Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Mkuu naona mzee lyatonga kapita na mbebez wako kwa kasi ya kimbunga, vumilia tu mkuu huwezi kumpangia mtu kuoa ikiwa hao mabinti wameshafika umri wa kuolewa.....
 
Mkuu naona mzee lyatonga kapita na mbebez wako kwa kasi ya kimbunga, vumilia tu mkuu huwezi kumpangia mtu kuoa ikiwa hao mabinti wameshafika umri wa kuolewa.....
Mkuu nimesema kwamba wengi wa vigoli hawa hurubuniwa na wazee pamoja na wazazi wao kwa sababu ya ufukara; wengi hawaolewi kwa kupenda bali kwa mashinikizo y wazaz/walezi wao. You get me right?
 
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa. Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.

Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na sasa mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa hivi karibuni na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe. Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.

Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono. Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.

Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio. Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.

Nawasilisha.​
Kiongozi wa majuha
 
Kichaa huyo
Kweli huyo jamaa ni chizi aisee. Ina maana kweli haoni tatizo la wazee kuwakatisha masomo mabinti na kuwaoa huku wakizidi kudidimiza jitihada za mama Samia kuwasomesha watoto wa kike? Tukawafiche wapi mabinti zetu sie?
 
Siku wakitaka kuoa watamuoa nani wakati wazee watakuwa wameishaoa wote? Acha roho mbaya mkuu.
Hao wazee wapo wangapi mpaka waoe mabinti wote ?....acha ramli chonganishi
 
Kiongozi wa majuha
Juha ni wewe mwenyewe unayeacha kuwaoa wakubwa wenzako badala yake unawaoa mabinti wenye umri sawa na wajukuu au mabinti zako. Umelaaniwa wewe umbwa sio bure!
 
Hao wazee wapo wangapi mpaka waoe mabinti wote ?....acha ramli chonganishi
Hata kama hawawaoi wote lakini wana disturb equilibrium ya wasichana mtaani. Wewe hukwenda shule kumbe mkuu?
 
Ibrahimu mwenyewe alioa kijakazi wake mdogo kabisa na still Mungu alimpenda sembuse Lyatonga
Mkuu usitumie hadithi za uwongo za Agano la Kale kuhalalisha uhalifu.
 
Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono. Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao
Hivi unajua muasisi wa Imani yake alioa binti wa umri gani?!!!

Huu uzi ulianzisha jana jioni, hadi muda huu Una views zaidi ya 1,200 na posts zaidi ya 90, lkn bado hakuna like hata moja!
Maana'ake wadau hawaafikiani na maoni yako!
 
Hivi unajua muasisi wa Imani yake alioa binti wa umri gani?!!!
Mkuu hapa hatuongelei imani ya mtu bali tunaongelea sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971. Tunaomba irekebishwe ili kuwazuia wazee wasiwaoe mabinti wanaolingana na watoto/wajukuu zao. Umenipata?
 
Sasa wewe unataka nani aingilie kati mkuu? Basi wewe lichukue ulifanyie kazi.
Tatizo lako unafikiri mwanaume akizeeka dushe linakuwa kubwa. On contrary anapokuwa mzee dushe linasinyaa na kuwa dogo. Ndiyo maana mabinti wadogo huwa wanawapenda mababu. Kwa kukuelimisha dushe linakua hadi mtu akifikisha miaka 35, hapo huanza kusinyaa. Nadhani utakuwa umeelewa na wivu wa kichura na maji ….yangu yangu yangu…. Wakati hawezi kumaliza maji ya kisima utakuwa umekutoka
 
Kweli huyo jamaa ni chizi aisee. Ina maana kweli haoni tatizo la wazee kuwakatisha masomo mabinti na kuwaoa huku wakizidi kudidimiza jitihada za mama Samia kuwasomesha watoto wa kike? Tukawafiche wapi mabinti zetu sie?
Hv unawafanya hao mabinti ni wajinga!!??
mifano yote uliyotoa hao mabinti ni wawekezaji...
wanazitazama fursa kuliko uonavyo
 
Hv unawafanya hao mabinti ni wajinga!!??
mifano yote uliyotoa hao mabinti ni wawekezaji...
wanazitazama fursa kuliko uonavyo
Wanawekeza nini mkuu? Kama ndoa ni uwekezaji kusingekuwa na wanawake wanaoachika.
 
Back
Top Bottom