya jua? We si unaona life la Makonda bado anakula raha tu.

Me siamini kama kuna MWANA-CCM anaeweza kushika nyazifa za miaka kafhaa afu akatika masikini.
 
Kwa wa Mara (Team Mkemia) ilikuwa ni Suala la muda tu na bahati nzuri hata Mhusika alishaandaliwa Kisaikolojia zamani mno kuwa ataondolewa.

Kwa wa Kagera (Team Mkemia) huyu ilikuwa aondolewe tokea mwaka jana ila kutokana na kuwa Mjeda tena Brigedia umakini ulitakiwa Kwanza kabla ya Kumuondoa na kuna uwezekano pia akateuliwa kuwa Balozi siku si nyingi na 'Film Director' wetu.

Hata hivyo huyu kwakuwa ni Poti wangu (mwana Mkoa wa Mara) atanisamehe kwa huu Ukweli ambao nitampa hapa.

Poti wangu Afande (uliyekuwa Kagera) Wewe ni Mchapakazi na Mtu Mweledi mno, ila sijui ni kwanini hutaki Kubadilika na tabia yako ya kupenda Pombe (Mkude) ambayo ndiyo inakuharibia kila mara na kutokana na lile Kosa lako ulipokuwa Jeshini baada ya Kuteuliwa na Mkemia mshukuru sana Mtemi (Film Director) kwa kuendelea Kukubakisha mpaka Leo hii alipoamua 'Kukubwaga' mazima.

Afande na Poti wangu Ile Kasoro yako nyingine sitoisema hapa kwani hata Mimi naipenda mno na ndiyo Udhaifu wangu Mkuu.

Na hata ulivyopelekwa tu kwa Watani zetu Wahaya (Mkoani Kagera) na jinsi ninavyowajua Wahaya (hasa Maua yao yalivyo) nilijua tu kuwa huwa 'Watakukoma' na utakuwa 'unazikeshea' Kunakotukuka na kwa ninavyokujua Poti wangu nina uhakika imekuwa hivyo.

Poti Afande nakusubiri Kibaha au Mbweni au pale Kijiweni Kwako Mbezi Beach au kule Kigamboni kwa Rafiki yako Mkubwa Carlos (Mtoto wa aliyekuwa Boss wako JKT) ili unipe 'direction' ya wapi tunaenda 'Kuzimua' huku tukipata na 'Kichuri' chetu na tukiyaangalia 'Maua' tunayoyapenda.

Kwa Kafulila hapa hata nisiwe Mnafiki huyu pamoja na kwamba alikuwa Upinzani na alipendwa mno na Mkemia Binafsi kama GENTAMYCINE sikuona 'Potential' yake katika Uongozi na nilishangazwa zaidi nilipoona Kalamba Uteuzi katika Utawala wa Mkemi na bado tena 'Film Director' nae kwa Uwoga au Kujishtukia akaendelea Kumuamini na Kumteua mpaka hivi leo alivyomla Kichwa mazima.

Kwa akina Mtaka na Msando (ambao nanyi pia ni Team Mkemia) anzeni Kujiandaa Kisaikolojia mapema kama alivyofanya Mwenzenu wa Mara kwani nanyi mpo katika Rada za 'Kufyagiwa' mazima japo Mmoja ni RC na mwingine ni DC.
 
Uzuri wa serikali ukipigwa Chini unamshukuru Rais na unaendelea na maisha mengine..

Next time utakuja kuteuliwa tena kama Chalamila..

Kafulila kilichomponza ni kuwakazia wapigaji wa ccm maana hao wakuu wa Mikoa huwa ni mapambio ya CCM.
 
Maskini. Ndio kwanza nyumba yake iko kwenye lenta! Sijui atakuja kupanga upade mmoja Sinza! [emoji3][emoji3][emoji3]
Miongoni mwa vijana walioletwa kwenye tasnia na the late, ni Makonda tu ndiyo alijua kusomba mali za kutosha. Kama ni for living decently tu, huyu atakula hela mpaka ataziacha.

Sabaya naye alipiga hela, sema ndo hivyo alinasa, sitaki kuamini kama Ally Happy alikuwa boya kiasi hicho.
 
Atakuwa alikwisha jiandaa kisaikolojia...
Its a game of thrones! Leo yuko huyu, kesho yuko yule...

Leo uko kwenye kiyoyozi, kesho uko kwenye mionzi, unapigwa na jua.
Leo unafunguliwa mlango wa V8, kesho unashika bomba kwenye DCM la Gongo la Mboto.
Aisee yani uwe mkuu wa mkoa alafu uje kupigwa vumbi,ina maana ulikua hujajipanga maisha baada ya ukuu wa mkoa?😂
 
Chalamila ndani ya nyumba!!
CCM huwa hawasahauliani mkuu, wanapeana ulaji kila inapobidi. Hawa wote unaowaona wamewekwa nje ya track, mbeleni kidogo utawaona kwenye system tena.

Mpaka kizazi kinazeeka ni mwendo wa kubadilishana madaraka tu.
 
Back
Top Bottom