Rais Samia ahutubia taifa leo Agosti 22, 2022. Ametoa wito na kuwasihi Watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa

Ni vyema kukausha Marijuana kabla ya kuvuta.
 
Kwahiyo saa 6 kuna mtu atakuja kubisha hodi kwangu eti anihesabie?
 
Nina mashaka na upeo wako katika mambo.
Mimi nimesema sio rais?
Nimesema asisikilizwe?

Nilichofanya, nimei rate hotuba yake na tangazo tu la sensa.
Hotuba hubeba content nzito yenye hisia mchanganyiko kwa audience na hata mtoa hotuba.

Samia kikatiba ni rais kamili lakini hana presidential materials.

1. Hana ufahamu wa mambo mengi
2. Hana ushawishi kama mkuu wa nchi
3. Poor leadership strategic
4. Hana sauti ya kiuongozi
5. Anapelekeshwa na kikundi cha watu wachache.
6. Jinsia yake inamfanya akose kujiamini anaongoza nchi kama kiongozi wa UWT

NOTE ukichukizwa na mawazo yangu saga chupa shushia na soda nitalipa mimi..
dudus
 
Naona unaandika tu mradi umeandika, yaani kwa upeo wako unazani Ni Jambo gani ambalo mh Rais Hana ufahamu nalo, kikundi gani kinacho mpelekesha mh Rais, naona hata kukujibu hustahili kujibiwa maana umeongea bila adabu na heshima kwa mh Rais, umeandika Kama mtu ambaye Hana malezi ya wazazi wake
 
Tatizo lenu mmekaririshwa na kulelewa kipuuzi kwamba raisi yuko sahihi muda wote na hawezi kukosea au kuwakosea wengine ,rais hatakiwi kukosolewa , mnamuona rais kama mungu halafu mnasahau kuwa rais ni binadamu kwa asili ambaye anaweza kuwa na mapungungu mengi tu ya kiubinadamu.
 
Unaweza ukajenga hoja nzuri na ukaeleweka, lakini siyo mtu unatumia maneno ya dharau na kejeli kwa mh Rais, hiyo haikubaliki popote, Tuwe na heshima na adabu kwa mh Rais wetu
 
Nina mashaka na upeo wako katika mambo.
Mimi nimesema sio rais?
Nimesema asisikilizwe?

Nilichofanya, nimei rate hotuba yake na tangazo tu la sensa.
Hotuba hubeba content nzito yenye hisia mchanganyiko kwa audience na hata mtoa hotuba.

Samia kikatiba ni rais kamili lakini hana presidential materials.

1. Hana ufahamu wa mambo mengi
2. Hana ushawishi kama mkuu wa nchi
3. Poor leadership strategic
4. Hana sauti ya kiuongozi
5. Anapelekeshwa na kikundi cha watu wachache.
6. Jinsia yake inamfanya akose kujiamini anaongoza nchi kama kiongozi wa UW
Ndugu Mtanzania unayeishi #MAKONDOO COUNTRY#
Hakuna mahali nimejaribu hata kumvunjia heshima rais wangu mpendwa bali nimetea sifa alizo nazo.
Kuna vitu mtu hupewa na Mungu huwezi kuvitavuta kwa akili zako...mfano uongozi ni kipawa toka kwa Mungu, unaweza kufanya kazi ya kuongoza lakini usiwe kiongozi
 
Akili kashikiwa na mwigulu huyo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Jamani niuweni Niueniiii......
Man U leo wamekaza kwenye mkesha wa sensaa...
 
Nchi yetu itajengwa na sisi watanzania,Sasa wewe unataka Nani atujengee nchi yetu tusipokuwa tayari kuijenga wenyewe kwa mikono yetu wenyewe, au unataka Nani abebe mzigo na wajibu wetu wa kuijenga nchi yetu

Pesa zinapigwa hovyo na watu wachache maisha yamekua magumu matozo kila kona maendeleo hayaonekani. Hii nchi anaijengea wapi?
 
Mh Rais yupo Sanaa tu Hadi 2030. Watanzania bado tunamhitaji Sanaa kuweza kututumikia maana ameonyesha uwezo mkubwa Sana ndani ya muda mfupi, tumeridhishwa na utendaji kazi wake ulio tukuka
Ndio ameonesha uwezo ila ni wa "chini" na ndio uwezo wake ulipoishia.

Kwanza alichaguliwa na nani huyu?

Viongozi walioingia madarakani bila kuchaguliwa wana tabia ya kutojali na viburi.
 
tumeanza kuhesabiwa leo trh 23 saa sita usiku......kazi inaendelea

Tuko tayari kusensabika.
sensa kwa maendeleo yetu na vizazi vyetu
 
Ni kweli lengo la sensa ni kuiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo iwe shule, miundombinu kama barabara na huduma zingine za jamii.

Lakini pia raisi amesema kuwa hii ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya Uhuru lakini pia ni baada ya miaka 61 ya uhuru wa nchi yetu.

Ieleweke pia kuwa sensa ya idadi ya watu na makazi haiitaji namba za simu kwani hiyo yaweza kuweka hisia kuwa serikali yaingiza mkono wake zaidi kutaka kuiweka jamii chini yake na kuibinya zaidi kwa kuifuatlilia khasa kwenye masuala kama tozo na mengine.

Taarifa za jina la mtu, na watu anoishi nao pamoja na taarifa za nyumba na jengo zatosha sana.

Jambo jingine ni kwamba ni muhimu ofisi ya takwimu ikaweza wazi taarifa za sensa katika tovuti yake ili kutoa elimu zaidi ya maana ya sensa na umuhimu wake.

Ni jambo la umakini kueleza jinsi sensa inavyotengenezwa, masuali yake yaandaliwa vipi, na matumizi ya taarifa zote za sensa na utunzaji wa kumbukumbu za sensa.

Ni dhahiri kwamba licha ya miongo sita ya ukusanyaji wa taarifa za sensa nchini bado serikali haijaweza kuiimarisha idara ya takwimu kwa kuiwezesha kwa nyenzo muhimu za kiteknolojia ili iweze kuitumia ipasavyo idara hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Hii yaweza kuisaidia idara hii kuandaa zoezi la sensa kwa njia pia ya mtandao ambapo mtu aweza kujaza taarifa zake popote pale alipo bila kumsubiri karani wa sensa.

Njia ingine ni ile ya posta ambapo fomu za sensa zaweza kuwekwa tayari kwa wananchi kuzichukua katika ofisi za serikali za mitaa ni kisha baada ya kujaza mbele ya maofisa pale fomu hizio hutumwa na ofisi hiyo kama ambavyo zoezi la kuomba pasi ya kusafiria linavofanywa.

Taarifa za sensa zikiwa sahihi na zilizojidhihirisha, mikoa, wilaya na kata zaweza kabisa kutumia taarifa hizo kuhakikisha barabara na mitaa zajengwa, mataa ya barabararani na maji yapatikana katika kila kila nyumba, na hiyo ni mifano michache.

Ni jambo jema kwa kufanya sensa ya sita nchini na miaka 61 baada ya uhuru, lakini huu ni wakati wa kuhakikisha sensa ya safari hii inaleta tija inotarajiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…