Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa nchini huku akiingiza majina mapya tisa akiwemo Albert Chalamila aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Wakuu wa mikoa 10 wamebaki kwenye vituo vyao vya kazi vya awali huku 7 wakihamishwa.

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Hapi ameachwa katika orodha mpya, dhahma hiyo pia imewakumba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila.

Pia aliyekuwa katibu mkuu wa Bunge na baadae kupewa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai nae ametemwa.

======

Mkeka wa wakuu wa mikoa.
View attachment 2306342View attachment 2306343
View attachment 2306345
Huyu Chalamila ni yule aliyefukuzwa kazi mwaka jana akaanza kuimba imba mapambio au ni mwingine?
 
Raisi amefanya teuzi, mikoa yote ya Tanzania Bara ipo kwenye mkeka, kasoro Mkoa wa Simiyu tu.

Tayari watu wana assume Kafulila kaliwa kichwa, pamoja na Mkoa wake kitoonekana kwenye huo mkeka.

Zuhura Yunus weka sawa mambo yako, makosa madogo madogo yanajirudia sana, kila siku na jambo jipya.
 
Hata wakiwemo wana kusaidia nini? Low mind
 
Soma hiyo taarifa ya uteuzi kipengele cha tisa. (9).

Kuna mkuu wa mkoa mpya.
 
Aje huku nimfundishe kubeti. Maisha lazima yaendelee.

Hata sie tuliwahi kuwa kwenye viyoyozi.

Siku naambiwa paki hapa gari letu, ajira ikaisha nilidhani ndio mwisho wa Dunia.

Leo hii Mungu si Athumani, napandisha kaghorofa, maisha yanaendelea kama kawa.

So, waliopigwa chini, wajue kabisa kuwa maisha lazima yaendelee...
Hata wasipotaka kujua njaa na kupoteza influence kutawajulisha.
 
Lile agizo la Mkuu wetu wa mkoa wa Mtwara kuwashughulikia wale wajinga waliosambaza picha za watoto wetu( Mwenyezi Mungu Awarehemu) litakuwaje Sasa!?
 
Back
Top Bottom