ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Unadhani hata wakiachika wanatoka bure!?Wanawekeza nini mkuu? Kama ndoa ni uwekezaji kusingekuwa na wanawake wanaoachika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unadhani hata wakiachika wanatoka bure!?Wanawekeza nini mkuu? Kama ndoa ni uwekezaji kusingekuwa na wanawake wanaoachika.
Unaelewa maana ya two consenting adultKwani wanatokaje mkuu? Si wengi wao tuanawaona wakiachika wanabeba mabakuri, masahani na makochi? Hiz nazo ni mali?
Mama Samia hatoweza fanya lolote kwa sababu tatizo hili linaendekezwa sana na waze wa Kiislam. Mtu ana mshipa eti anakwenda kuoa katoto ili kawe kanachezea mshipa wake usiku.Jambo wakuu!
Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa. Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.
Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na sasa mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa hivi karibuni na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe. Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.
Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono. Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.
Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio. Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.
Nawasilisha.
Kwani ni under 18?Kula ni sawa wazee kuwaoa mabinti wadogo, wanawaharibia future
Mrema anaswali msikiti gani?Mama Samia hatoweza fanya lolote kwa sababu tatizo hili linaendekezwa sana na waze wa Kiislam. Mtu ana mshipa eti anakwenda kuoa katoto ili kawe kanachezea mshipa wake usiku.
Mengi alikuwa mshamba wa mademu, Mrema ni muhuni tu, usimtilie maananiMrema anaswali msikiti gani?
Mengi nae alikuwa ni muislam?
Au nawewe umeolewa na Mzee?
Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
Kabisa...unatakia ukiwa miaka yako 70 unavuta pisi ya miaka 28 hivi unatulia nayo iwe ina kuna mbupuz zako. Tena ikiwezekana uwe nao wawili... hilo ni jambo la kheri mzee acha hizo! Muhimu kupita mule mule.
𝐍𝐚𝐨𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐰𝐞𝐦𝐞𝐤𝐮𝐬𝐡𝐚𝐦𝐛𝐮𝐥𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤�𝐮𝐰𝐚 𝐮𝐦𝐞𝐢𝐭𝐚𝐣𝐚 𝐝𝐡𝐚𝐦𝐛𝐢 𝐲𝐚 𝐬𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐭𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐢𝐚𝐛𝐮𝐝𝐮, 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮 𝐚𝐭𝐮𝐬𝐚𝐦𝐞𝐡𝐞 𝐭𝐮 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐬𝐢 𝐬𝐚𝐰𝐚 𝐦𝐭𝐨𝐭𝐨 𝐤𝐮𝐮𝐨𝐧𝐚 𝐮𝐜𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐛𝐚𝐛𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐧𝐚 𝐭𝐞𝐧𝐚 𝐧𝐢 𝐥𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐣𝐮𝐢 𝐭𝐮,Siku wakitaka kuoa watamuoa nani wakati wazee watakuwa wameishaoa wote? Acha roho mbaya mkuu.
Hakuna kushinikizwa ikiwa wamefikia umri wa kuolewa, ina maana wanatambua wanachokifanya.........Mkuu nimesema kwamba wengi wa vigoli hawa hurubuniwa na wazee pamoja na wazazi wao kwa sababu ya ufukara; wengi hawaolewi kwa kupenda bali kwa mashinikizo y wazaz/walezi wao. You get me right?
Mkuu, utawanyima watu haki zao wakati hawavunji sheria yoyote (kama binti ni above 18)Mkuu hapa hatuongelei imani ya mtu bali tunaongelea sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971. Tunaomba irekebishwe ili kuwazuia wazee wasiwaoe mabinti wanaolingana na watoto/wajukuu zao. Umenipata?
kuna mzee mmoja alinambiaJambo wakuu!
Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa.
Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.
Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na sasa mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa hivi karibuni na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe.
Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.
Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono.
Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.
Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio.
Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.
Nawasilisha.
Huu uzi ni mujarabu kwa kuwa hakuna dislike hata moja kuonyesha kuwa watu hawajanielewa.Hivi unajua muasisi wa Imani yake alioa binti wa umri gani?!!!
Huu uzi ulianzisha jana jioni, hadi muda huu Una views zaidi ya 1,200 na posts zaidi ya 90, lkn bado hakuna like hata moja!
Maana'ake wadau hawaafikiani na maoni yako!
Watu wengi hawajui laana iliyojificha kwenye kuona uchi wa mzazi wako. Na hii laana ndiyo inatutafuna watanzania hadi leo. Sijui tunakwama wapi. 😳 😳 😳𝐍𝐚𝐨𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐰𝐞𝐦𝐞𝐤𝐮𝐬𝐡𝐚𝐦𝐛𝐮𝐥𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤�𝐮𝐰𝐚 𝐮𝐦𝐞𝐢𝐭𝐚𝐣𝐚 𝐝𝐡𝐚𝐦𝐛𝐢 𝐲𝐚 𝐬𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐭𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐢𝐚𝐛𝐮𝐝𝐮, 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮 𝐚𝐭𝐮𝐬𝐚𝐦𝐞𝐡𝐞 𝐭𝐮 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐬𝐢 𝐬𝐚𝐰𝐚 𝐦𝐭𝐨𝐭𝐨 𝐤𝐮𝐮𝐨𝐧𝐚 𝐮𝐜𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐛𝐚𝐛𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐧𝐚 𝐭𝐞𝐧𝐚 𝐧𝐢 𝐥𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐣𝐮𝐢 𝐭𝐮,